TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Aaah Nape!!!!! kumbe bado uko mbali hivyo kimtazamamo kuusu watanzania wa sasa unafikiri kweli watakubali kirahisi maelezo yako kuwa "baadhi" yao wamepongeza kipindi cha leo kutoka bungeni kwa kuwa serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake kwa madai ya gharama kubwa ya matangazo ya moja kwa moja! aibu.

Nape, Watanzania hawa ni wa kuwaambia kuwa unasitisha matangazo kwa sababu eti ni "gharama" kuyaendesha hivyo sasa utawekwa utaratibu wa kuonyesha baadhi ya matangazo ya moja kw amoja lakini mengine yatarushwa saa nne usiku! huku ni kudhalilisha akili za watanzania kwamba hawawezi kufikiri kilicho nyuma ya upuuzi unaoendelea.

Baadhi yetu tuliona jinsi kampeni zilivyoendeshwa kwa ubaguzi wa vyombo vya habari huku waandishi wakinyanyaswa na wengine kufikia kufukuzwa kwa kuandika habari wasizopenda wakubwa, tukabaini kwamba mfalme mpya hawezi kutaka mambo yame yaanikwe. takribana siku 75 baada ya kuingia mfalme na utawala wake wamefanya mambo ya kukandamiza uhuru wa habari kwa kiwango cha kujiuliza huko tuendako itakuwaje?. mawio liko wapi?

Gharama!, Nape bajeti ya mwaka ya TBC ni kiasi gani ambayo inaathiriwa na kurusha matangazo ya moja kwa moja ya bunge kulinganisha na vipindi vingine vinavyorushwa hapo TBC? Je gharama hizo ni kubwa katika kuonyesha matangazo ya bunge tu au pia katika matangazo ya moja kwa moja ya shughuli kama siku ya ukimwi, mapinduzi nk? hivi yatakayoathirika ni matangzo ya bunge au matangazo yote?

Nape, kwanini kujidhalilisha na kujiumbua mbele ya kadamsnasi jinsi mlibyokuwa na fikra ndogo kwa kutoa mtamshi ya aina hii. si ndio nyinyi hapa majuzi mmerusha Live matangazo ya harusi moja! inaingia akilini kweli kuonyesha matangazo ya harusi ya mtu binafsi na kuacha matangazo ya Bunge?

Aaah Nape, hebu twende taratibu, utupatie mchanganuo wa gharama mnazoingia kiwa kurusha hayo matangazo ili tuweze kubaini ukweli wake. lakini pia kwa kiongozi wa awamu hiii ambayo imebatizwa jina la #whatwouldmagufulido# hauoni ilikuwa ni changamoto ya kukuongezea sifa ya utendaji bora kama ungefanikiwa kufanya ubunifu wa kuzitafuta fedha hizo kutoka katika vyanzo mbalimbali ili kuwafikishia wananchi matangazo hayo?
Nape, Wakati seriikali yako inafanya jitihada za kufikisha umeme vijijini wewe na TBC yako mnafanya jitihada za kuwanyima matangazo muhimu ili huo muda muonyeshe tamthilia za Kikorea au Mexico au kile kipindi maarufu cha kijiweni. Nape kuwa serious kidogo. Na hatab kama ni kweli kwamba gharama ni Bil nne kwa mwaka, Mheshimiwa sana waziri wa sanaa kwani kuna tatizo gani kwa watanzania kutumia hela zao kiasi cha shilingi bilioni nne kati ya makusanyo ya Trillioni 1.4 kwa mwezi?
Nape, Watanzania wa leo?!
 
Kwa nilivyoona leo wanavyozomea bora tu wasitishe labda itasaidia wabunge kuwa makini maana wengine alitumia nafasi hiyo kuwa maarufu kwa kutukana kuzomea na kufanya vituko wakijua kesho wataandikwa magazeti na kuongelewa kila kona
Safi sana Magufuli
hapa kazi tu
Mimi nakubalia kabisa na kusitisha kuonesha Live bunge itasaidia watu kujenga hoja na kwa hakika wale wanao penda kujipatia umaarufu kwisha habari yao....
 
Poleni sana wakuu naona nape kawatouch sana,lakini nahakika sio uamzi wake pekee.

Zama za kuuza sura kwenye luninga zimepita,NI KAZI TU
Cha kushangaza wanao lia ni wale wano iponda kila siku TBC na wanasema huwa hwwaiangalii....
Hili ni pigo kwa UKAWA maana walitegemea kujitafutia umaarufu kupitia TV
 
Hii serikali ya Magufuli lenyewe Ni jipu. Hawataki likosolewe. Tv za majirani zetu wanashindana kuonyesha live matukio yote muhimu kwa maslahi ya watu wao,sisi ahh. Jamaa wanaonyesha hadi kesi za mahakani. Awamu hii wako too manual.
Hapa tutamkumbuka Kikwete,alikuwa mvumilivu Sana kwa wakosoaji wake,sio hawa wa sasa.
Sishangai Sana,maana waziri wa habari na michezo hajui hata TFF ni nini,inasimamia nini na wapi. Majipu kila kona
Ni kweli aise, walimvumilia sana Dr. Ulimboka. Kama haitoshi wakamvumilia Mwangosi wa habari. Wakazidi kumvumilia mpare wa katiba!
Msijidanganye, watawala wote mama yao ni mmoja, matumbo tu yanakuwa mbali mbali
 
