Poor Brain
JF-Expert Member
- Jul 5, 2019
- 19,644
- 40,546
Wewe nakuonya tena..... usini'misquote' ndugu!, ... juzijuzi tu nilikuwa Kawe!
๐
Utapigwa ๐๐๐๐
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe nakuonya tena..... usini'misquote' ndugu!, ... juzijuzi tu nilikuwa Kawe!
๐
๐๐ Kuna walevi wa MI walikuja kuropoka kwamba watu wa orodha C walitak kuongezewa mafungu kwenye tradeeeee. ๐คธ Haya ya Gongo la mbotoSikuwepo ila kila nikitazama rejea za hayo matukio mawili kwenye madhara naona picha za unguided rockets na waandishi ndio wanaita jina la kiujumla kuwa ni mabomu. Roketi zenyewe naona nyingi zikizidi sana zitakuwa 220mm au hata ndogo 122mm.
Yawezekana mabomu ndio yalilipukia kambini na kuleta madhara makubwa ambayo hayakuonekana kwa public alafu mizinga ikaruka sehemu mbalimbali. Ila ilikuwa ni milipuko midogo sio missiles zile wala sio rockets kubwa kama 300mm.
Duh noma sanaNinachokumbuka tu ni dada mmoja akiwa na underwear pekee alikutwa msimbazi center anashindwa hata kueleza amefikaje hapo katika hali hiyo.
Basi baada ya kutulia na wasamaria kumsitiri ndio akaanza kutiririka anasema ilikuwa majira ya saa tatu kasoro usiku alikuwa ametoka bafuni kuoga akiwa na amejifunga kanga na kuingia ndani ile amevaa underwear akasikia mlipuko, ikabidi atoke na kanga yake ila hakukumbuka kurudi tena ndani kwa yaliyotokea,
Waziri wa Ulinzi hakuhojiwa na Polisi.
Nakumbuka pia Rais Ali Hassan Mwinyi alikuwa anasema," Nchi yetu safi kabisa. Siyo kama jirani zetu. Hapa hatuzalishi wakimbizi. Hapa tunapokea wakimbizi."
Kesho yake yale mabomu yakalipuka na wakimbizi wengi walikwenda Stadium.
Halafu nasikia watoto wengi walipotea.
Af,nakumbuka nilikuwa nimefunga kula chakula for two weeks non-stop .
Niko Mikocheni naisikiliza Ile milipuko inadunda kwenye moyo wangu.
Nikashukuru siko karibu kule.
Halafu ilikuwepo tafrifa kwenye garden ya Ikulu
Nilikuwa na - chat na yule Kamanda wa Jeshi anaitwa Mbowe, alikuwa Jeshini amekamatwa finances za Jeshi.
Nikamuuliza unamfahamu Freeman.
Akasema ni,sijui alisemaje,yule Freeman ni mdogo wangu au kama mtoto wangu.
Basi kesho yake asubuhi,for some reason, Kikwete akamchagua yule kuiongoza tume ya kupelekeza lile tukio.
Kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia matukio muhimu ya kiusalama nchini, milipuko ya mabomu katika maghala ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Mbagala mwaka 2009 na Gongo la Mboto mwaka 2011 ni miongoni mwa matukio yaliyoshtua taifa zima.
Tukio la kwanza la Mbagala lilitokea Aprili 29, 2009, na miaka miwili baadaye, Februari 16, 2011, milipuko mingine ilitikisa Gongo la Mboto, na kusababisha vifo, majeruhi, na uharibifu mkubwa wa mali.
Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, chanzo cha milipuko yote miwili kilihusisha hali duni ya hifadhi ya mabomu na vifaa vya kijeshi. Ghala zilizohifadhi mabomu hayo zilikuwa na changamoto za miundombinu, ikiwemo uchakavu wa silaha zilizohifadhiwa.
