TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Hoja mfu eti ni wakati wa kazi ... Sisi analyst tunaotegemea TV kuchambua tuende Bar asubuhi ?
 
waliosema vyama vya upinzani vitakufa baada ya magufuli kuchaguliwa walibugi, yaani uwanja sasa umepanuka sana. sijui hata kama hawa jamaa wataweza kutuletea katiba mpya.
 
Wakati tunafikiri kwenda digital na 4G.
News before News.
Nape aboleshe live streaming video, live information zi flow kama maji ya Bomba kila kona mpaka TBC TV zikose kazi.
 
maswali ya kujiulza:
kama gharama 4.2bilions kwa mwaka...je wanaporusha baadh y vpnd wanaokoa kias gn. uckute 2bilions tu wanazookoa! sasa hapo hawatakuw wameokoa pesa ispokuw wanatukandamiza cc wannchi.hoja ya TBC na nape wao nyepec hazna mashko. ni bora wauze yale mashanging yao kipnd ch TBC kiwe online!!!
 
Inaskitisha na kushangaza sana, na tayari watu makini tumeshampa Nape Nauye 40% ya imani ktk utendaji kazi wake... Haiwezekani kuanza tu kwa Bunge tayari Nape anatoa mawazo kama yale ktk siku za mwanzo hili ni tishio na kauli zake ni threat complete.
Maana kwa kauli hiyo ya TBC1 kutaka kurusha matangazo ya umma yakiwa recorded huko ni kudhulumu haki wananchi, kwani wanapoingia bungeni inatakiwa tuingie wote na ndiyo kazi ya hiki chombo kuhakikisha kinatupeleka mpk mle ndani..
Kinyume na hapo basi naiona kauli ya Membe ikiwa hai, alisema watanzania watamkumbuka sana Jk ktk Uhuru wa hbr...
Daaah! Yaani huyo katibu mkuu wa wizara ya hbr ndivyo anavyomshauri hivi Nape kweli!!
Leo Serikali inashindwa kulipa gharama za matangazo tena ya Tv yetu kisa bana matumizi lkn kwenye mambo ya capacity charge wanalipa mamilion ya shilling kwa siku... Hili la Nape sitaki kuliamin kbs.
 
Vyombo binafsi kama ITV, star times, Azam na redio mbalimbali ziruhusiwe ,ziweze kuonyesha, cut cost ipo kwenye vyombo vya serikali basi vyombo binafsi ni wakati basi wao waendelee kutoa huduma hiyo kwa wananchi. Kama watu mil 5 au zaidi wanaangalia hicho kipindi kwa nini msiwapatie haki yao? hata kama ni jobless, lakini wanahaki ya kujua kinachojili na hatima ya nchi yao. Pili, serikali ina mpango mzuri wa kupunguza gharama lakini tumewahi jiuliza ni kwanini vitu vya serikali kama TBC,viwanda, ATCL, reli..... vimekufa? wakurugenzi au serikali uwezo wao wa kuviendesha hivi vyombo kibiashara ni mdogo, huu ulikuwa ni wakati mzuri wa TBC kujitangaza kibiashara kwani zaidi ya watu M5 wanatazama, converts 5M people into revenue, hapo ilitakiwa wapate pesa za matangazo ya biashara, Kituo kitakuwa famous na kuattract wawekezaji zaidi na kuzidi kujitanua, ndo maana kila mwaka ,50 yrs TBC ni ileile palepale Dar, nilitegemea muda huu TBC ingekuwa imeshafika au kuwa na branches mikoa yote ya TZ, tumeishia kusema ohh gharama ni kubwa, ohhh hakuna ruzuku ohhh chombo cha serikali, tutaishia kuanzisha vitu vinakufa kwa sababu ya kuendesha vitu kisiasa zaidi kuliko kibiashara. Watu hawa hawana marketing plan, no website, no google promotion/per click, no yahoo promotion, no face book promotion, no online streaming, sasa serikali kwa utendaji huu mbona majibu kila mahali? tumekuwa na watu incompetence kila sector, anzia wabunge walewale, serikali yale yale, mawaziri wale wale, tujiulize, kama wabunge wetu ni competence kuna haja ya kuogopa bunge kutorushwa live kwa kisingiziio cha umaarufu wa chama fulani utashuka au utaongezeka?, toa hoja nitoe hoja, kama bunge kinajadili muafaka wa taifa bila upendeleo haki zinafuatwa wht is the problem? kama wananchi wanatazama au hawatazami wht is the problem, TBC ilitakiwa wafocus kwenye biashara tu, focus on looking subscribers, sasa mtapata subscribers kama hamtajulikana? mtapata wapi matangazo? ,tukiibana sana TBC maana yake itakufa. Ilitakiwa serikali kama ina 5OM usd ya TV invstments wawaambia hao TBC, my friend atter 5 yrs nikute TBC kama hii 7 mwanza, zanzibar, arusha, mbeya, tanga, dodoma,.........., Hii ndo key performance indicator yenu (KPI).
 
Wabunge wa upinzani wachange hela bunge irushe live na itv
 
Tuliwaambia sisiem ni ile ile mkabisha kwa nguvu zote... ELIMU... ELIMU... ELIMU.. Tutakukumbuka sana Lowasa, Mungu akupe Maisha marefu.. Tunauchungu mwingi mno mioyoni mwetu ni vile tu hatuwezi kuwasha Moto.
 
