TBT: Unakumbuka nini kuhusu mabomu ya Mbagala (2009) na Gongo la Mboto (2011)?

TBT: Unakumbuka nini kuhusu mabomu ya Mbagala (2009) na Gongo la Mboto (2011)?

Ya mbagala nilikua Tosa boys, form 6,tuko domitory tunasikiliza radio hata Dar siijui na sijawah kufika

Ya Goms nilikua mwaka wa kwanza Ifm, niko hostel kigamboni majira ya saa 2 usiku sitakuja kusahau yanaitika kama yako kilometa chache yan wave unaisikia kabisa inavyokata upepo. Nikajiuliza sijui walio karibu inakuaje kama kigambon huku fery mpaka nyumba zinatikisika vivuko vikasimama kufanya kazi.
Wewe
Ya mbagala nilikua Tosa boys, form 6,tuko domitory tunasikiliza radio hata Dar siijui na sijawah kufika

Ya Goms nilikua mwaka wa kwanza Ifm, niko hostel kigamboni majira ya saa 2 usiku sitakuja kusahau yanaitika kama yako kilometa chache yan wave unaisikia kabisa inavyokata upepo. Nikajiuliza sijui walio karibu inakuaje kama kigambon huku fery mpaka nyumba zinatikisika vivuko vikasimama kufanya kazi.
Wengine tulikua karibu nayo hapo Pugu boys, na shule ilikuwa imefunga ijumaa , watu tukawa tumebaki, nafikiri yalitokea siku ya alhamis kama sikosei.
 
Nakumbuka wimbo wa Diamond na niliukalili wote enzi hizo niko mpitimbwi huko.

Nilikua nikicheka tu nikisikia zile story ati mtu badala ya kubeba mtoto kabeba paka sijui mbwa basi zilikua story za vituko huko skonga, unaangalia taarifa ya habari saa 2 nyumbani kesho yake unaenda kuwapumzikia wenzio na uongo kibao kama una ndgu gomz vile, lakini poleni mliofikwa na hayo maafa.
 
Nakumbuka SUA, leteni hao panya wa kutegua mabomu,, oh mara hv mara vile
 
😂😂 yani ww matukio yote mawili ulikuwemo, unatakiwa kuwa steringi wa hii movie aisee😂😂​
Kwenye haya maisha kuna mengi, lakini muda mwengine tunaogopa kuyaweka wazi kwa kuhofia kufichua Identity zetu. Msome huyu mwanamama Violet Constance Jessop (2 October 1887 – 5 May 1971) ambaye alinusurika kuzama katika meli zote mbili Titanic 1912 na Britannic 1916. Kuna jamaa mwengine alinusurika kufariki zaidi ya mara mbili kwa kupigwa na radi, cha kushangaza hadi alipokufa kaburi lake pia lilipigwa na radi.
 
Kuna bidaboda alijikuta yupo mbezi ya kimara wakati alikuwa gomz,amefikajefikaje gakuna anayejua.yote juu ya yote,kama Hussein Mwinyi aingekuwa mtoto wa mwinyi ilitosha kumuwajibisha
Awajibishwe kwa sababu ipi?
 
Waziri wa Ulinzi hakuhojiwa na Polisi.
Nakumbuka pia Rais Ali Hassan Mwinyi alikuwa anasema," Nchi yetu safi kabisa. Siyo kama jirani zetu. Hapa hatuzalishi wakimbizi. Hapa tunapokea wakimbizi."
Kesho yake yale mabomu yakalipuka na wakimbizi wengi walikwenda Stadium.
Halafu nasikia watoto wengi walipotea.
Af,nakumbuka nilikuwa nimefunga kula chakula for two weeks non-stop .
Niko Mikocheni naisikiliza Ile milipuko inadunda kwenye moyo wangu.
Nikashukuru siko karibu kule.
Halafu ilikuwepo tafrifa kwenye garden ya Ikulu
Nilikuwa na - chat na yule Kamanda wa Jeshi anaitwa Mbowe, alikuwa Jeshini amekamatwa finances za Jeshi.
Nikamuuliza unamfahamu Freeman.
Akasema ni,sijui alisemaje,yule Freeman ni mdogo wangu au kama mtoto wangu.
Basi kesho yake asubuhi,for some reason, Kikwete akamchagua yule kuiongoza tume ya kupelekeza lile tukio.
Ali Hassan Mwinyi hakuwahi kuwa Waziri wa Ulinzi, na wala kipindi chake cha Uwaziri wa Mambo ya Ndani hapakuwahi kutokea milipuko ya Mabomu popote katika ardhi ya Tanzania. Labda ulikuwa umelewa na wewe ni mtu mzima kwa hiyo jina la Ali Hassan Mwinyi kwako liko karibu zaidi kichwani.
 
Awajibishwe kwa sababu ipi?
Huoni kosa hapo?baba yake mzee ruksa aliwahi kuwa waziri wa mambo ya ndani,alijiuzulu baada ya mahabusu kufia lock up huko shinyanga,ulikuwa hujazaliwa,sembuse hili balaa
 
Gomz ndio yalikuw hatari...

Uzuri wa yale madude yalikuwa hayalipuki.. hilo ndio la kumshukuru Mungu sana..

Ubaya wake yalikuw yanaruka juu alafu kabla hayajashuka chini yanatembea kimo cha mbuzi kwa umbali flani.. sasa omba lisikukute ktk site..

Mbaya zaidi ni USIKU... watu wameacha familia zao ndio wanarudi kupumzika nyumbani unapishana na watu ikiwemo watoto wadogo, foleni kubwa.. hujui huko nyumbani watoto au familia yako ipoje.. pia mitandao ya simu ilikatika hivyo mawasiliano yalikuw magumu.

Nakumbuka nilikuwa Home Tabata.. nachek juu naona wekundu na vishindo.. Mzee akasema hapa tusepeni.. tulienda Msasani.. mpk kesho yake asubuh saa 5 tukarudi maana wasiwas mwingine ni nyumba kama tutaikuta au tutakuta kifusi.
 
Duh, Mungu mkubwa mkuu. Poleni sana aisee, binti alikua akiishi wapi kwa siku hizo tatu?​
Serikali iliweka Kambi kama Wajimbizi hapo Sababa kila aliyeokotwa popote au alikosa makazi alipelekwa hapo.
Bint tulimpata akiwa hata hana wasi wasi, yupo kama yupo vile, ana godoro lake, blanket na upande wa kitenge.
Tukambeba godoro tukamuachia ambae hana, blanket tunayo hadi leo tunaitunza kama ukumbusho!
 
Kuna jamaa aliniambia alikimbia toka Gongo la Mboto mpaka Buguruni bila kusimama wala kugeuka nyuma wakati sio mtu wa mazoezi na ana boonge la tambi. Wallah kifo kinatisha.😂😂
 
Back
Top Bottom