Hii ilisababisha ajali ya kwanza Mbagala, na kisha Gongo la Mboto, ambako hali kama hiyo ilijirudia. Mabomu yalilipuka na kusambaa kwa umbali mkubwa, yakiharibu miundombinu ya kijamii kama nyumba, shule, na hospitali.
Matukio haya yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 50 kwa ujumla, na kujeruhi mamia ya raia. Wengi walipoteza makazi yao huku maelfu ya nyumba zikiharibika. Kwa mfano, baada ya milipuko ya Mbagala, zaidi ya watu 7,000 walihitaji msaada wa haraka wa makazi. Vifo na uharibifu wa mali vilileta huzuni na taharuki, huku jamii ikibaki na maswali mengi kuhusu usalama wa maghala ya silaha yaliyokaribu na makazi ya watu.
Serikali ilichukua hatua za haraka kutoa msaada kwa waathirika, huku Rais wa wakati huo, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na aliyekua waziri wa Ulinzi wa kipindi hiko Mh. Dr. Hussain Mwinyi, wakitembelea maeneo ya matukio yote mawili.
Rais Kikwete aliahidi uchunguzi na fidia kwa waathirika. Hata hivyo, mijadala ilizuka kuhusu iwapo hatua zilizochukuliwa na serikali zilikuwa za kutosha au kama matatizo ya msingi ya usalama wa hifadhi ya silaha yalishughulikiwa kikamilifu.
Mbali na vifo na majeruhi, madhara ya kiuchumi yalikuwa makubwa. Serikali ililazimika kutumia rasilimali nyingi kutoa misaada kwa waathirika, wakati raia wengi waliopoteza mali zao walibaki na mzigo wa kurejesha maisha yao. Biashara, makazi, na miundombinu mingine iliyoathiriwa vilihitaji kurekebishwa upya, na baadhi ya maeneo yaliathirika kwa muda mrefu.
Katika tukio la gongo la mboto, aliyekua meya wa Ilala kwa kipindi hicho Mh. Jerry Silla alitoa report iliyoainisha idadi ya majeruhu na vifo, japo report hiyo ilipingwa sana kwa kipindi hiko huku wananchi wakiwa wanahofia kuwa idadi ya watu iliyotajwa ni ndogo kuliko uhalisia
Matukio haya yalifungua mjadala mzito kuhusu usalama wa raia wanaoishi karibu na maghala ya silaha. Wananchi walitilia shaka uwezo wa JWTZ na vyombo vingine vya serikali kudhibiti silaha kwa viwango vinavyohakikisha usalama wa raia. Maswali yalizuka kuhusu kwa nini mabomu haya yaliachwa kuhifadhiwa katika hali duni na ni kwa namna gani serikali inaweza kuhakikisha kwamba milipuko kama hiyo haitatokea tena.
Miaka kadhaa baada ya matukio haya, tunapaswa kujiuliza, je, tumejifunza vya kutosha ili kuzuia ajali kama hizi kutokea tena? Serikali iliahidi kuboresha viwango vya usalama wa maghala ya silaha, lakini bado kuna mijadala kuhusu kama hatua za kutosha zimechukuliwa.
Kwa kuwa matukio haya yanaacha alama kubwa katika historia ya Tanzania, na ikiwa leo ni alhamisi ya TBT, em tuambie unakumbuka nini kuhusu matukio haya?๐คท๐ฝโโ๏ธ
View: https://youtu.be/tEmOeOKWcEI?si=B2xOxjCrBjG9HQE2
PIA SOMA:
Kila kitu kina muda wake wa kuisha matumizi na kina maelezo kihifadhiwe katika mazingira Gani.Mlipuko wa hayo mabomu ilikuwa ni uzembe wa hali juu sana.
Mpaka leo najiuliza wanaokimbia marathon mapafu yao yakoje? Niliongozana na baba aliyekuwa na kichanga cha approx chini ya miezi 3, hakijafunikwa chochote. Ikabidi nimpatie kanga niliyokuwa nayo amfunike. Namuuliza mamake yuko wapi, kosa, ndio kaanza kilio mke wangu..mke wangu...Ama, nikajiongezea mbio kunusuru ya kwangu...