......katika comment zooote za mwaka huuu hii nimecheka mno
Ndio ivyo my friend,,,kwa mujibu wa maandiko matukufu na kauli ya M/ mungu isiyo na Shaka, anasema ya kwamba;; '' UMPA UFALME AMTAKAE,,NA UMUONDOLEA UFALME AMTAKAE KATIKA WAJA WAKE,, kwaiyo kama mungu hajataka wewe uwe kiongozi katika nchi,,utamaliza makafara,,,,ila kila alichofanyalo mungu huwa na maana kubwa mwenyewe,,kwaiyo ngojea tuone mwisho wa Ccm,,ila nahisi mwisho wa ccm utakuwa mbaya mno huko katika vizazi vyetu vijavyo vya wasomi,,baada ya sisi wazee wao wajinga kuondoka ktk mgongo huu wa ardhi,,,
 
Nape anatakiwa apigiwe kura ya kutokuwa na imani naye.hafai kuwa Waziri Wa habari
 
TBC ya wazee imekaa kimagumashi zaidi....Matoz hatuna tym mayo km vp wazime mitambo yao kabisa inakera CHAN tu wameonesha vigame vichache utafikiri mgao wa mirathi
 
Ni bora kufanya utafiti kidogo maana siku hizi ruzuku ni kama hazipo kabisa. Kwa sasa mashirika mengi ya umma yanatakiwa kujiendesha bila kutegemea ruzuku toka serikalini. Kwa hali kama hiyo TBC itabidi ibane matumizi hakuna jinsi. Maoni yangu ni kuwa Wabunge wapunguziwe marupurupu ili fedha hizo zigharamie suala hili
Wanaposema ruzuku maana ake ni kuwa TBC ni Ofisi ya Serikali hivyo basi ina bajeti yake kwa ajili ya kila kitu inachofanya na bajeti ilishapita mkuu
 
Hii Serikali ya CCM sijui ina matatizo sana kiukweli

Ni shida sana ,tutajuta hii bado
 
Wanaposema ruzuku maana ake ni kuwa TBC ni Ofisi ya Serikali hivyo basi ina bajeti yake kwa ajili ya kila kitu inachofanya na bajeti ilishapita mkuu
Hizo ni ndoto, baada ya ESCROW waliopata shubili ni afisi za serikali kama TBS ambazo ruzuku zake kama ilivyopangiwa katika Bajeti zilipungua hadi chini ya 30 percent. Nasema acha theories tafuta uhalisia. Muite Mshana kama yupo hapa JF anaweza kukueleza
 
Kama gharama ni kubwa hakuna haja ya kurusha mipasho hiyo, pesa hizo zielekezwe kwenye huduma nyingine za jamii mfano kununua madawati shuleni n.k
Na hizo fedha zinazotengwa kwa ajili ya madawati shuleni nazo zipelekwe wapi?
 
Hizi sasa ni sifa tena bila maarifa kwani kuendesha bunge huwa wanatumia mavi ?
Ila hapo serkali ya john pombe imeonesha upunguani hali ya sana.
 
Naunga mkono 100%
We mtu siku hizi akiangalia Bunge basi unamskiki anasema aahh leo hasa hakuna raha,maana nilitaka fulani arushe madongo.
Hapa ndio tutajua kwamba mdomo ndio unaoleta maendeleo au kuuza sura.
Tumeishawaona woote inatosha sasa,kuna watu kwenye majimbo yao wamepata credit kwa kuongea tuuu,ila majimbo yao taaaabani.Sasa watu wanataka maendeleo.
Waonyeshe wasionyeshe poa tu,na hii itafanya wabunge mara kwa mara warudi majimboni kwao kutoa taarifa wa walioomba serikalini na kuweka wazi hatu na mikakati ya maendeleo ya jimo na mkoa kwa ujumla.

Maendeleo hayaletwei kwa kuangalia upuuzie wa matusi kila siku,acha watukanane kimya kimya huko,wakitoka sie wananchi tunawahoji nini wamefuatilia na nini wametekeleza.Tunataka maendeleo ya kuonekana na sio ya kupiga zogo.
We 4.2 Billions za wananchi kwa mwaka sio mchezo,na hili tulikuwa wananchi hatulijui kama kodi yetu kubwa hivyo inaenda kwa Bunge hilo kuomyeshwa Live,tungelianzisha mapemaaa,Bora nape umeliibua.
Pesa nyingi saaana hizo.Mahospitalini taabani huko,kisa upuuzi wa kuona Bunge.
 
serikali imeweka vipingamiz kwa TBC kuonesha bunge live,kwa sababu ya kiuchumi, nk wazijuazo wenyewe....nilitaka kujua vip vyombo binafs kama ITV,AZAM TV,...NK HV HAVITAONESHA?? AU NAVYO VILIKUWA VINAJIUNGA NA TBC??? KUPATA HABAR ZA BUNGE??..INAWEZEKANA KELELE ZA UPINZAN ZIKAGOTA THEN WHAT NEXT???? CCM NI ILE OO NI ILE ILE MWAKA HUU WATAISOMA
 
Ahahahahahaha duh clouds inaonyesha show live ya fiesta kwa zaid ya masaa 4 kwaiyo nao wanakalibia gharama izo duh gari ya wachina waliotupa zawadi la matangazo live cjajua gharama yake ila naona litaoza pale bbc na live zake itakua inatumia bajeti kubwa zaidi ya bajeti ya taifa tanzania ooh poor me
 
Back
Top Bottom