TBS: Mchele, mafuta ya kupikia ya alizeti na maharage kutoka Marekani, ni Salama kwa Walaji

MUGUFULI tunakukumbuka baba; donor country tumeletewa mchele na maharage yenye virutubisho baba kweli tunafananishwa na kuku wa kisasa , kwanini wasilete nyama kama wanatupenda NYAU HAWA.
 
Ukiiweka hivi sina budi kukazia "sisi tupambane na viongozi wetu tu"
 
Ni kukosa uzalendo kwa nchi yetu .Hakuna kitu kibaya kama kukosa uchungu wa kuipigania nchi Yako ..wenzetu wa china wametushinda hapo tu ..
 
Aiseee mbona wamepima fasta na kupata jibu fasta hivyo? bidhaa nyingine utasikia sampo mpaka iwe nini sijui wana misamiati yao ya kizungu migumu hiyooo! Haya ngoja tuone matokeo yake Mungu aturehemu.
 
Wakuu msada ni msada tu haiwezekani mtu atake kukupa msaada kisha umpangie mashariti

Kama nyinyi mnamchele mwingi Tanzania mbona hao watoto wanashinda na njaa huko mashuleni
 
Reactions: Lax
Endelea kushangaa mkuu, utakuja kushtuka hauna uhuru..
 
Chanjo zimerudi kwa kasi kama hazina akili nzuri, hatujatulia mchele wenye virutubisho nao huo so kupanga ni kuchagua ila kiuhalisia tunajiangamiza sisi wenye kwa kuendekeza umasikini, suala la watoto kula vyakula vyenye virutubisho ni suala la elimu zaidi sio la kimsaada halafu kesho tuje tushangae magonjwa yanatoka wapi wakati tunajikaanga wenyewe.
 
Kama mchele ni salama na mtamu waupeleke IKULU YA SAMIA.

Samia aule huku tunamuangalia kwenye teRevisheni kama alivyojidunga machanjo ya uviko 😹
 
Endelea kushangaa mkuu, utakuja kushtuka hauna uhuru..
Mkuu miaka 62 ya uhuru bado tunapewa misaada kwa ajili ya kupambana na matatizo ya lishe; huo uhuru umetusaidia nini labda.
 
Watanzania kila mara ni ubishi tu. Mbona sukari iliyooingizwa hivi karibuni hamkuuliza kama inafaa kwa matumizi ya binadamu na kama ilithibishwa na TBS.
 
MUGUFULI tunakukumbuka baba; donor country tumeletewa mchele na maharage yenye virutubisho baba kweli tunafananishwa na kuku wa kisasa , kwanini wasilete nyama kama wanatupenda NYAU HAWA.

Watoto wetu wa Shule Wakila Maharage ya michele iliyo ongezwa Virutubisho watapata Madhara kama hawa Kuku wa kisasa ona hizo picha hapo juu.

Je, kuna madhara yoyote ya kula nyama ya kuku wa kisasa kwa muda mrefu?​

Madhara yapo mengi kiafya.
1.unapunguza uwezo wako wa kufkiri maana kuku hao hupewa dawa nyingi zenye madhara kwa binadamu pia kwa kuku wenyewe ndo maana mda wote unawakuta wamesinzi kama mateja jiulize kama kuku huyo utamla wewe utakuwaje??
2.kupunguza nguvu za kiume,kuku hao mpaka wa kuwe wanapewa dawa nyingi,ARV PIAna nyingine kibao,
3.kubadilisha mfumo wa homoni kwa mwanamke piano mwanaume
 
Mkuu
Haya mambo yamekuwa magumu kwa sababu hata waliopewa dhamana wameshindwa kuwa na vision
 
Reactions: Lax
Mkuu Tanzania hatuna njaa unamaanisha??
Unajua ni familia ngapi zina uwezo wa kula milo 3 tena yenye mboga 1?? Ni shule ngapi zinawapa watoto uji?? Halafu tunalalamika watoto wetu hawafaulu wakati hata uwezo wa kuwapa milo bora hatuna
Ndo kitu kinachonshangaza kwa wale wakosoaji wa huu msaada
Kuna shule nyingi tu swala la kula mzigo umebebeshwa wazazi serekali imeshindwa leo watu wanakuja kutokwa na mapovu

Watoto wanashinda na njaa huko shuleni wazazi wanapiga chenga wanapoambiwa wachangie na serekali imeshindwa kuhakikisha wamekula

Kituko cha bashe eti waje wanunue huku yaani mtu anakupa msaada na bado unampangia hiki si kituko, bashe ni mtu anayeongozwa na hisia kuliko akili yaani hafai kuwa kiongozi
 
Wakuu msada ni msada tu haiwezekani mtu atake kukupa msaada kisha umpangie mashariti

Kama nyinyi mnamchele mwingi Tanzania mbona hao watoto wanashinda na njaa huko mashuleni
Umeongea point sana; shule nyingi za serekali wanafunzi wanashinda njaa
 
Swali la msingi;Je ni kweli tuna uhaba wa bidhaa tajwa? Na kama ndio kwani tusifanye namna sisi tukawa ndio wazalishaji wa hizo bidhaa ilhali tuna ardhi ya kutosha?
 
Kwahiyo siku hizi tunaagiza mchele na mafuta ya alizeti kutoka marekani? Basi tuagize na nyanya kutoka UK
sukari si imewasumbua hapa muda mrefu sana? umesahau mafuta ya kupikia kuna kipindi yalifika tsh 45,000 kwa lita 5 ?dogo nyie mbona wasahaulifu sana
 
Mimi kama MwanaNchi nacho hoji Tz Kuna njaa kiasi Cha kusaidiwa chakula kweli? Kwanini tumelia na uhaba wa sukari hawajaleta je tuliomba au wao tu wameona watupe ?

Msaada kama huu ni laana hata kama kwako ukiwa mtu wa kupewa misaada tu ni dalili mbaya sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…