Sana tuAisee, kuna waliobeba mpaka paka wakifikiri ni watoto. Aisee itoshe kusema Amani ni muhimu sana.
Kikwete hakuwa mhusika wa armoury au ammunition depot yoyote jeshini. Jeshi lenyewe ndio lilifanya uzembe, suala la kuharibu silaha chakavu nalo limsubiri Rais?Naunga mkono hoja, japo wapo wanaodai kuwa Kikwete aliambiwa mapema atoe hela kwaajili ya kufanyia maintenance ayo mabomo akagoma
Yes, namaanisha hawakupewa mpunga wa kufanyia maintenance ayo mabomuKikwete hakuwa mhusika wa armoury au ammunition depot yoyote jeshini. Jeshi lenyewe ndio lilifanya uzembe, suala la kuharibu silaha chakavu nalo limsubiri Rais?
Sasa kazi ya maofisa wa jeshi ni nini au unamaanisha hawakupewa bajeti.
Aisee, noma sanaa duhIlikuwa mida ya saa saba kwenda Saa nane mchana nakumbuka tulikuwa darasani kipindi cha Physics mwalimu akiwa mzee mmoja anaitwa Nzohi.
Ghafla tukaanza kusikia vishindo na ngurumo kama radi, hakuna aliyeuliza kuna nini watu wote tulijikuta mlangoni tukigombania kutoka, kufika nje tukakutana na class ya PCB nao wanakuja mbio upande wa class za PCM kuuliza ni nini Hamna mwenye jibu but inaonekana matatizo yapo huko upande wa mbele ya shule.
Basi almost shule nzima ikaelekea upande wa bonden like kama unaenda kisarawe, sasa kuna makombora yakalipuka huko yakaja na kipande cha roof ya huko jeshini, yakaangukia huko pondi (bondeni) kwa waliosoma pugu wanapajua bondeni aka pond au kwa mama P njia ya kwenda kwa mkandawile.
Watu wote tukaanza kurudi mbio tena shulen, kufika nusu ya mlima tunakutana na rundo la wanajesh nao wanakimbia kuja huku bonden pond, aisee ilikuwa ni mshike mshike haswaa! Wananchi, wanajeshi kwa wanafunzi kila mtu na njia yake.
Madhara yalikuwa mengi kwenye mali na vifo!
Hayo Ndo nakumbuka kwa ufupi.
Mshangazi na bichwa komwe hakika hawajawahi kuwa seriousNakumbuka bomu moja lilitua vilivyo kwenye WOWOWO LANGU, lakini bahati nzuri nilikua nimevaa kigodoro .....lile bomu halikuleta madhara makubwa japo kigodoro kilifyatuka chote.
Cc: Kapeace Kalpana Mpaji Mungu Lloyd Munroe Poor Brain Extrovert Bantu Lady binti kiziwi mshamba_hachekwi cocastic Lamomy
Kama inafaa, share mkasa mkuu.Doh! Hiyo siku 2011, ni kama umenitonesha kidonda!
Mm si mwandishi nzuri lkn ningetiririka vilivyo. Kwa kifupi nilikuwa naishi Goms kipindi hicho, na nilipotelewa na binti yangu wa miaka 7 akapatikana Viwanja vya Sabasaba baada ya siku 3. Namshukuru muumba alikuwa mzima kitu ambacho hatukukitegemea kabisaa!Kama inafaa, share mkasa mkuu.
Mm si mwandishi nzuri lkn ningetiririka vilivyo. Kwa kifupi nilikuwa naishi Goms kipindi hicho, na nilipotelewa na binti yangu wa miaka 7 akapatikana Viwanja vya Sabasaba baada ya siku 3. Namshukuru muumba alikuwa mzima kitu ambacho hatukukitegemea kabisaa!