TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

sasa kama wanataka kubana matumizi, si wauze maVX wanayotumia watumie mabasi kwenda Dodoma. kwa ruti za mjini hapa watumie bodaboda au bajaji ............ CCM wenyewe ni majipu.

bora mkwere" tunakukumbuka.
 
Katika kauli za Mawaziri, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Nape Nnauye, ametangaza kwamba, Kuanzia tarehe 26 Januari mwaka 2016, TBC1 haitaonesha tena Mikutano ya bunge live kutokana na gharama za kuonesha live kufikia bilioni nne kwa mwaka.

Badala yake TBC1 watarekodi na kuonesha katika kipindi maalum usiku kuanzia saa nne hadi saa tano.

Hii itanyima wanchi fursa ya kuona kinachoendelea Bungeni.
=========



Mheshimiwa spika,
Naomba kutoa kauli ya serikali kuhusu TBC kutangaza moja kwa moja vikao vya majadiliano ya bunge. Mheshimiwa spika, shirika la utangazaji Tanzania, TBC lilianza kurusha moja kwa moja matangazo ya vikao vya bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania mwaka 2005. Kabla ya kuanza kurusha moja kwa moja, TBC wakati huo televisheni ya taifa ilikuwa inarekodi matukio yote ya bunge na kurusha usiku katika vipindi maalumu vilivyojulikana kama bungeni leo kwa maana ya yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika.

Baada ya kuanza kwa utaratibu wa kuanza kurusha matangazo moja kwa moja mwaka 2005, gharama za kufanya kazi hio zimekua zikipanda kwa kasi hadi kufikia Tshs. bilioni 4.2 kwa mwaka kwa maana ya mikutano minne ya bunge.

Shirika limekuwa likigharamia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo madogo ya biashara, ifahamike kuwa asilimia 75 ni vipindi vingi vinavyolenga kutoa elimu kwa umma na asilimia 25 ni burudani.

Mheshimiwa spika, kutokana na hali hii, TBC imeona ni busara kubadilisha mfumo wa utangazaji wa shughuli za bunge ili kukabiliana na kupanda kwa gharama za uendeshaji, hivyo basi, TBC imeona ni busara kuanzia mkutano huu wa bunge iwe inarusha baadhi ya matangazo ya bunge moja kwa moja yaani live ikiwa ni njia ya kubana matumizi.

Chini ya utaratibu huu, TBC itahakikisha kuwa, baadhi ya matukio ya matukio ya bunge yatarushwa moja kwa moja na mengine kurekodiwa na kuandaliwa kipindi maalum kitakachoitwa leo katika bunge. Kipindi hiki kitakua na mambo yote muhimu yaliyojiri ndani ya bunge kwa siku husika. Kipindi hichi kitakuwa kinarushwa kuanzia saa nne usiku hadi saa tano usiku.

Na mheshimiwa spika kipindi hicho kimeanza jana na tayari baadhi ya wananchi wameonyesha kuridhishwa na utaratibu huu na kuwa na kipindi maalum usiku kikishughulikia shughuli za bunge, mheshimiwa spika, uamuzi huu utapunguza gharama za uendeshaji wa shirika na pia kupitia kipindi cha leo katika bunge, watanzania walio wengi watapata nafasi ya kufahamu yaliyojiri bungeni kwani wakati bunge linaendelea mijadala yake, watanzania walio wengi huwa wanakua na kazi za kiofisi au zingine za ujenzi wa taifa kwa mahali walipo.

Mheshimiwa spika nakushukuru.

