TEKNOLOJIA
JF-Expert Member
- Jan 6, 2014
- 4,305
- 2,563
Hivi karibu Mh Rais kupitia Waziri wako wa Habari Bw. Nape Nauye mliutangazia umma kwamba kuanzia sasa TBC haitaonyesha vipindi vyote vya bunge live,kwamba eti mtakuwa mna_record baadhi ya sessions hasa ile ya jioni na kuionyesha usiku saa nne kwenye kipindi cha 'Leo Katika Bunge' ikiwa ni hatua ya kubana matumizi ya kituo hicho kinachoendeshwa kwa kodi za wananchi.Sawa hapa tumejaribu kuwaelewa japo kwa shingo upande ukitilia maanani kwamba Waziri wako wa Habari alikuwa Katibu mwenezi wa chama tawala na huyu mtu anajulikana kwa misimamo yake ya kuchukia upinzani.
Lakini sasa, mbona huku kwenye eneo linalohusu kugawiana madaraka hautaki kupagusa pia?Au kwa vile huku kunahusu ajira za jamaa zenu,rafiki zenu,ndugu zenu,makada wenzenu?Kusema ukweli tumeshtushwa sana na uamuzi wa serikali yako wa kuongeza wilaya nyingine mbili ndani ya jiji la Dar kwani uamuzi huu unapingana na dhana nzima ya kubana matumizi,kwa kuongeza wilaya hizi mbili maana yake pia na matumizi ya serikali yataongezeka.
Sasa tunajiuliza,mnaposema kwamba mnanuia kutorusha vipindi vyote vya bunge live na badala yake mta_record ili muonyeshe saa nne usiku kama hatua moja wapo ya kubana matumizi halafu hapo hapo mnakuja kuongeza idadi za wilaya,kwakweli tunashindwa kuwaelewa zaidi ya kuamini kwamba hii ni double standard tu mnayoionyesha kwavile huku kwenye suala la kurusha matangazo live linahusu utowaji wa taarifa za mijadala ya bunge kwa wananchi wakati huko inahusu ajira za watawala na maslahi yao ya kisiasa.
Yangu ni hayo Mh. Rais Magufuli.