TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

TBS: Kuanzia 01 Machi 2021, utaratibu wa kukagua magari kutoka nje ya nchi, utafanyikia hapa nchini

hiyo hela ya inspection kwa Tanzania tulikuwa tunaipoteza bure, kwa sababu inspection unalipia inafanyika nje kuna ubaya gani ikifanyika ndani?
Kwani fedha kiasi gani zinapotea kwenda nje? Umeona hiyo inspection tu? Mbona tunaagiza hadi toothpick toka china? Hatupotezi hela hapo?
 
itapunguza hamtolipa hela ya kigeni ile laki 7 badala yake mtalipishwa maybe 1- 2 lakhs only
Sasa wanakuja kukukamata kwenye storage ya TPA maana Japan gari ikienda inspection inachukua wiki 1, pia system ya TBS hadi ije kusoma debit inasumbua ipo slow sana..kwaio inakua ngumu kutoa gari ndani ya siku 7 za grace period ya TPA
 
Mi sioni cha ajabu hapa.
Kwa kuwa, hata sasa hivi ukiagiza gari kutoka Japan, lazima likaguliwe, na utalipia gharama ya kukaguliwa na kampuni ambayo imepata kibali kutoka Tanzania. Tena unalipa kwa $ kati $100 hadi $300 kama mdau alivyosema hapo juu.

Kilichobadilika ni kuwa badala ya kulipia na kukaguliwa Japan, sasa utalipia na kukaguliwa hapa.

Mi naona ni jambo nzuri. Kwanini tuiingizie hela ya ukaguzi Japan badala ya hiyo hela ibaki Tanzania?

Kwanini uangaike ku badilisha hela ya TSh kwenda $ kwa ajili ya kulipia ukaguzi Japan ambapo $ ni gharama badala ya kulipia kwa TSh?
Tunakosea sana kama gari ikikaguliwa hapa maana tunaangalia tunaingiza nini badala ya kufikiri tunaletewa uchafu gani.

Kipindi hiki au cha nyuma ukiagiza gari Japani ikiwa mbovu na wanajua itakwama kwenye inspection wanakwambia ubadili uchukue nyingine. Na kama tatizo ni dogo sana huwa wanarekebisha wenyewe halafu linapelekwa inspection na kuwa exported likiwa na condition nzuri.

Wasi wasi wangu hao wajapani sahizi watatuma magari mabovu bila woga wowote na mwisho wa siku mzigo unakua kwa mnunuaji, sababu inspection itafanyikia Tanzania
 
Sema itasababisha msongamano mkubwa na hivyo kuchelewesha clearance ya magari
Hamna msongamano wa clearance wala nini, ipo hivi unaclear na kulipa kodi zote za serikali, inabaki registration tuu, hapo kama gari ni bovu unakabidhiwa bila usajili ukalitengeneze vitu walivyoainisha, unapewa na muda wa kama mwezi mmoja hivi ukikamilisha matengenezo unapewa vibali vyako
 
Nina mwanangu aliagiza gari hakukagua huko JP. Hatari na nusu.

Gari ikafika wakaenda kukagua NIT gharama knm. Hafu ukirudishwa ni gharama zako kutengeneza. Unaweza kuta ukatumia Million kimasihara hivi hivi.
Huu utaratibu mpya nadhani utakuwa mzuri zaidi na wenye faida kwa mteja na serikali. Kwanza, majukumu ya ukaguzi yatafanywa na watanzania kinyume na awali ambapo ajira hii ya ukaguzi ilikuwa kwa mawakala wa kigeni. Mbili, gharama za ukaguzi za hapa ndani ni nafuu kuliko zile zilizokuwa zinatozwa nje na mawakala. Gari likikutwa bovu, taratibu ni kama zilizokuwa zinafanywa na mawakala. TUKUMBUKE HII SIYO MARA YA KWANZA KUFANYA UKAGUZI WA MAGARI HAPA NCHINI. NA HAMNA CHANGAMOTO ZILIZOJITOKEZA KWA WALIOFANYA UKAGUZI BAADA YA GARI KUFIKA KATIKA BANDARI YETU. Huu ni uamuzi mzuri sana wa serikali ulikuja kwa kuchelewa.
 
Kwani fedha kiasi gani zinapotea kwenda nje? Umeona hiyo inspection tu? Mbona tunaagiza hadi toothpick toka china? Hatupotezi hela hapo?
Hela nyingin sana zinapotea, pamoja na ajira...kumbuka watakaofanya inspection huku Tanzania ni hawa vijana ambao tunalia kila siku hawana ajira, na watakaofanya ufundi wa kurekebisha magari mabovu ni watanzania na hela inabaki tanzania

Sidhani kama umefikiri vizuri kabla ya kuandika comment ya ki wack namna hii...no brainer
 
Sijajua nini faida ya hili jambo...
Sioni faida kwa sababu njia ya mwanzo aina usumbufu. Sasa kama gari linahitaji marekebisho mfano kubadilisha parts, hizo parts zipo hapa nchini za kumwaga, pia kuna vifaa na wataalamu kama wa Japan ukiachilia Dubai?
 
