Matumizi mengine ya kijinga ni kulipa ruzuku kwa vyama vya siasa ambavyo vina zaidi ya miaka 20. Wafute hizi ruzuku vyama viendeshwe kwa ada na michango ya wanachama.
huku tunakoelekea sasa sio kwema kabisa. Hakuna kitu kibaya kama kuwanyima haki ya habari wananchi kkatika karne hii ya 21. Hili wasipoliangalia ndio litaiangusha CCM vibaya zaidiNi maafa, tena makubwa sana. Waziri Nape kaleta kauli ya serikali Bungeni kuwa maonyesho ya moja kwa moja Bungeni hayatakuwepo tena eti ni gharama na TBC1 hawana uwezo wa kugharamia shilingi Bil 4 kwa mwaka.
Dalili za kutoruhusu mijadala hiyo hasa kwa sasa wanapoijadili hotuba ya Rais ni kuwa hawataki wananchi waone wabunge wanavyo ichambua na kuiagiza serikali ifanye nini. Jee zuio hili lina baraka za Rais Magufuli?
Mbona yeye anapotumbua majipu anapenda kupata coverage ya Tv na Radio na awe hataki serikali yake kuwa kikaangoni watu waone? Hii ni dalili mbaya sana ya utawala wake na ni dhahiri anayoyafanya yana ashiria kuwa ni maigizo tuu na hana nia ya dhati ya uwajibikaji kwa mawaziri ambao tayari kaonyesha kutokuwa na imani nao kuweza kuwakabili wabunge.
Namsifu sana Mhe Zitto Kabwe kwa kuonyesha ujasiri wa kulipigania hilo ingawa amekumbana na vikwazo toka kwa Mwenyekiti wa Bunge Chenge. Chenge pamoja na kutajwa kuwa ni mweledi katika mambo ya sheria lakini leo kaonyesha ni mtupu kabisa na kawekwa pale kwa malengo maalum.
Sisi wananchi kama wamiliki wa TBC1 tupinge kwa nguvu chombo hicho kuzuiwa kutuonyesha Bunge live.
Sasa gharama hizi zinawahusu mpaka Star Tv?
Mbona kwenye banks wahudumu hawazitazami hizo tv wakati wa kipindi cha bunge? Tv zimewekewa wateja sio watoa huduma maofisini na sehemu nyenginezo.
Serikali imechukuwa uamuzi sahihi kabisa, ilikuwa inafikia wakati unakwenda ofisini kupata huduma wafanyakazi wamekodoa kwenye luninga wanaangalia Bunge, Nasema SAFI SANA NAPE!
Safi sana hiki kilikuwa ni kilio changu siku zote, Watu wafanye kazi na waache kuangalia Bunge, mkirudi nyumbani jioni baada yakazi mtaangalia Bunge tani yenu au kama mmechoka hata wkend!
Safi sana W. Nape!
Mkuu kweli watu wengi waliochagua upinzani tayari walishaanza kuikubali kazi anayoifanya jpm sasa kwa kuanzia kuminya uhuru wa habariNdio maana nilikuwa najilazimisha kuikubali hii serekali ya Magufuli ila moyo ukawa unakataa kabisa hii serekali inaweza kuwa ya kidikiteta kwanza bomoa bomoa pili wamezima tbc watu wasione udhaifu wao.. Hata mawaziri alio chagua ni wale wa hovyo tusiowatalajia.. Wallah nawaambia Kikwete alikuwa rais na tutamkumbuka.. Kikwete ambae tulipo lalamika kuhusu mawaziri wake kuwa wabovu aliwapiga chini nakuweka wengine kwa Magufuli hiyo hamna.. Leo tbc juzi mawio kesho sijui nn
Barbosa najua unaweza kufikiri zaidi ya hapo, too sad kuwa umeamua kuchagua upande wa kitu/MTU na wala Si upande hoja/misingi.
Serekali ya Magufuli inaweza kuwa mbovu kuliko yoyote uliyowahi kuiona.. Kikwete baba tutakukumbuka kwa uhuru wa habali..
Mkuu...
Pamoja na kwamba siipendi na siangaliagi TBC, Lakini sikutegemea kama haya ni maandiko yako aiseeee....😕
Kama Bilioni nne tutalipa Ndugu Nape,Mbona tumepigwa Bilioni 129 na NIDA huku Vitambulisha hatujapata?
Katika kauli za Mawaziri, Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, ametangaza kwamba, Kuanzia tarehe 26 Januari mwaka 2016, TBC1 haitaonesha tena Mikutano ya bunge live kutokana na gharama za kuonesha live kufikia bilioni nne kwa mwaka.
Badala yake TBC1 watarekodi na kuonesha katika kipindi maalum usiku kuanzia saa nne hadi saa tano.
Hii itanyima wanchi fursa ya kuona kinachoendelea Bungeni.
Anyway, sio kosa lenu. Mmezoea kusifia Kila kitu hata kama ni utumbo. Kwa ushauri tu. Wasirushe hata kipindi cha maswali na majibu maana wanawafanya watu wasifanye kazi waangalie bunge
Hilo nalo ni wazo lkn haliko chini ya uwezo Serikali, hili la Bunge ni rahisi kwa maana Bunge ni chombo cha Serikali na ndiyo kinaamua nani arushe matangazo yake!
Katika kauli za Mawaziri, Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, ametangaza kwamba, Kuanzia tarehe 26 Januari mwaka 2016, TBC1 haitaonesha tena Mikutano ya bunge live kutokana na gharama za kuonesha live kufikia bilioni nne kwa mwaka.
Badala yake TBC1 watarekodi na kuonesha katika kipindi maalum usiku kuanzia saa nne hadi saa tano.
Hii itanyima wanchi fursa ya kuona kinachoendelea Bungeni.
Mbona kwenye banks wahudumu hawazitazami hizo tv wakati wa kipindi cha bunge? Tv zimewekewa wateja sio watoa huduma maofisini na sehemu nyenginezo.