TBS: Mchele, mafuta ya kupikia ya alizeti na maharage kutoka Marekani, ni Salama kwa Walaji

TBS: Mchele, mafuta ya kupikia ya alizeti na maharage kutoka Marekani, ni Salama kwa Walaji

Tbs ni shirika la hovyo tu citu vingapi vipo feki vinauzwa madukani nawao wapi tu wanakula mshahara wa bure tu. Labda wanapima vinavyoenda ikulu tu vyakula
 
Tatizo kubwa ni Elimu Tu.

Na ulimbukeni, eti hatuhitaji huo msaada, yaani watanzania tunahitaji kuelimishwa maana ata ukisoma michango ya watu kweli inasikitisha.

kabla ya kujibu emm tembelea shule za kata za msingi. jaribu kuuliza kuhusu chakula uone majibu utakayopewa. Yaani mtoto wa maskini kuletewa wali matajiri wanamdanganya asiule eti kisa haujalimwa nchini.

Fungeni midomo nyie nyote msio na midomo ya kusema asante, kama wewe unacho basi usimsemee ambae hana. Kilicho wajaa ni udini, ubinafsi na umbea.

Hao hao walitoa zaidi ya billion 200 wakaelezea kua serikali ichague vijana itumie hiyo b.200 kama mtaji waweze kujijenga kwenye kilimo matokeo yake yamekuaje?
Unajifanya una uchungu kumbe huna lolote.

Tapeli tu.
 
Nchi hii ni shida sana,lini shirika kama TBS litajitegemea na kufanya kazi yake bila ya shinikizo la politicians?hizi GM ni hapana
Hivyo virutubisho vinatengenezwa na MONSANTO kampuni ijulikanayo kwa kutengeneza genetically modified foods!
Target yao ni wanafunzi ambao muda si mrefu wataanza kufanya mapenzi ya jinsi a moja kwasababu hormones zao zitakuwa z imebadilika’!! Halafu mtaanza kutafuta mchawi kumbe nyie ndio mmewaloga watoto wenu.
 
Swala sio usalama,kwani Tanzania tuna njaa Hadi tupewe Msaada? Hoja ni kuidhalilisha Nchi.

Pia Waziri amesema waje wanunue mazao yetu.Mwisho angekuwa Mwendazake angestamtimua Mkurugenzi wa TBS
Hii ni baadhi ya misaada kutoka Marekani kwa Tanzania kwa miongo kadhaa, halafu jiulize ni lini tuliwahi kuikataa kabla ya kuukataa huo mchele;
1. Chanjo mbalimbali
2. Ujenzi wa mashimo ya vyoo
3. Vyandarua vya wajawazito
4. Condoms
5. ARVs
 
Alichofanya bashe ni sawa na alichofanya mkurugenz wa tbs ni sawa, kama unaakili za kutafuta buku7 huwez kuelewa kitu
 
Hivyo virutubisho vinatengenezwa na MONSANTO kampuni ijulikanayo kwa kutengeneza genetically modified foods!
Target yao ni wanafunzi ambao muda si mrefu wataanza kufanya mapenzi ya jinsi a moja kwasababu hormones zao zitakuwa z imebadilika’!! Halafu mtaanza kutafuta mchawi kumbe nyie ndio mmewaloga watoto wenu.
Hii ni akili ya kuvukia barabara.
Hujui chochote kuhusu sayansi, umekaririshwa.

Fahamu tu, wapenzi wa jinsia moja ni matokeo ya watu kubadili mifumo ya kufikiri, mitazamo ya asili ya kijamii, fikra za kimaumbile na akili (yaani akili zilizoharibiwa!), ambapo watu wenye malengo hayo watakuhamasisha, kukufundisha, kukuonyesha na kukusikilizisha content zenye mlengo huo wa mapenzi ya jinsia moja. Na kama USA wanataka hayo, wanayafanya kupitia media wanazozimiliki (Whatsapp, Google, Facebook, Twitter, instagram, Telegram, Tiktok nk) app ambazo wewe unazo kwenye device yako hapo ulipo.

Na ikiwa unazani, wanataka kuharibu hormone za watoto basi hawataleta hizo mambo kupitia vyakula vichache vya msaada bali kupitia chanjo za wajawazito, chanjo za watoto, dawa na chanjo za mifugo (kuku, ng'ombe, nguruwe, mbuzi, kondoo), mbegu za mazao, maziwa ya kopo, vyakula vya kusindika, vinywaji baridi (Cocacola, Pepsi nk)
 
Hii ni baadhi ya misaada kutoka Marekani kwa Tanzania kwa miongo kadhaa, halafu jiulize ni lini tuliwahi kuikataa kabla ya kuukataa huo mchele;
1. Chanjo mbalimbali
2. Ujenzi wa mashimo ya vyoo
3. Vyandarua vya wajawazito
4. Condoms
5. ARVs
Hizo Misaada hapo hatuna ila msosi tunao.

