Uchaguzi 2020 TCRA, hamuwaoni TBC wanavyopiga kampeni wazi siku ya Uchaguzi?

Makumbele

Member
Joined
May 9, 2009
Posts
77
Reaction score
431
Kwa wote mnaoangalia TBC, wana “Mchambuzi wa Masuala ya Siasa” anamwaga sifa kemu kemu kwa Dkt. Magufuli ambaye ni mgombea Urais kupitia CCM.

Mchambuzi wao huyu anaonekana wazi kuwa amekuja kuhamasisha watu kumpigia kura Ndg. Magufuli na mbaya zaidi anamkandia Mzee Mwinyi na kueleza mazuri ya Magufuli.

Mnatuona Watanzania kuwa ni wajinga sana kiwango hiki?
 
Hakuna anayeweza kufanya lolote km wamfanya figiso kwenye internet 'let us cross our fingers and pray before God'
 
Wanapoteza muda, tena wakifanya vituko hivi ndo kwanza wanawatia hasira wananchi wanapiga kura za komoa.
 
Aibu Yao, matokeo yatawahukumu .waanze kutafuta ajira zingine.
 
Muache Kulia lia Magufuli ndiye Rais mpaka 2025
 
Watu tulishafanya maamuzi tangu 2017, mwache abwabwaje hapo!
 
Tulia wewe!

Mwambie lisu na yeye anaweza ku act kwenda kununua nyanya kariakoo tena
Umelewa eti, mtachanyikiwa sana, wizi wenu wote na mbinu zote chafu zinazidi kufichuliwa. Kumbe madaraja hamyaamini tena kama yatawasaidia kwenye uchaguzi huu, tuliwaambia nchi haiendeshwi kama vile ina wizara moja tu ya ujenzi
 
Umelewa eti, mtachanyikiwa sana, wizi wenu wote na mbinu zote chafu zinazidi kufichuliwa. Kumbe madaraja hamyaamini tena kama yatawasaidia kwenye uchaguzi huu, tuliwaambia nchi haiendeshwi kama vile ina wizara moja tu ya ujenzi
Wameendesha nchi km familia ama kampuni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…