Heshima kwenu wote,
Nasema hii agenda ya kubana matumizi kwenye mambo muhimu haikubaliki.TBC ni shirika la UMMA linaloendeshwa kwa kodi zetu watanzania wote,inakuwaje mtu mmoja aje na agenda ya kuzuia BUNGE lisionekane LIVE,eti kisa kubana matumizi,nasema PESA ya Bunge kuonekana LIVE ilishapitishwa/kutengwa na bunge mwaka wa fedha 2015/2016,nataka kujua hiyo pesa inayosema inafikia bilioni 4,(Tshs) imepelekwa wapi au kuna wajanja wamekula ndio maana mnataka kutunyima wananchi HAKI yetu ya KIKATIBA kupata HABARI.???

Hii ndi double standards na haikubaliki,hatuwezi kutegemea vituo binafsi vituoneshe mikutano ya bunge huku TBC ikionesha mambo mengine,ikumbukwe macho na masikio ya watanzania makini yako Dom,kufuatilia bunge.Nina hofu na hivyo vituo binafsi vinaovyoonesha BUNGE,ikitokea wakafungiwa kama MAWIO,ina maana tukose haki yetu moja kwa moja kisa kubana matumizi?? Nasema TBC ni mali ya UMMA sio mali ya waziri binafsi!!!!
 
Sasa walalamikie nini kama hakuna cha kulalamikia?
Hotuba yenyewe imegusia kila kitu sijui Rais alitaka wengine wakose cha kusema..
 
Nape unayofanya siyo sawa. hata aliyewahi kupata F tatu Enzi akisoma hawezi kufanya vile. Ghrama unazipunguzaje wakati unaoungeza kazi ya kuedit, kuapprove kurusha????? kumbuka watakao record na kuemdsha mitambo Bungeni ni wala wale. Mnachofanya ni switching on and off os atransmitter to satelile for broadcasting. tunajua kuwa satellite ni yetu means owned by GVT!!!!! Then what is issue behind, pla Nape come with black and white reasons and not political wish wash!!!!!!!!!!!
 
Waziri asiyefahamu kirefu cha TFF lazima alazimishe TV zizimwe!

Hehehehehe!!
 
What's the point of your right to speak if there is no one to listen to what you are speaking? Doesn't the very concept of censorship clash with the idea of democracy? If we are going to cover the ears of our listeners, then what is the difference between democracy and dictatorship?!?


If the content in the media is manipulated by some people with vested interests, then the whole point of democracy and freedom of thought goes out of the window anyway. And, how difficult do you think it is to get an uncensored version of anything these days? By censoring it, you are promoting it even more!! We are heading into the Ditch!
 
Shirika limekuwa likigharamia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo madogo ya biashara, ifahamike kuwa asilimia 75 ni vipindi vingi vinavyolenga kutoa elimu kwa umma na asilimia 25 ni burudani.
Hivi kikijitokeza kituo kama Citizen cha Kenya au kingine chochote wakasema wanarusha bila kutoza gharama kwa yeyote itakuwaje!? ...au ndipo tutajua unafiki wa wanasiasa wa TZ!
 
Nchi haiendeshwi kama gheto wewe pongo..

Shirika la utangazaji la umma (TBC) linaendeshwa kwa kodi za wananchi, hivyo tuna haki ya kujua na kufuatilia kile kinachoendelea hususan Bunge ,..
 
Ukiwa na hulka ya kuongoza kwa vyombo vya habari, usiishie kutaka kufuatilia ya wanaokuwa na mrengo wako hasa wanaokusifia ukaacha ama ku-ban media zisizo mrengo wako.

Itafikia mahala mawaziri wakapata shida kufanya kazi kisa mirengo ya kichama wakasahau majukumu kwa taifa.

Hili la kutokuonesha bunge linatufanya turudi kwenye karne/zama za kizamani. Hii si dunia ya umbumbumbu.

Ni haki ya watanzania kupata habari, zilizo na uhakika na si kuishia kusimuliwa kama hawachangii kodi zao kuendeshea TBC.

Itafikia kipindi kupiga kura ya kutokuwa na imani na waziri wa habari. Na hili laja!
 
Hivi BBC inaoneshaga bunge live?
BBC unayoiona wewe ni BBC International, ukiwa Uk wana BBC kama tatu hivi pamoja na Bbc za redio kama 6 hivi, kuna bbc moja bunge ni laivu, yaani house of commons sijui house of lords ni laivu!
 
Umejuaje kama nchi nyingine hawalalamiki kama sio kuendeleza tabia ileile ya uzushi na kusema vitu visivyokuwa na uhakika?
 
Back
Top Bottom