Wadau, amani iwe kwenu.
Nimefuatilia sana mjadala unaoendelea bungeni hususani hoja iliyotolewa na serikali juu ya kutorusha Live baadhi ya mijadala bungeni. Hakika iam totally confused. Ukisikia michango ya wabunge na baadhi ya wadau humu mitandaoni hakika unakuja kugundua kuwa ama hii hoja imepokelewa kisiasa ama kuna watu wameamua kujivika ujinga. Nasema haya kutokana na jinsi michango ya watu ilivyo.
Ukisikiliza na kuangalia kwa jicho pevu michango hiyo utagundua kuwa kweli tuna safari ndefu. Wapo wanaoamini kuwa Serikali haitaki mikutano ya bunge irushwe live kwa sababu haitaki wananchi waone mijadala inayoendelea bungeni kwa lengo la kuwakandamiza wapinzani. Wengine wanasema kuwa serikali inataka kuedit kwanza michango ya wabunge ndipo iwafikie wananchi. Wengine wanasema serikali ni waoga sana na hivyo wanaogopa michango ya wapinzani.
Hakika hoja zote hizi ni za kijinga. Kwanini nasema hivyo kwasababu serikali haijapiga marufuku kuoneshwa live kwa vikao vya bunge. TBC1, Star TV na Azam TV wamekuwa wakirusha hewani kipindi cha maswali na majibu bungeni. Then Star TV na Azam TV kupitia Channel ya Xtra wamekuwa wakirusha moja kwa moja mijadala yote inayoendelea bungeni.
Hakika nimestaajabu sana kuona wabunge wetu wamekuwa wakitoa mapovu kwa mambo yasiyo na tija as if sisi wananchi hatujui nini kinaendelea. Serikali imekuwa very clear kueleza kwa nini wamechukua maamuzi hayo. Hivyo basi wapinzani kuweni wawazi. Msitudanganye sisi wananchi.