Uh mi naona kuna vipindi vingi visivyokuwa hata na wateja TBC lakini vinaendelea kurushwa tu kana kwamba hawana namna ya kuona nani kaangalia vipindi vyao. Kwa kutorusha matangazo ya bunge moja kwa moja kwanza kunaifanya TBC iwe si chombo cha wananchi, pili itaipunguzia hata umaarufu kidogo iliokuwa inaupata kwa kurusha vipindi ambavyo havijafanyiwa editing kwa kuwa waki edit tu utaona TBC watu wanaiita TV-CCM. Hii si oni la kupuuza kama tunataka kujenga jamii bora inayojali wananchi wake. Wenye takwimu watuwekee hapa uone waliokuwa wanaangalia TBC ya Tido Mhando na kilichojiri baada ya Tido. Lakini alichofanya Tido ni sawa na ilivyo BBC hadi Tony Blair mbele ya tume maalum juu ya ushiriki wake katika vita vya Iraq kama ulikuwa na maslahi kwa Uingereza vyote vilikuwa live hadi Iraq kwenyewe....Dr Magufuli tumbua jipu hili la ndugu zako wanaoogopa vivuli visivyo kuwepo maana agenda ya wapinzani umeshaimeza, unalo jukumu la kujenga demokrasia ya kweli. Sisi wanyonge tuko pamoja nawe. Huko kuwapa uenyekiti wapinzani wako ndani ya chama chako utaja jutia. Ni ushauri tu kama unapokeleka
 
Wana wa nchi hii wakiwa bado na majonzi na uchungu uliotokana na ghiliba za kikundi cha watu wachache, waroho wa madaraka waharibifu na wakatiliwa hali ya juu, waliodiriki kuitumia katiba vibaya kupora haki ya walichochagua.

Sasa Taifa linazidi kupondwa na kuumizwa na kundi lilelile kwa mbinu ya kupofusha watu macho na kuwatoboa masikio wasisikie wala kuona uchafu na uozo wa ufalme uliopita.

Kitendo cha kuzuia Matangazo ya Bunge yasitazamwe moja kwa moja ni kuua uhuru wa kupata taarifa.
 
Mfalme akitoka nje hajavaa nguo,hataki aambiwe yupo uchi.
Anataka aambiwe nguo zake zinampendeza sana
Hii Ni hulka ya tawala zote za kidikteta na kifashisti kupenda kusifiwa hâta wasipostahili
 
KAULI YA SERIKALI KUHUSU TBC KUTANGAZA MOJA KWA MOJA
MAJADILIANO YA VIKAO VYA BUNGE

Shirika la Utangazaji Tanzania TBC lilianza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya vikao vya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania mwaka 2005.

Kabla ya kuanza kurusha moja kwa moja TBC wakati huo Televisheni ya Taifa, ilikuwa inarekodi matukio yote ya Bunge na kurusha usiku katika vipindi maalum vilivyojulikana kama Bungeni Leo kwa maana ya yaliyojiri ndani ya ukumbi wa Bunge kwa siku husika.

Baada ya kuanza kwa utaratibu wa kurusha matangazo moja kwa moja mwaka 2005 gharama za kufanya kazi hiyo zimekuwa zikipanda kwa kasi hadi kufikia Shilingi Bilioni 4.2 kwa mwaka (mikutano minne ya Bunge).

Shirika limekuwa likigharimia kwa sehemu kubwa matangazo hayo kwa kutumia mapato yake yanayotokana na matangazo madogo ya biashara. Ifahamike kuwa Asilimia Sabini na Tano ni vipindi vingi vinavyolenga kutoa elimu kwa umma na asilimia ishirini na tano ni burudani.

Kutokana na hali hii TBC imeona kuwa ni busara kubadilisha mfumo wa utangazaji wa shughuli za Bunge ili kukabiliana na kuzidi kupanda kwa gharama za uendeshaji.
Hivyo basi TBC imeona ni busara kuanzia Mkutano huu wa Bunge iwe inarusha baadhi ya Matangazo ya Bunge moja kwa moja (Live) ikiwa ni njia ya kubana matumizi.

Chini ya utaratibu huu TBC itahakikisha kuwa baadhi ya matukio ya Bunge yatarushwa moja kwa moja na mengine kurekodiwa na kuandaliwa kipindi maalumu kitakachoitwa LEO KATIKA BUNGE. Kipindi hicho kitakuwa na mambo yote muhimu yaliyojiri ndani ya Bunge kwa siku husika.

