TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

Watu wa kale mlipata sana shida!!!! Kwaio pesa ilikua inatumwa kwa bus[emoji23]
Ela zamani ilikuwa inatumwa Posta kwa njia ya EMO inachukua wiki au kwa EMS inachukua siku moja akiingiza muamala asubuhi na mapema jioni au kesho yake unapigiwa simu unakwenda kuchukua mkwanja kama una simu ya mezani au unakwenda posta unakuta kikaratasi cha kuchukulia mkwanja (hii ni mpaka miaka ya 90 mpaka mwanzoni mwa 2000.

Hali ya barabara ilivyoanza kuwa nzuri ndipo baadhi ya makampuni ya Mabasi yakaanza kutoa huduma ya kutuma fedha na vifurushi kwa kuwa mtu akituma leo anapokea siku hiyo hiyo au kesho yake kutokana na bus limefika muda gani, hii tumekwenda nayo mpaka 2010 hivi kwa baadhi ya maeneo maana huduma za kutuma fedha kwa simu zimeanza 2007/2008 na kwa baadhi ya watu walianza kupitia bank transfer mara baada ya mifumo ya kibenki kuboreshwa kwa uanzishwaji wa ATM maana kumbuka mpaka mwaka 2000 bank nyingi zilikuwa zinatumia vitabu, kabla ya hapo information za mteja zilikuwa zinapatikana kwenye kitabu na bank ukitoa wanaandika na kugonga mhuri na ukienda nje ya tawi lako lazima wafanye mawasiliano na tawi lako ndo unahudumiwa

Ila wewe wa juzi juzi mkuu nadhani umepata akili za utambuzi umekuta Tipopesa, Airtel na Mpesa zinapeta
 
Tunyande Dar Mby dereva ni mmakonde mmoja na mwenye Mali Sanga.
Kina Safina walikua wanaisoma namba kwa mbali.
Mnakumbuka enzi zile mabasi ya Mbeya yalikua yanatekwa?
Mabasi ya wakinga yalikua hayatekwi, ukitaka kufika Dar na hela zako panda bus la Mkinga au mhehe.
 
Naunga mkono hili. Hood ni tajiri hata Abood hamfikii. Miaka ya 89-93 nilikuwa nina Coaster nafanya safari Dar - Moro nauli 500, kuna siku wapiga debe Moro wakafanyia fujo basi la Hood Scania yenye engine nyuma ambayo ndio pekee ikifanya safari Dar-Moro. Mzee aliposikia akafungulia majeshi, zile marcopolo mpya zina majina ya wachezaji wa Brazil nauli 300 kwenda Dar.!! Abood aliomba poo!
 
Mada Safi sana hii ,imeniletea good and happy memories, nakumbuka hii bus ya Kiswele route ya Dar to Songea, moto sana Ile Lukumburu pass ni mziki wa break tu ndio unasikika,thanks Scandinavian express, sitowasahau maisha yangu yote, tumeondoka Dar 600am(pale kamata)by 1700 tupo tunduma osbp, saa 20:00 Zambian time tumeondoka pale nakonde 05:00 good morning Lusaka, then ni Inter cape Bus to ....,hii connections huipati tena ,salute kwa Kwacha na Bus yenu Navolonge Swela (hii CD ilikua mziki tosha),mmmmmm I live my life nhe
 
Wakuu kulikua kuna Bus moja inaitwa Comfort, route yake Mbeya to Arusha, kina mwenye historia yake pls, hii CD ilikua Simba wa nyika!,pia Twiga international, Dar to Lilongwe!,nayo ilikua inavuka border pale Kasumulu
 
Brother Scandinavia ilikuwa cha mtoto. Kuna basi lilikuwa linaitwa HOOD likitoka Dar SAA 12 asubuhi SAA 8:30 mchana mpo TUNDUMA lile basi lilikuwa linakimbia wajameni sijawahi ona nchi hii

Sent from my TECNO KC6 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…