TBT: Unakumbuka nini kuhusu mabomu ya Mbagala (2009) na Gongo la Mboto (2011)?

TBT: Unakumbuka nini kuhusu mabomu ya Mbagala (2009) na Gongo la Mboto (2011)?

Tupe story kidogo aisee😁
Mpaka leo najiuliza wanaokimbia marathon mapafu yao yakoje? Niliongozana na baba aliyekuwa na kichanga cha approx chini ya miezi 3, hakijafunikwa chochote. Ikabidi nimpatie kanga niliyokuwa nayo amfunike. Namuuliza mamake yuko wapi, kosa, ndio kaanza kilio mke wangu..mke wangu...Ama, nikajiongezea mbio kunusuru ya kwangu...
 
Mpaka leo najiuliza wanaokimbia marathon mapafu yao yakoje? Niliongozana na baba aliyekuwa na kichanga cha approx chini ya miezi 3, hakijafunikwa chochote. Ikabidi nimpatie kanga niliyokuwa nayo amfunike. Namuuliza mamake yuko wapi, kosa, ndio kaanza kilio mke wangu..mke wangu...Ama, nikajiongezea mbio kunusuru ya kwangu...
poleni sana!
 
Watanzania hatuko makini na hivyo vyote ulivyotaja, binafsi sikuwahi hata kuwazia vita, ile ya Mbagala yenyewe mpaka nilipoona magari ya Polisi yanaelekea huko. Hii ya Gongolamboto wengi tulikuwa tunadhani ni Diwali ile ya Wahindi, lakini nilijiuliza sana lakini mbona Diwali fataki huwa maeneo ya Posta Posta!!
Ukahisi Diwali gani ipo Gongolamboto, hukujiuliza Wahindi gani waishi uko.
 
Ya mbagala nilikua nipo mkoani kipindi hicho nasoma...

Ila haya ya juzi ya gongo la mboto..

Picha linaanza siku hiyo mchana nilienda bwawani kuoga.. nikaibiwa nguo zangu.. kipindi hicho tunakaa kule mbande sehemu moja wanapaita kwa tinyango...

Kwa tinyango miaka hiyo kulikua kuna njia ya magaro yale ya mchanga (selela)..
Siku hiyo nimeibiwa nguo narudi hom mama alinichapa kinoma noma..
Nikasusa na kula kabisa.. siku hiyo mchana sikupata menu.

Imefika sa 12 tukaanza kusikia kwa mbaaaali milio ya mabomu..
Kwa mda huo tulikua hatuelewi kitu chochote kile...

Sa 2 juu ya alama ndio mambo yalianza changanya hapo mambo yakawa vururu valala..

Ila kufupisha story tulitembea kwa mguu kutoka mbande tukapita ndani ndani mpaka mwanambaya.... Moja kwa moja mpaka mkuranga...

Tukaridishwa kesho yake kwa msaada wa polisi...
 
Hii ilionesha ni namna Gani hili jeshi la wavunja matofali lilivyo na uwezo mdogo kijeshi.Yaani silaha tu kuzihifadhi vizuri limeshindwa Hadi imepelekea milipuko kutokana na uchakavu na mazingira mabovu?.Kama kutunza tu limeshindwa je wanauwezo kweli wa kuenda na wakati kama majeshi mengine kama jeshi la Rwanda.
Jeshi lolote lile duniani mlipuko kwenye ghala la silaha unaweza tokea.
Pia, Rwanda ni nchi yenye uwezo wa kawaida sana kijeshi wala sio wa kuwalinganisha na Tanzania kivita.
 
Kwa wale ambao wamekuwa wakifuatilia matukio muhimu ya kiusalama nchini, milipuko ya mabomu katika maghala ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) huko Mbagala mwaka 2009 na Gongo la Mboto mwaka 2011 ni miongoni mwa matukio yaliyoshtua taifa zima.

Tukio la kwanza la Mbagala lilitokea Aprili 29, 2009, na miaka miwili baadaye, Februari 16, 2011, milipuko mingine ilitikisa Gongo la Mboto, na kusababisha vifo, majeruhi, na uharibifu mkubwa wa mali.

Kwa mujibu wa uchunguzi wa awali, chanzo cha milipuko yote miwili kilihusisha hali duni ya hifadhi ya mabomu na vifaa vya kijeshi. Ghala zilizohifadhi mabomu hayo zilikuwa na changamoto za miundombinu, ikiwemo uchakavu wa silaha zilizohifadhiwa.

Hii ilisababisha ajali ya kwanza Mbagala, na kisha Gongo la Mboto, ambako hali kama hiyo ilijirudia. Mabomu yalilipuka na kusambaa kwa umbali mkubwa, yakiharibu miundombinu ya kijamii kama nyumba, shule, na hospitali.

Matukio haya yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 50 kwa ujumla, na kujeruhi mamia ya raia. Wengi walipoteza makazi yao huku maelfu ya nyumba zikiharibika. Kwa mfano, baada ya milipuko ya Mbagala, zaidi ya watu 7,000 walihitaji msaada wa haraka wa makazi. Vifo na uharibifu wa mali vilileta huzuni na taharuki, huku jamii ikibaki na maswali mengi kuhusu usalama wa maghala ya silaha yaliyokaribu na makazi ya watu.

Serikali ilichukua hatua za haraka kutoa msaada kwa waathirika, huku Rais wa wakati huo, Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na aliyekua waziri wa Ulinzi wa kipindi hiko Mh. Dr. Hussain Mwinyi, wakitembelea maeneo ya matukio yote mawili.​


Rais Kikwete aliahidi uchunguzi na fidia kwa waathirika. Hata hivyo, mijadala ilizuka kuhusu iwapo hatua zilizochukuliwa na serikali zilikuwa za kutosha au kama matatizo ya msingi ya usalama wa hifadhi ya silaha yalishughulikiwa kikamilifu.