Kipindi hicho kitakuwa kinarushwa kuanzia saa nne usiku hadi saa tano usiku. Kipindi hicho kimeanza tarehe 26 Januari, 2016 yaani jana na tayari baadhi ya wananchi wameonesha kuridhishwa na utaratibu huu wa kuwa na kipindi maalumu usiku kuhusiana shughuli za Bunge.

Uamuzi huu utapunguza gharama za uendeshaji kwa shirika na pia kwa kupitia kipindi cha LEO KATIKA BUNGE Watanzania walio wengi watapata nafasi ya kufahamu yale yaliyojiri Bungeni kwani wakati Bunge linaendelea na mijadala yake Watanzania walio wengi huwa wanakuwa na kazi za kiofisi au zingine za ujenzi wa Taifa kwa mahali walipo.
Someni kwa makini hii kauli then jengeni hoja.
 
kumbuka TBC wanapata ruzuku na inaendeshwa na kodi ya Watanzania.swali hizo galama zinatumika na zinaenda wapi? hapo kuna jipu na Nape usiwarudishe watanzania kwenye zama za kale.

swissme
 
Mimi napongeza serikali kwa fikiria hili suala, hili ni fundisho kwa kila mtu kutumia kutokana na uwezo.Safi sana wizara, mimi nawaunga mkono.
 
kumbuka TBC wanapata ruzuku na inaendeshwa na kodi ya Watanzania.swali hizo galama zinatumika na zinaenda wapi? hapo kuna jipu na Nape usiwarudishe watanzania kwenye zama za kale.

swissme

= gharama
 
Hongera serikali kwa kutekeleza kwa dhati sera ya Ukawa kuhusu kubana matumizi ya fedha za umma. Ukawa mmejitia kitanzi wenyewe sasa mnalialia nini? #Hapakazitu.
 
ni haki ya kila mtz kupata habari hasa kuhusu bunge. basi viacheni vyombo binafsi vishughulike haya ya bunge,maana sasa wanaongalia hichi kipindi watakuwa wengi hence itaongeza gharama za kutangaza biashara wakati wa kipindi cha bunge.

serikali ina complain kila kitu,hata hzio ndege mnazonunua zitawashinda.
nilishasema serikali kufanya biashara ni biashara kichaa.

magufuli anataka biashara huku bado ni ant business
 
Hiyo ya usiku inatosha kabisa, wanaotaka live wakalipie wenyewe gharama hizo
 
hakuna nchi hapa duniani bunge linaoneshwa live kipindi chote.
hatutaka kuona sura zenu hapa tunataka maendeleo kwenye majimbo
 
kitendo cha tbc kutooneshwa live kimenifurahisha sana.
lilikuwa ni jambo lililokuwa linanikera sana kutoa maneno ya hovyo na wajinga watazamaji wanalishangilia pasipokujua mbunge wao anawasaidia nini kwenye jimbo lao
 
Sio ujinga , hili suala ni la maana kweli kuweza kutokea kwa Watanzania. Sisi watanzania tunahitaji wanasiasa wakweli, wenye kujua majukumu yao. Sasa watapata muda wa kufanya kazi sio kuleta utoto, kuropoka ovyo, kukosa heshima na fujo nyingine. Walifikira watanzania wote tunapenda maigizo,wamezoea siasa za kuonekana, sasa wafanye kazi kubadili maisha ya mtanzania.
 
kitendo cha tbc kutooneshwa live kimenifurahisha sana.
lilikuwa ni jambo lililokuwa linanikera sana kutoa maneno ya hovyo na wajinga watazamaji wanalishangilia pasipokujua mbunge wao anawasaidia nini kwenye jimbo lao
You wont understand until you understood
 
kitendo cha tbc kutooneshwa live kimenifurahisha sana.
lilikuwa ni jambo lililokuwa linanikera sana kutoa maneno ya hovyo na wajinga watazamaji wanalishangilia pasipokujua mbunge wao anawasaidia nini kwenye jimbo lao
Kwa hiyo lisipoonyeshwa Ndio atawasaidia jimboni?sometimes kukaa Kimya kunalinda identity Sana
 
Back
Top Bottom