TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Hoja sio bunge kurushwa live. Hoja ni bunge kurushwa live na Televisheni ya Taifa. Tunapoita Televisheni ya Taifa ina maana ya kuwa inaendeshwa na kodi ya wananchi wa Tanzania. Na moja kati ya haki za kikatiba ni ile ya uhuru wa kupata ama kutafuta habari. Sasa unapotaka kusitisha kurusha moja kwa moja ni kuwanyima haki watanzania.

Hebu labda nikuulize, hakimu anayehukumu wahalifu kifungo cha miaka kadhaa jela, endapo akatenda kosa na kupewa nafasi/uhuru wa kujihukumu mwenyewe je atajihukumu ama atajiweka huru?

Kinachoenda kutokea ni kuwa, serikali kupitia TBC haitakuwa tayari kuona inaaibika mbele ya wananchi wake pale wanapoboronga kwa kurusha matangazo yaliyorekodiwa eti kuonesha waliopoboronga. Lazima wataonesha pale walipopatia na kusifiwa. Pia jiulize baada ya maswali na majibu, kipindi cha bunge kinaendelea kwa saa 5 (saa 5 hadi saa 7 na saa 11 hadi saa 2 usiku) sasa hebu niambie muda wa saa moja utatosha kuonesha yale ya muhimu yaliyojiri?

Kuhusu chaneli binafsi kuonesha moja kwa moja (Star Tv na Azam TV) sio sababu zenye mashiko za kufanya TBC kupata uhalali wa kutoonesha moja kwa moja. Hii ni kwa sababu zifuatazo:

1. Vyote hivyo ni vyombo binafsi kwahiyo wakiamua saa yeyote kuonesha vipindi vingine badala ya bunge hakuna wa kuwauliza. Ila TBC wakikata matangazo wataulizwa.
2. Star Tv tunaifahamu mrengo wake wa kisiasa. Wakati wowote wanaweza kushinikizwa na kutorusha moja kwa moja. (Hili liko wazi hata umiliki wake)
3. Si watu wote wenye uwezo wa kuipata Azam TV. Tunafahamu Azam Tv inapatikana kwenye visimbuzi vya Azam Tv pekee. Mpaka leo kuna baadhi ya watu wanatumia madish ya LNB na wengine visimbuzi vya Star Times, Zuku na vingine. Hivyo kuipata Azam Extra ni vigumu.

Hivyo basi suluhuhisho pekee ni kuiacha TBC ambayo ni mali ya kila Mtanzania ioneshe live.

Magnesium

Lakini sisi wananchi tuliowengi tumekubaliana na uamuzi wa Serikali yetu na kwamba TBC yetu isirushe Bunge muda wa kazi ili tufanye kazi, kwanza ndiyo tulioiomba ifanye hivyo!
 
Pasco haya yote serikali na TBC wanayajua kindakindaki ,shida ni kwamba Nchi imeamua kuendesha kila jambo kama tupo kwenye kampeni za uchaguzi ,ila hili litawatokea serikali puani muda sio mrefu
 
Mtazamo wangu, TV zote zingerusha vipindi vya bunge usiku, baada ya watu kufanya kazi za kujenga taifa. Sababu kubwa watanzania hawafanyi kazi wanatazama bunge, mbaya zaidi wabunge wenyewe wanaotazamwa wanaongea na kufanya vitendo vya ovyo kabisa. Hii inapelekea Tanzania kuwa nchi ya siasa muda wote badala ya kujenga nchi.
 
kwa hiyo toka uzaliwe huu ndo mwaka wako wa kwanza kufanya kazi???,alafu usi claim kuwa kazi zinafanyika mchana tu kama mawazo yako yanakutuma kuwa tv zitafanya watu wasifanye kazi basi zingekuwa zinarusha vipindi vyao usiku tu
Yaelekea wewe ni mmoja was watu ambao hawajui kwamba MAENDELEO popote pale huletwa na kufanya KAZI kwa bidii na maarifa. Kama maarifa kwako ni kuangalia TV wakati wa kazi kwa kisingizio chochote kile ni ujuha!
 
