TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

TBT ya kibabe: Mabasi na vyombo vya usafiri Tanzania

Hatujaona Torino za Hood zilikuwa na madirisha madogo juu kama mabanda ya njia
Unalikumbuka hili goma?

1660974130876.png
 
Huu uzi mzuri kweli kwa kumbukumbu. Umetukumbusha mbali mkuu, baada ya kupitia uzi kuna visa vimenivutia.
1. Kupata kiini cha kufa kwa kampuni ya Hood
2. Dereva aliyetoka Dar na kufika Mbeya saa 7, hii ni balaa.
3. Ajali iliyokula 70 dah! Bado natamani kupata mwendelezo wake, 70 kwenye bus moja ni kisanga hiki. Halafu kwanini ajali za miaka ya nyuma ziliua sana watu wengi kwa mpigo? Nakumbuka bus jingne sijui (air msae) lilipata ajali kilimanjaro likaua sana wanafunzi.
4. Simon Sirro RPC Tanga [emoji1]
5. Nami niongeze yangu nnayokumbuka ambayo sijayaona huko juu
  • Air Shengena
  • Kizota
  • Fresh ya Shamba
  • Bembea
  • Royal
Bunda Bus, Super Najimunisa.
 
Mimi simu niliyomnunulia Mzee wangu mara baada ya simu kutoka (ilikuwa Siamen ngapi sijui, ile nyeusi yenye kiantena) niliituma kwa Scandinavia kumpelekea mzee daah..
Ilianza Siemens mkonge ikaja Siemens dole gumba.
 
Ela zamani ilikuwa inatumwa Posta kwa njia ya EMO inachukua wiki au kwa EMS inachukua siku moja akiingiza muamala asubuhi na mapema jioni au kesho yake unapigiwa simu unakwenda kuchukua mkwanja kama una simu ya mezani au unakwenda posta unakuta kikaratasi cha kuchukulia mkwanja (hii ni mpaka miaka ya 90 mpaka mwanzoni mwa 2000.
Umenikumbusha mbali sana,,, Kipindi nasoma O level tulikuwa tunatumiwa hela kwa njia ya Posta,,,na Kero ya hii njia ilikuwa ni Ukitumiwa hela basi Majina wanabandika Notice Board na kiasi ulichotumiwa,,, Kama unakuwa na Madeni basi lazima ushikwe Shati....
 
Kwenye hii list linakosekana BUFFALO Dsm-ARU hawa jamaa walikua wanatoka Dar 12 nakufika Arusha saa 6 mchana ilikua siokulimbiza bali ni zaidi ya gari km ya magazeti.
 
Kwenye hii list linakosekana BUFFALO Dsm-ARU hawa jamaa walikua wanatoka Dar 12 nakufika Arusha saa 6 mchana ilikua siokulimbiza bali ni zaidi ya gari km ya magazeti.
Hiyo ilikuwa kawaida sana tu, mabasi mengi Dar Arusha yalikuwa yanageuza siku hiyohiyo
 
IMG-20221031-WA0006.jpg

Safina Investment Bus service Dar Mbeya, Dar Kyela, Dar Tunduma, Mbeya Sumbawanga Long time kitambo
 
Tawaqal
Zainabu
Masiah
M Sleeping Coach
Matema Beach
Scandinavia Express
Kiswele
Executive
Hood ltd
Safina
Embakassy
Lupelo
Sayuni
Hiyo masihDar Tunduma ilikua unatoka dar saa 11 afajiri mnafika tunduma saa 7 mchana unakula chakula kisha unaendelea na biashara
 
Back
Top Bottom