Wazee heb fikirien bas na ajira ngapi zitazalishwa sio kupinga tu kila kitu

Sehem zitakazo kuwa na changamoto toa ushaur kwel wajapan wapige pesa ss tupo tu
 
Shetani anasingiziwaga mengi sana 😂😂😂😂😂😂
Ila uwepo wake muhimu kweli ameokoa ndoa nyingi utasikia tukisema mke wangu tu kemea shetani ndio kanitoa kwenye mstari mnakemea mambo yanakaa sawa! Halikadhalika CCM wana bahati mbaya kweli kweli wame muuwa shetani wao Chadema sijuwi wata kemea nini kwa wana nchi pana kazi ni suala la muda itabidi watafute shetani wao wa ndani wa kukemea ambayo sio poa sana
 
fundi25 hivi waliopewa notice kule Dubai na Japan walikua wameajiri watu gani? Vipi kuhusu gharama na ubora wa kazi waliyokua wanafanya?
 
Ila uwepo wake muhimu kweli ameokoa ndoa nyingi utasikia tukisema mke wangu tu kemea shetani ndio kanitoa kwenye mstari mnakemea mambo yanakaa sawa! Halikadhalika CCM wana bahati mbaya kweli kweli wame muuwa shetani wao Chadema sijuwi wata kemea nini kwa wana nchi pana kazi ni suala la muda itabidi watafute shetani wao wa ndani wa kulemea ambayo sio poa sana
Hahahaaa ila wanaume buana, yaani mnajuaga kutudanganya kama watoto wadogo... tunakemea halafu mkifika kwa huyo mnayetuaminisha ni shetani mnamwita malaika😃

Chadema imara ipo bungeni na ndio wakuu wa vitengo muhimu kule💥
 
Lengo la serikali ni zuri.
1.Kuongeza mapato ambayo yalikuwa yanapotelea nje .
2. Kuongeza ajira kwa vijana.

Tatizo kubwa ni urasimu, tabia iliyoibuka awamu hii ya kubambikia watu kodi na faini na Watanzania kutokuwa waaminifu.

Kama TBS itasimamia vyema kukawa na uaminifu, haki ikatendeka na kuhakikisha hakuna rushwa wala ucheleweshaji jambo hili ni jema.

Tatizo ni hii attitude mpya ya taasisi za serikali kutaka watanzania waishi kama mashetani yan roho mbaya iliyopitiliza.
 
fundi25 hivi waliopewa notice kule Dubai na Japan walikua wameajiri watu gani? Vipi kuhusu gharama na ubora wa kazi waliyokua wanafanya?
Wanaweza kuambia iyo gari ina tatizo
Ukaikubali au ukaikataa ikabadilishwa au ika fanyiwa marekebisho ila sio mara zote!
Gari nyingi hazinaga matatizo! Sasa bahati mbaya gari ikifika hapa kuna matatizo mengi yatakuwa changamoto haswa kwa magari ya kisasa kidogo maana spear nyingine itabidi waagize sensor!
Kuajiri huko wataalam wa ajuzi wa ukaguzi ni wengi na vifaa ni vingi na bei nafuu kuliko huku! Kazi ya ukaguzi inahitaji Dr.mjuzi aliye bobea akisikia tu sauti ya engine bila ku kusogelea anajua tiari shidaha ni nini mara nyingi bila kutumia vipimo ndio sifa kubwa ya ufundi vinginevyo uta tafuta tatizo siku 20 au masaa mengi!
Aina za magari huku kwetu zina badilika kila siku zinaonekana aina mpya hko Ulaya zinajulikana mda na utatuzi wa changamoto zake! Tujiandae kuumia kidogo! Kwanza kitu cha kwanza TBS wata fungua duka la matairi magari yote watataka yabadilishwe tairi...
 
Ngoja tuone wale wenye kuuza magari huko Japan watalifikiaje soko huku wakikidhi vigezo na taratibu bila kupata hasara na tuone process hapa inakuaje
 
Hii nchi inaendelea kuwa ngumu na taabu kubwa kuishi, kwa nini tuharibu maisha ya watu kwenye inchi yetu ? watu wote tutakuwa vibaraka wa kodi km watumwa ?
 
Hahahaaa ila wanaume buana, yaani mnajuaga kutudanganya kama watoto wadogo... tunakemea halafu mkifika kwa huyo mnayetuaminisha ni shetani mnamwita malaika😃

Chadema imara ipo bungeni na ndio wakuu wa vitengo muhimu kule💥
Tunapiga adi magoti shetani m'baya sana moyoni unasema tatizo linakaribia kwisha! Unapiga maneno mazuri shetani anapita maisha yana songa! Ukitoka una nyanyua simu una mpigia jamaa yako unamwambia home kimenuka wife kapandisha mzuka una mpa story anakuambia aahhhh iyo mbona kawaida sana iyo mpango wa kando me mbona ndogo sana me nime mtongoza Mama mkwe na tuka kemea shetani ya kwisha 😂
 
Back
Top Bottom