Kweli wewe unafikiri kwa ma.ta.k..o Tuambie elimu yako ili tukusamehe unamaanisha watu hawafanyi kazi kwa sababu ya kuangalia tv hasa vipindi vya bunge???? Watanzania sio wajinga kama unavyofikiria
 
Uamuzi WA nape juu ya tbc1 ni pigo kwa ukawa,kwa sababu ukawa walishazoea kujipatia umarufu kupitia drama wanazozifanya wakati WA bunge,vyanzo vyangu vya habari vinasema drama zinazofanyika bungeni zilipangwa kwa ajili ya kutengeneza attetion kwa wanachama,uamuzi WA nape ni Tishio kwa ukawa ndo maama walikua radhi hata kurusha ngumi kupinga uamuzi huo ,hata style ya kutoka nje ya bunge si kwa ajili ya kukutetea maslai ya wanachama la hasha ni kwa ajili ya kuwambia wananchi kua tupo

Maskini chadema ndo inazikwa lasmi
 
Kama unajijua kichwa cha panzi kunywa fanta bangi waachie wenye vichwa vyao naona asubuhi asubuhi kitu kimeshausika ngoja twende makanisani tukakuombee
 
Uamuzi WA nape juu ya tbc1 ni pigo kwa ukawa,kwa sababu ukawa walishazoea kujipatia umarufu kupitia drama wanazozifanya wakati WA bunge,vyanzo vyangu vya habari vinasema drama zinazofanyika bungeni zilipangwa kwa ajili ya kutengeneza attetion kwa wanachama,uamuzi WA nape ni Tishio kwa ukawa ndo maama walikua radhi hata kurusha ngumi kupinga uamuzi huo ,hata style ya kutoka nje ya bunge si kwa ajili ya kukutetea maslai ya wanachama la hasha ni kwa ajili ya kuwambia wananchi kua tupo

Maskini chadema ndo inazikwa lasmi
Tulia uandike vizur kwani unakimbizwa ?? Jifunze kuumba herufi...
 
hivi bado upo Namtumbo wewe?????
naona unaendeleza ukilaza wako,..
hivi kwann hubadilikagi wewe ndugu yangu..?????
unanini.........
 
uamuzi wa nape ni pigo kwa watanzania wote wapenda uwazi na uwajibikaji kwa wabunge wao waliowachagua bila kujali vyama vyao. lakini uamuzi huu ni furaha kwa wabunge wote walioingia bungeni kwa ajili ya maslahi binafsi na familia zao. maana wataingia bungeni kwa ajili ya noti na hawatawasilisha matatizo ya wananchi wao serikalini. wengine wanaweza toroka baadhi ya siku na bila umma kujua kama wako bungeni ama hawapo. uamuzi wa nape unaiondoa ccm mioyoni mwa wapenda demokrasia na haki za kupata habari kwa wakati....
 
Inaelekea mtoa post kalala anaiwazia ukawa na kukurupuka kutoa post
 
Uamuzi WA nape juu ya tbc1 ni pigo kwa ukawa,kwa sababu ukawa walishazoea kujipatia umarufu kupitia drama wanazozifanya wakati WA bunge,vyanzo vyangu vya habari vinasema drama zinazofanyika bungeni zilipangwa kwa ajili ya kutengeneza attetion kwa wanachama,uamuzi WA nape ni Tishio kwa ukawa ndo maama walikua radhi hata kurusha ngumi kupinga uamuzi huo ,hata style ya kutoka nje ya bunge si kwa ajili ya kukutetea maslai ya wanachama la hasha ni kwa ajili ya kuwambia wananchi kua tupo

Maskini chadema ndo inazikwa lasmi
Ubongo wako ni mwepesi mithili ya viaz mviringo,sijui utakua mhusika mwenyewe.hizi ni cheap politics in 30yrs ago,ni matokeo ya kubebwa na majina ya wazaz pasipo na sifa.I due respect mwigulu umefika hapo kwa political will na wengne waliofika hapo kwa majina ya wazaz wao,ndio mana wanafanya maamuzi ya kichekechea.
 
Ccm imewaharibu sana watanzania walio wengi. Hali hii inaonyesha hata waziri wa kilimo na chakula naye akitoa tamko bungeni la kutaka watanzania wale mlo mmoja tu kwa siku mtasifia na kusema pigo kwa Chadema.
 
Uamuzi WA nape juu ya tbc1 ni pigo kwa ukawa,kwa sababu ukawa walishazoea kujipatia umarufu kupitia drama wanazozifanya wakati WA bunge,vyanzo vyangu vya habari vinasema drama zinazofanyika bungeni zilipangwa kwa ajili ya kutengeneza attetion kwa wanachama,uamuzi WA nape ni Tishio kwa ukawa ndo maama walikua radhi hata kurusha ngumi kupinga uamuzi huo ,hata style ya kutoka nje ya bunge si kwa ajili ya kukutetea maslai ya wanachama la hasha ni kwa ajili ya kuwambia wananchi kua tupo

Maskini chadema ndo inazikwa lasmi
Haaaa haaaa Sasa Drama wanazofanya zipi?kuwaambia mpango wa maendeleo wamekosea?Kuifanya Serikali iondoe hoja yake na kwenda kujipanga upya?Kipi Ni drama?Lets be great thinker na tusiwe tu mashabiki
 
Back
Top Bottom