Mbali na vifo na majeruhi, madhara ya kiuchumi yalikuwa makubwa. Serikali ililazimika kutumia rasilimali nyingi kutoa misaada kwa waathirika, wakati raia wengi waliopoteza mali zao walibaki na mzigo wa kurejesha maisha yao. Biashara, makazi, na miundombinu mingine iliyoathiriwa vilihitaji kurekebishwa upya, na baadhi ya maeneo yaliathirika kwa muda mrefu.

Katika tukio la gongo la mboto, aliyekua meya wa Ilala kwa kipindi hicho Mh. Jerry Silla alitoa report iliyoainisha idadi ya majeruhu na vifo, japo report hiyo ilipingwa sana kwa kipindi hiko huku wananchi wakiwa wanahofia kuwa idadi ya watu iliyotajwa ni ndogo kuliko uhalisia


Matukio haya yalifungua mjadala mzito kuhusu usalama wa raia wanaoishi karibu na maghala ya silaha. Wananchi walitilia shaka uwezo wa JWTZ na vyombo vingine vya serikali kudhibiti silaha kwa viwango vinavyohakikisha usalama wa raia. Maswali yalizuka kuhusu kwa nini mabomu haya yaliachwa kuhifadhiwa katika hali duni na ni kwa namna gani serikali inaweza kuhakikisha kwamba milipuko kama hiyo haitatokea tena.

Miaka kadhaa baada ya matukio haya, tunapaswa kujiuliza, je, tumejifunza vya kutosha ili kuzuia ajali kama hizi kutokea tena? Serikali iliahidi kuboresha viwango vya usalama wa maghala ya silaha, lakini bado kuna mijadala kuhusu kama hatua za kutosha zimechukuliwa.

Kwa kuwa matukio haya yanaacha alama kubwa katika historia ya Tanzania, na ikiwa leo ni alhamisi ya TBT, em tuambie unakumbuka nini kuhusu matukio haya?🤷🏽‍♂️​


View: https://youtu.be/tEmOeOKWcEI?si=B2xOxjCrBjG9HQE2

PIA SOMA:
  1. Thread 'Tukumbushane yaliyojiri mlipuko wa mabomu ya Gongo la Mboto'
  2. Thread 'Milipuko ya mabomu Mbagala ni makosa gani ya na kibinadamu na ya kiufundi yalisababisha kutokea kwa ajali hizi'
  3. Thread 'Bungeni: Milipuko ya mabomu Mbagala yatafuna Tsh. Bilioni 17.4'

Nakumbuka wimbo wa diamond na mpoto
 
Ya mbagala nilikua Tosa boys, form 6,tuko domitory tunasikiliza radio hata Dar siijui na sijawah kufika

Ya Goms nilikua mwaka wa kwanza Ifm, niko hostel kigamboni majira ya saa 2 usiku sitakuja kusahau yanaitika kama yako kilometa chache yan wave unaisikia kabisa inavyokata upepo. Nikajiuliza sijui walio karibu inakuaje kama kigambon huku fery mpaka nyumba zinatikisika vivuko vikasimama kufanya kazi.
 
Sikuwepo ila kila nikitazama rejea za hayo matukio mawili kwenye madhara naona picha za unguided rockets na waandishi ndio wanaita jina la kiujumla kuwa ni mabomu. Roketi zenyewe naona nyingi zikizidi sana zitakuwa 220mm au hata ndogo 122mm.

Yawezekana mabomu ndio yalilipukia kambini na kuleta madhara makubwa ambayo hayakuonekana kwa public alafu mizinga ikaruka sehemu mbalimbali. Ila ilikuwa ni milipuko midogo sio missiles zile wala sio rockets kubwa kama 300mm.
 
Itoshe kusema uliyasikia kwa mbali hali ilikuwa hivyo, je watumiaji wakiwa field inakuwaje!! Vita mbaya sana tuendelee kudumisha amani yetu!!
True..hii kitu vita kilinifikirisha sana kipindi kile, sisi yalikuwa ya bahati mbaya. Imagine nchi ambazo hiyo milio ni 24/7!..
 
Tupe maelezo huu ulikuwaje mkuu
Ilikuwa mida ya saa saba kwenda Saa nane mchana nakumbuka tulikuwa darasani kipindi cha Physics mwalimu akiwa mzee mmoja anaitwa Nzohi.

Ghafla tukaanza kusikia vishindo na ngurumo kama radi, hakuna aliyeuliza kuna nini watu wote tulijikuta mlangoni tukigombania kutoka, kufika nje tukakutana na class ya PCB nao wanakuja mbio upande wa class za PCM kuuliza ni nini Hamna mwenye jibu but inaonekana matatizo yapo huko upande wa mbele ya shule.
Basi almost shule nzima ikaelekea upande wa bonden like kama unaenda kisarawe, sasa kuna makombora yakalipuka huko yakaja na kipande cha roof ya huko jeshini, yakaangukia huko pondi (bondeni) kwa waliosoma pugu wanapajua bondeni aka pond au kwa mama P njia ya kwenda kwa mkandawile.

Watu wote tukaanza kurudi mbio tena shulen, kufika nusu ya mlima tunakutana na rundo la wanajesh nao wanakimbia kuja huku bonden pond, aisee ilikuwa ni mshike mshike haswaa! Wananchi, wanajeshi kwa wanafunzi kila mtu na njia yake.

Madhara yalikuwa mengi kwenye mali na vifo!

Hayo Ndo nakumbuka kwa ufupi.
 
Back
Top Bottom