Hizi kelele zote za sijui Bunge kutokuonyeshwa kwenye TV moja kwa moja ni sababu ya Watz kutokuwa na hobby na hivyo basi huishi kwa matukio, yaani hukaa na kusubiria kuangalia Bunge walipate cha kufanya, laiti kama Watz wangekuwa na hobby tusingeona humu watu wakilalama kama watoto, kisa TV imezimwa!
Dunia nzima ni Tanzania tu ambapo utasikia watu wakilalalmika eti Bunge halionyeshwi live, hata ukienda hapo Kenya tu hakuna mtu ana muda huo wa kungalia Bunge live hivyo waonyeshe au wasionyeshe hakuna atakayelalamika kwa maana watu wengi wana mambo muhimu ya kufanya ila hapa Bongo kwa kuwa watu wako idle yaani wapo wapo tu na hawajui wafanye nini hivyo wanasubiri matukio ndiyo sasa wapata cha kufanya na siku iende!
Hivyo nawashauri tafuteni hobby jifunzeni labda kuogelea, ua hata kung fu na karate zitawasaidia au hata fanyeni jogging tu beach mtaona tofauti kubwa sana na wala hamtkaa kusubiri Bunge ndiyo mpate cha kufanya!
Sijawahi kuiona sehemu yoyote ile Duniani watu wanalalamkia Bunge kutokuonyeshwa live kwenye TV!