Uchaguzi 2020 TCAA yawajibu CHADEMA, yasikitishwa na upotoshaji wao

Nadhani sasa tupunguze kukimbilia kwenye media na kurusha tuhuma tuu bila kufanya tafiti na kujiridhisha kiini cha maamuzi flani flani..
 
Ni vizuri watuambie pia siku zote ni nani aliyekuwa anaendesha hiyo helikopter???? Kama ni rubani huyohuyo imekuwaje wamzuie sasa???
Umeshaambiwa hiyo kampuni imeomba msamaha ili imtumie huyo rubani na ndio maana mamlaka zikakataa kwa kuwa ni kinyume na sheria.

Lisu hapati zaidi ya 20%ya kura
 
Ukisoma comments kwenye huu uzi Kisha ukienda kusoma na ule wa taarifa ya CHADEMA haki utacheka sana!

Ukitaka kuwajua vizuri chadema soma hizo mada mbili kwa utulivu hakika huta pata shida tena na hawa watu.

Nimejikuta nakumbuka propaganda za hovyo kabisa kuwahi kutokea yani hata Kama mtu ulilewa bado tu utagundua kuwa ni move kabisa.

1 "Tumekuja kukuvunja mguu tuone utafanyaje kampeni" . Jambazi alikuwa anajitambulisha hapo!!!

2: Kuchomwa ofisi za chadema mara mbili mfululizo huku baadhi ya nyaraka muhimu zikiondolewa kwanza.

3: Kutekwa tekwa ovyo kwa wagombea .

3: watu kurusha mawe kwenye msafara wa Lissu huku wakiwa wamevaa nguo za ccm!
 
Huwezi kusema Chadema walificha ukweli bila kujua jibu walilopewa.

Hao wenye helicopter wanajua kuna utaratibu wa kuomba kibali kama pilot ni above 65 YO ndiyo sababu waliomba kibali vinginevyo wasingeomba kibali.

Swali kama hiyo kampuni siku za nyuma ilipewa kibali kumtumia pilot ambaye ni above 65 YO kwanini leo walinyimwa hicho kibali?

 
Taarifa hii siyo credible. Imechanganya hoja ya defense.

Kwanza wanazungumza na kusisitiza kuwa kizuidi kilitokana na umri wa rubani kuwa nje ya bracket ya muda unaoruhusiwa kurusha helicopter.

Lakini paragraph ya pili kutoka mwisho mamlaka inachomeka hoja nyingine, tena kinyemera. Eti wahusuka hawakuwa na/hawakuwasilisha mpango wa safari (flight manifest), kwa hiyo wasingeweza kurusha chopper bila hiyo manifest.

Ukiona kujichanganya huko ujue kuna kitu, ni hujuma!
 
Kamanda jinga jinga sheria inasemaje kuhusu umri?
That "however" will apply when TZ enacts a law to that effect. If our aviation agency has not been given the mandate, it cannot do it for political activities or any other activity.
 
Chadema acheni ubabaishaji, ona rubani mliyetaka kumtumia....Mungu anawaona!
 
Hiyo Helcopta angeomba baba mwenye nyumba alieyumba angepewa fasta sana!

Bacicha muwe mnasoma muache ujuaji mwingi! Ukisoma taarifa inasema wazi hiyo chopa ina kibali kabisa cha hadi mwisho wa kampeni wala hawanashida ya vibali na walisha vipata zamani ! Lakini ni ukweli ulio wazi kuna sheria inayo tuongoza kuhusu umri wa marubani! Rubani aliyetaka kutumika amevuka umri unao ruhusiwa kutumika! Rubani aliyetumika umri wake haukybaliki kabisa kisheria!
 
Umeyaona majibu waliyopewa Chadema kutoka TCAA? Hebu tuwekee hapa kama Chadema wamedanganya basi hatutapindisha.

 
Hizo taasisi hazioni matumizi ya kisukuma kwenye kampeni?

Kisukuma ni lugha. Kama anadhani message yake itafika vizuri akitumia kisukuma kwa nini asitumie. Hakuna sheria inayomkataza.
 
Ni mambo ya ajabu sana. Kwa watu ambao wako serious Dar-Bagamoyo kwa private ni dakika 20 au chini ya hapo walishindwa nini kwenda kuhutubia wanachama wao wanasingizia chopa

Hawa jamaa kampeni zinaelekea kuwashinda
 

Muwe mnasoma kwa makini taarifa iko wazi kuwa kuna kibali cha msamaha lakini huwa kinategemea na mazingira na rubani husika lakini huyu amekataliwa....someni kwa makini
 
Wanatafuta huruma ya wananchi, hawana lolote
 
Tukijua kuheshimu taaluma na kutenganisha siasa na vitu tunavyohitaji ushauri wa kitaalamu tutakua tumestaarabika. Hadi sasa hakuna anayejua wasifu wa huyo pilot huko TCAA ila wengi wetu tunailaumu mamlaka.
Hii ya kupinga kila kitu, ya kulalamikia kila kitu, ya kutaka kila tunachotaka kiwe hivyo hakitufikishi mbali na zaidi tunaonekana watu waajabuajabu

Wenyewe viongozi wa chadema kwenye taarifa yao hawakuweka wazi hiyo sababu maana walijua wangeonekana wajinga ila wafuasi wao sasa ni wajuaji kuliko hata pilot mwenyewe.... 🙄🙄
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…