TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

TBC1 yasitisha kuonesha baadhi ya Mikutano ya Bunge moja kwa moja (Bunge LIVE)

Hivi karibu Mh Rais kupitia Waziri wako wa Habari Bw. Nape Nauye mliutangazia umma kwamba kuanzia sasa TBC haitaonyesha vipindi vyote vya bunge live,kwamba eti mtakuwa mna_record baadhi ya sessions hasa ile ya jioni na kuionyesha usiku saa nne kwenye kipindi cha 'Leo Katika Bunge' ikiwa ni hatua ya kubana matumizi ya kituo hicho kinachoendeshwa kwa kodi za wananchi.Sawa hapa tumejaribu kuwaelewa japo kwa shingo upande ukitilia maanani kwamba Waziri wako wa Habari alikuwa Katibu mwenezi wa chama tawala na huyu mtu anajulikana kwa misimamo yake ya kuchukia upinzani.
Lakini sasa, mbona huku kwenye eneo linalohusu kugawiana madaraka hautaki kupagusa pia?Au kwa vile huku kunahusu ajira za jamaa zenu,rafiki zenu,ndugu zenu,makada wenzenu?Kusema ukweli tumeshtushwa sana na uamuzi wa serikali yako wa kuongeza wilaya nyingine mbili ndani ya jiji la Dar kwani uamuzi huu unapingana na dhana nzima ya kubana matumizi,kwa kuongeza wilaya hizi mbili maana yake pia na matumizi ya serikali yataongezeka.
Sasa tunajiuliza,mnaposema kwamba mnanuia kutorusha vipindi vyote vya bunge live na badala yake mta_record ili muonyeshe saa nne usiku kama hatua moja wapo ya kubana matumizi halafu hapo hapo mnakuja kuongeza idadi za wilaya,kwakweli tunashindwa kuwaelewa zaidi ya kuamini kwamba hii ni double standard tu mnayoionyesha kwavile huku kwenye suala la kurusha matangazo live linahusu utowaji wa taarifa za mijadala ya bunge kwa wananchi wakati huko inahusu ajira za watawala na maslahi yao ya kisiasa.
Yangu ni hayo Mh. Rais Magufuli.
 
Kuna wilaya ya Ubungo na kigamboni aliongeza JK. Je. JPM naye kaongeza zipi tena?
 
Hizo ni Wilaya majimbo ya Kura? Ninavyojua majimbo yaliyoongezwa ni Kibamba na Mbagala.
 
Uamuzi WA nape juu ya tbc1 ni pigo kwa ukawa,kwa sababu ukawa walishazoea kujipatia umarufu kupitia drama wanazozifanya wakati WA bunge,vyanzo vyangu vya habari vinasema drama zinazofanyika bungeni zilipangwa kwa ajili ya kutengeneza attetion kwa wanachama,uamuzi WA nape ni Tishio kwa ukawa ndo maama walikua radhi hata kurusha ngumi kupinga uamuzi huo ,hata style ya kutoka nje ya bunge si kwa ajili ya kukutetea maslai ya wanachama la hasha ni kwa ajili ya kuwambia wananchi kua tupo

Maskini chadema ndo inazikwa lasmi

Pigo kwa UKAWA na WANANCHI ila kwa wale wavivu wa CCM wanaochapa usingizi bungeni waende na neti kabisa maana wananchi hawatawaona.

Unachoshangilia hapo sijaona mkuu...........
 
Mkuu unaweza kujua ni gharama kiasi gani itatumika kuanzisha hizo wilaya mpya?

Kwa upande wa TBC tutasave bilioni 4.2 /year
 
Kwa hiyo mleta mada unata kutuambia Wilaya na matangazo ya TBC ni vitu viwili vinavyoweza kuwekwa kwenye mizania moja? Kwamba matumizi kwenye matangazo ya moja kwa moja kuhusu mijadala ya 'kuchaniana chupi na kukata shanga' yana tija kama sawa na kuwa na Wilaya?
 
Kwa upande wa kuanzisha wilaya mpya hakuna tutakacho save badala yake tujianda kupoteza zaidi ya Billion 50+.
 
Absolutely, kwasababu hivyo vyote viwili vinahusu matumiza,na ndo hapo tunapoona double standard ikitumika.
Kwa hiyo mleta mada unata kutuambia Wilaya na matangazo ya TBC ni vitu viwili vinavyoweza kuwekwa kwenye mizania moja? Kwamba matumizi kwenye matangazo ya moja kwa moja kuhusu mijadala ya 'kuchaniana chupi na kukata shanga' yana tija kama sawa na kuwa na Wilaya?
 
Kwa hiyo mleta mada unata kutuambia Wilaya na matangazo ya TBC ni vitu viwili vinavyoweza kuwekwa kwenye mizania moja? Kwamba matumizi kwenye matangazo ya moja kwa moja kuhusu mijadala ya 'kuchaniana chupi na kukata shanga' yana tija kama sawa na kuwa na Wilaya?
Unaweza kututanabaishia kuwa in faida gani tunayopata kwa kuanzisha wilaya zingine nani ya jiji LA DAR ESALAAM??.

Hivi hitaji kubwa la watu wa DAR Kwa sasa ni kuongezewa wilaya zingine???.
 
Mkuu unaweza kujua ni gharama kiasi gani itatumika kuanzisha hizo wilaya mpya?

Kwa upande wa TBC tutasave bilioni 4.2 /year

Kwa akili ya kawaida tu ni ghali kuanzisha wilaya hamuwezi kukaribiana na bilioni 4 it's pretty expensive
 
Back
Top Bottom