Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Kwani shida ipo wapi sasa kama hawatawayumbisha tigo na voda? [emoji848]Maandishi mengi ila ushuzi mtupu. Ndo maana Mwigulu alisema watu kama nyie mhamie Rwanda. Utaratibu wa Starlink ni wa hovyo mno kiasi kwamba nchini Zambia wanaotumia Starlink ni wachache mno. Ofisi zikiwepo Tanzania itasaidia kupata vifaa na huduma zao kirahisi badala ya huu mwanya wa kuwaachia madalali kazi ya kuwaagizia watu. Kosa walilofanya nchi zingine ndo hatutakiwi kulifanya sisi. Nalo ni Starlink kutokuwa na ofisi kwenye nchi husika. Ukitoa speed ya internet hakuna kingine chenye unafuu kwenye starlink. Hata wakipewa vibali leo hii hawataweza kuziyumbisha Vodacom, Tigi na wengine kwenye biashara zao. WANANCHI MASKINI HAMHUSIKI NA STARLINK. HIYO NI KWA AJILI YA WENYE FEDHA ZAO.
Kama ni ya watu wenye pesa shida ipo wapi watu wakitumia pesa zao wanapotaka wao wenyewe?
Kama shida ni upatikanaji wa vifaa kwan hilo ni tatizo la taifa au la wateja? Ni magari mangapi au mashine ngapi tunanunua na vipuli au spear ni za kuagiza hakuna hata wakala hapa tz?
Shida ni ipi hadi kupangiana Maisha na nini cha kutumia?
Why jambo ambalo limeshindikana watu wasitafute suluhu kwa ISP wakubwa kama Star link?
Nadhani hapa kinachoendelea ni tabia zile zile za ukiritimba na uzembe unaofanya taifa liwe slow na kuchelewa kufika maendeleo.
Nina uhakika angekuwa magufuli angeshamtimua Nape na kumpa Elon kibali mchana kweupe.
Kwan lazima ajenge ofisi kwanza si anaweza kuoperate hadi atakapoona ulazima wa kuweka physical offices ataweka kwa muda wake. Why iwe shida?
Acheni mambo yenu bana mnatia hasira sana.