Nakumbuka yalinikuta sina hili wala lile najaza choo tu ndani
Saa kumi na dakika zake nakumbuka nimeshtuka toka usingizini nilipumzisha fuvu nashika simu angu nakuta missed call za kutosha (40 missed calls) kama rapcha ila mm sasa ilikua dada angu kanipigia kama mara 13, mshkaji wangu Lee huyu tumesoma wote from primary to UNI mpka leo we brothers, na ndgu wengine vihelele tu kunikata stimu nao walipiga.
Sasa bhna mtu wa kwnza kumrukia hewani alikua huyo Lee msela wangu maana wengine nawajua wangeharibu siku, khaaaa msela kupokea simu anaongea kama anakata roho kajiongeza nkamwambia ngoja nakupigia bro, nkawa sina hata papara na mtu mm hua najiamin ujinga, nkaoga taratibu kabisa na kuimba nisepe kuchukua vocha nicheck mwenyewe maana bi mkubwa alikua kajikaza mama wa watu kaninunulia mwanae pc slim hp nilikua natamba nayo back in the days nayo pia alininunulia blackberry simu nadhani mtakua mnazifahamu na wakati niko form IV alinipangishia chumba karibu na shule niliokua nasoma kijana wake niwe karibu na elimu, walimu na shule maana alikua akini aminia kijana wake kiufupi alitisha vitu Vidgo vdgo nilikua nikimuomba.
Haya bhna nkamaliza kuoga ile natoka sijafika hata dukani ujumbe ukaingia kweny sim yngu kufungua ni sister wangu kajiongeza ubwa yule kumbe wameongea na ni mkubwa kampa namba yangu kwahio Kumbe wenzangu wanajua matokeo yangu mm nadhani ntakua wa kwnza kuwapa habari njema, sijafungua hata message imeingia nyengine sasa iyo nyengine ndo nkafungua nakuta sister kasema kiufupi hapo una mswaki [emoji23][emoji23][emoji23] kama mazuri ila that day mda ule nilihisi mifupa ya mwili mzima inauma afu kama nikapigwa na kitu kizito kichwani nkashindwa ata kutembea ikabd nimpigie bi mkubwa ila hakupatikana nkarudi ndani nkapitiwa na usingizi mzito balaa mara naskia mlango unafunguliwa ni bi mkubwa katoka kazini nkamuwahi kumpokea cha kwnza akauliza vipi matokeo kipenzi changu aiseee nililia ila bi mkubwa akanambia usilie mwanangu hiyo ni hatua moja kabla nyingi zijazo know yourself baada ya mda mfupi nkaja kuitwa na dgo tukatoka bi mkubwa bhna akatutoa out kula kuku mm na dgo maana tumeishi watatu tu na sister alikua akiishi na bibi afu yupo chuo.
Ila usiku nilimsikia bi mkubwa chumbani kwake analia na kuomba nkawa na umia kweli kweli na sijawai kufeli tena