TBT: Ulipokea matokeo yako ya Form Four ukiwa wapi, na ilikuwaje?

Nilikuwa tabora kwenye kochi la shemejii, nikalipuka kwa furaha ya ajabu.

Enzi hizo namiliki ITEL KITOCHI, basi nikapigiwa simu nikaambiwa nimepata DIVISHENI TWO. Niligaragaraa nikachana shatii huku watu wamenibeba juu.

Watu walikuwa wananisifia na kuniita GENIUS, maana kwenye shule yetu tulifaulu 10 tu kati ya 200.

Nilivimba komwe, bichwa likawa kubwa nikawa kama mfalme wa nyumba, FATHER HOUSEEE.

Wakati huo waliopata MADIVISHENI FOO wananionea gere balaaa.... nikawaambia wakafungue kiwanda cha CHEREHANI.

Depal

Nyani Ngabu
 
Kochi la nani 🀣🀣
 
Hhahahhaha kipindi hicho wazazi wang walikuwa tayari wameshaniandalia zana za kilimo wakijuwa kuwa siwez kufaulu kamwe hvyo nipelekwe shambani Kisha baadae nitafutiwe mke nioe

Ajabu zilivyotoka niliwaduwaza kijij kizima kwan mm pekee ndio nimefaulu kwa kiwango kikubwa kijij pale hkn mpk leo aliyefunja record hyo mkp sasa nashikilia mm
 
Mimi ilikuwa mwaka 20__.
Nilikuwa zangu nyumbani nimetulia naperuzi tu.

Ila nilifurahi sana
Yako yalikukutia wapi, na ilikuwaje?
MUNGU NI MWEMA WAKATI WOTEEEEE
Ningefail shule ninge umia from local government school kijijini sanaa na nilikuaga mnyonge siongei mkimya sanaaa ila ndani yangu na ndugu marafiki hawakuamini kama ntatoboa...

Ndani yangu nilikua kama THE UNDERTAKER au THE BEAST (BLOCK LIESNER) wale wa WWE nilikua napiga msuli TEMBO ila Kwa kua sikuaga mtu wa matambo nikawa UNDERRATED

Thanks salva my classmate form 1
ulijenga msingi bora wa kujitegemea formula zetu ilikua ni kusoma somo husika Kila kitu maana sisi hatukupenda kupata shida au tabu kwenye EXAMINATION ROOM na ndio maana may mosi ulichukua ufanyakazi bora..

Matokeo yangu yaliwanyamazisha ndugu , jamaa na marafiki na wote walio ni underrate

Maana Kuna walio peleka watoto wao shule za mapesa Mingi ila nikawakalisha from local government school kijijini sanaa ....

Kabatini Nina degree 3 nikizimiss naziangalia😊😊

Na sio za kuombea ajira maana wengine tulisha tokaga huko
 
Mimi ilikuwa mwaka 20__.
Nilikuwa zangu nyumbani nimetulia naperuzi tu.

Ila nilifurahi sana
Yako yalikukutia wapi, na ilikuwaje?
Nilikuwa kijijini nachunga ng'ombe, niliporudi jioni nikapokelewa na Pongezi kuwa nina Div I ya kuchechemea, nilifurahi sana maana masomo niliyoyapenda nilifaulu yote.

Kingine, nilikuwa kibonde wa Kiswahili nikakuta nina karai langu safi tu jambo ambalo nilitegemea kupata F na kuhofia kupigwa penati sababu kuna mwanafunzi aliwahi kupigwa penati kwa kupata F ya Kiswahili kwenye shule yetu.
 
πŸ‘πŸ‘
 
πŸ™ŒπŸ™Œ
 
πŸ€£πŸ€£πŸ™ŒπŸ™Œ
 
Huko kufanya kazi tofauti na ulichosomea imekuwa kawaida sana siku hizi.
 
Nakumbuka yalinikuta sina hili wala lile najaza choo tu ndani
Saa kumi na dakika zake nakumbuka nimeshtuka toka usingizini nilipumzisha fuvu nashika simu angu nakuta missed call za kutosha (40 missed calls) kama rapcha ila mm sasa ilikua dada angu kanipigia kama mara 13, mshkaji wangu Lee huyu tumesoma wote from primary to UNI mpka leo we brothers, na ndgu wengine vihelele tu kunikata stimu nao walipiga.
Sasa bhna mtu wa kwnza kumrukia hewani alikua huyo Lee msela wangu maana wengine nawajua wangeharibu siku, khaaaa msela kupokea simu anaongea kama anakata roho kajiongeza nkamwambia ngoja nakupigia bro, nkawa sina hata papara na mtu mm hua najiamin ujinga, nkaoga taratibu kabisa na kuimba nisepe kuchukua vocha nicheck mwenyewe maana bi mkubwa alikua kajikaza mama wa watu kaninunulia mwanae pc slim hp nilikua natamba nayo back in the days nayo pia alininunulia blackberry simu nadhani mtakua mnazifahamu na wakati niko form IV alinipangishia chumba karibu na shule niliokua nasoma kijana wake niwe karibu na elimu, walimu na shule maana alikua akini aminia kijana wake kiufupi alitisha vitu Vidgo vdgo nilikua nikimuomba.
Haya bhna nkamaliza kuoga ile natoka sijafika hata dukani ujumbe ukaingia kweny sim yngu kufungua ni sister wangu kajiongeza ubwa yule kumbe wameongea na ni mkubwa kampa namba yangu kwahio Kumbe wenzangu wanajua matokeo yangu mm nadhani ntakua wa kwnza kuwapa habari njema, sijafungua hata message imeingia nyengine sasa iyo nyengine ndo nkafungua nakuta sister kasema kiufupi hapo una mswaki [emoji23][emoji23][emoji23] kama mazuri ila that day mda ule nilihisi mifupa ya mwili mzima inauma afu kama nikapigwa na kitu kizito kichwani nkashindwa ata kutembea ikabd nimpigie bi mkubwa ila hakupatikana nkarudi ndani nkapitiwa na usingizi mzito balaa mara naskia mlango unafunguliwa ni bi mkubwa katoka kazini nkamuwahi kumpokea cha kwnza akauliza vipi matokeo kipenzi changu aiseee nililia ila bi mkubwa akanambia usilie mwanangu hiyo ni hatua moja kabla nyingi zijazo know yourself baada ya mda mfupi nkaja kuitwa na dgo tukatoka bi mkubwa bhna akatutoa out kula kuku mm na dgo maana tumeishi watatu tu na sister alikua akiishi na bibi afu yupo chuo.
Ila usiku nilimsikia bi mkubwa chumbani kwake analia na kuomba nkawa na umia kweli kweli na sijawai kufeli tena
 
2012 ilikuwa ya moto sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…