TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Kumbuka TBC tu ndio anaweza kurusha live, hao wengine walikua wanachukulia TBC
Sio kweli, Azam wapo kivyao na star tv wapo kivyao, labda uniambie huwa wanakaa "chumba" kimoja cha kurushia matangazo na tbc pekee ndo wana ufunguo wa chumba, hapo labda naweza jaribu elewa!
 
Tunahitaji sana kujua kinachoendelea bungeni..Tunahitaji sana ili kujua namna wawakilishi wetu wanavyotuwakilisha ili tujipange kimaamuzi

Sababu za kubana matumizi na sijui kufanya kazi kwa bidii hazina mashiko
 
walisema huyu sio jembe bali ni "tingatinga"
 
inawezekana Nape akawa ndio waziri mbovu kabisa wa habari kuwahi kuwepo katika nchi hii .
 
Wasio kuwa na lakufanya kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana ajira yao kuangalia runinga tu kwa kisingizio eti bunge imekula kwao
Na kutafuta umaarufu kipitia kuuza sura bungeni nao imekula kwao tutashuhudia wabunge hata kuchangia hoja wataacha kisa hawaonekani kwenye luninga
Watu wafanye kazi
Unatetea ujinga.
 
Duh kwa mara ya kwanza nimemkumbuka mzee wangu "kuchomeka na kuchomoa" pamoja na yote hakika nitakukumbuka kwa uhuru wa vyombo vya habari.
 
Haaaa haaa Dr Magufuli akienda Muhimbili anaambatana na wanahabari anatumua Mkurugenzi,akienda wizara ya fedha hivyo hivyo ikifika wakati serekali yake inahojiwa hataki wananchi wasikie madudu ya serekali yake.
 
Sisi wananchi ndio tunalipa kodi kuiendesha TBC. Tunataka tuone live kazi za wawakilishi wetu bungeni. Serikali isiwe na uoga kupitiliza hadi kutunyima haki hii muhimu na wala Tanzania ya Magufuli si masikini kiasi hicho.
 
Duh kwa mara ya kwanza nimemkumbuka mzee wangu "kuchomeka na kuchomoa" pamoja na yote hakika nitakukumbuka kwa uhuru wa vyombo vya habari.
Ndio pale tunataka kila kitu kiwepo kwenye KATIBA ya NCHI sio kutegemea Huruma ya MTU ni wajinga tu wanaoamini ktk MTU kuendesha NCH
 
katika vitu ambayo serikali hii imefanya vya ajabu ni pamoja na hili, kodi zetu ila hata hatushirilishi kwenye maamunzi,nafikiri inabidi wafikiri upya!
 
Just wait, some few days to come nchi hii itakuwa na utawala kama wa Idd Amin Dada
 
ngoja niangalie mambo yangu yanyoke tu maana nikianza kufuatilia huko naona bora kuhama nchi
 
Magazeti sasa yatafanya biashara,kwani kila mtu alikuwa anaripoti na hivyo magazeti kuwa yanakosa radha na hivyo kutonunulika sana,
sasa wamiliki wa magazeti ndo mda wa kutuma maripota wao dodoma ili kufuatilia bunge na kuripoti
 
Hizi kelele zote za sijui Bunge kutokuonyeshwa kwenye TV moja kwa moja ni sababu ya Watz kutokuwa na hobby na hivyo basi huishi kwa matukio, yaani hukaa na kusubiria kuangalia Bunge walipate cha kufanya, laiti kama Watz wangekuwa na hobby tusingeona humu watu wakilalama kama watoto, kisa TV imezimwa!

Dunia nzima ni Tanzania tu ambapo utasikia watu wakilalalmika eti Bunge halionyeshwi live, hata ukienda hapo Kenya tu hakuna mtu ana muda huo wa kungalia Bunge live hivyo waonyeshe au wasionyeshe hakuna atakayelalamika kwa maana watu wengi wana mambo muhimu ya kufanya ila hapa Bongo kwa kuwa watu wako idle yaani wapo wapo tu na hawajui wafanye nini hivyo wanasubiri matukio ndiyo sasa wapata cha kufanya na siku iende!

Hivyo nawashauri tafuteni hobby jifunzeni labda kuogelea, ua hata kung fu na karate zitawasaidia au hata fanyeni jogging tu beach mtaona tofauti kubwa sana na wala hamtkaa kusubiri Bunge ndiyo mpate cha kufanya!

Sijawahi kuiona sehemu yoyote ile Duniani watu wanalalamkia Bunge kutokuonyeshwa live kwenye TV!
 
Hata mteja ataangalia Bunge jioni akirudi nyumbani, kuna wateja wengi huwa wanapitiliza wanaitwa namba zao hawazisikii kwa sababu wamekodolea luninga, Bunge na hii yote hupunguza uzalishaji kwani unasogeza muda mbele ambapo wateja wengine wangeshahudumiwa tayari!
Nchi hii ni ya wote sio ya watawala wasio na maono kama serikali ya awamu ya tano watakwama vibaya sana
 
Back
Top Bottom