Angekuwa Magufuli angeshamtimua huyo Mkuu wa TBS.
 
Hakuna siku mchele utatoka USA harafu TBS wakaja kutoa taarifa za chakula Halifax tunachoweza ni kuchoma moto vifaranga kutoka Kenya...
 
Mimi nilishangaa watu walivyokuwa wanatoka povu kuhusu hii ishu. Kwamba NGO iingize vyakula bili idhini ya mamlaka husika??

Alichofanya Waziri ni damage control baada ya watu kuhoji. Hii program iko muda na uongezaji wa virutubishi haujaanza leo na upo kisheria.

Mbona tunakula unga wa ngano, mahindi, mafuta na chumvi vyote vimeongezwa virutubishi, hivyo virutubishi tunateneneza sisi??

BTW wakitaka kutumaliza hawashindwi.. wanaanzia kwenye dawa na chanjo za bure. Hatutaki hiyo misaada tujikwamue kiuchumi!!
Bora usemee wee
 
Tanzania hatuna mchele mpaka tuletewe msaada kutoka marekani? Kwanini wasitowe fedha tununue kwa wakulima wetu hapa hapa nchini?
Kwann hao wakulima wasipeleke huo mchele wao huko mashuleni, kwan watoto wa nan wanakula? Mnapangia watu matumizi ya pesa zao? Lol
 
Wewe ndugu yangu usije taka kula mchele tyu huku usijue baada ya kushiba utalipa nini?[emoji23][emoji1787]

Oy Rafiki sisi tule ugali tu bwana tukipata sawa
Wee nae huna hata unachokijua, unalishwa na kuveshwa unabaki kuongea ujinga, unaijua njaa wee? Kuna familia hata ugali huo haupo.
 
Wamesha lamba asali bila shaka, mbona kauli zao zinakinzana na za Bashe?
Inamaana Bashe alitoa ile kauli kabla ya kuwasiliana na wataalamu wa TBS!? Kama alifanya hivyo hilo ni kosa kubwa sana, mambo ya kitaalam tuachiea wataalamu wa fani zao!!!
 
MUGUFULI tunakukumbuka baba; donor country tumeletewa mchele na maharage yenye virutubisho baba kweli tunafananishwa na kuku wa kisasa , kwanini wasilete nyama kama wanatupenda NYAU HAWA.
Ila ARV, chanjo, na madawa mengine je? Hivi nyie mko timamu?
 
Hivyo virutubisho vinatengenezwa na MONSANTO kampuni ijulikanayo kwa kutengeneza genetically modified foods!
Target yao ni wanafunzi ambao muda si mrefu wataanza kufanya mapenzi ya jinsi a moja kwasababu hormones zao zitakuwa z imebadilika’!! Halafu mtaanza kutafuta mchawi kumbe nyie ndio mmewaloga watoto wenu.
Hivi nyie mnawaza ushoga sanaa? Ushoga uko hapa kabla ya hiyo misaada, na wakitaka kuuleta ushoga watauleta kwa mbinu yoyote tyuuh.
Wala hamuwezi zuia.
 
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limesema mchele, mafuta ya kupikia ya alizeti na maharage ambavyo vyote vimeongezwa Virutubishi vilivyotolewa na Wizara ya Kilimo ya Marekani kwa ushirikiano na Taasisi ya Jumuiya za Kimataifa (Global communities) kwa baadhi ya Shule za Dodoma, vyote ni salama kwa Walaji

TBS imesema taratibu za uingizwaji wa chakula Nchini zilifuatwa ikiwemo ukaguzi na uchunguzi wa Kimaabara

Meneja Uhusiano na Masoko wa TBS, Gladness Kaseka amesema "Utaratibu wa kuongeza virutubishi kwenye chakula (food fortification) unakubalika kitaalamu na hufanyika kwa lengo la kuboresha hali ya lishe kwa walaji.

Pia, soma; Hussein Bashe, Waziri wa Kilimo: Waagizaji hawakupaswa kuleta mchele wa Msaada kutoka Marekani kwani Tanzania ina hazina ya mchele


Yawezekana upo sahihi kaka ila wamarekani wenyewe wanasema hivi




View attachment 2937939
Huu upendo umeanza lini?
 
Back
Top Bottom