Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,817
Hoja sio bunge kurushwa live. Hoja ni bunge kurushwa live na Televisheni ya Taifa. Tunapoita Televisheni ya Taifa ina maana ya kuwa inaendeshwa na kodi ya wananchi wa Tanzania. Na moja kati ya haki za kikatiba ni ile ya uhuru wa kupata ama kutafuta habari. Sasa unapotaka kusitisha kurusha moja kwa moja ni kuwanyima haki watanzania.
Hebu labda nikuulize, hakimu anayehukumu wahalifu kifungo cha miaka kadhaa jela, endapo akatenda kosa na kupewa nafasi/uhuru wa kujihukumu mwenyewe je atajihukumu ama atajiweka huru?
Kinachoenda kutokea ni kuwa, serikali kupitia TBC haitakuwa tayari kuona inaaibika mbele ya wananchi wake pale wanapoboronga kwa kurusha matangazo yaliyorekodiwa eti kuonesha waliopoboronga. Lazima wataonesha pale walipopatia na kusifiwa. Pia jiulize baada ya maswali na majibu, kipindi cha bunge kinaendelea kwa saa 5 (saa 5 hadi saa 7 na saa 11 hadi saa 2 usiku) sasa hebu niambie muda wa saa moja utatosha kuonesha yale ya muhimu yaliyojiri?
Kuhusu chaneli binafsi kuonesha moja kwa moja (Star Tv na Azam TV) sio sababu zenye mashiko za kufanya TBC kupata uhalali wa kutoonesha moja kwa moja. Hii ni kwa sababu zifuatazo:
1. Vyote hivyo ni vyombo binafsi kwahiyo wakiamua saa yeyote kuonesha vipindi vingine badala ya bunge hakuna wa kuwauliza. Ila TBC wakikata matangazo wataulizwa.
2. Star Tv tunaifahamu mrengo wake wa kisiasa. Wakati wowote wanaweza kushinikizwa na kutorusha moja kwa moja. (Hili liko wazi hata umiliki wake)
3. Si watu wote wenye uwezo wa kuipata Azam TV. Tunafahamu Azam Tv inapatikana kwenye visimbuzi vya Azam Tv pekee. Mpaka leo kuna baadhi ya watu wanatumia madish ya LNB na wengine visimbuzi vya Star Times, Zuku na vingine. Hivyo kuipata Azam Extra ni vigumu.
Hivyo basi suluhuhisho pekee ni kuiacha TBC ambayo ni mali ya kila Mtanzania ioneshe live.
Magnesium
Lakini sisi wananchi tuliowengi tumekubaliana na uamuzi wa Serikali yetu na kwamba TBC yetu isirushe Bunge muda wa kazi ili tufanye kazi, kwanza ndiyo tulioiomba ifanye hivyo!