TCRA matapeli wa tuma kwa namba hii dawa yao ni moja tu Ban NIDA iliyosajili hizo namba, pamoja na ku Ban namba zote zilizosajiliwa na hiyo NIDA

TCRA matapeli wa tuma kwa namba hii dawa yao ni moja tu Ban NIDA iliyosajili hizo namba, pamoja na ku Ban namba zote zilizosajiliwa na hiyo NIDA

Kwa kweli wachukue hatua kali, bado hakuna mabadiliko yoyote.

Kila ukiripoti namba za utapeli kwa ile namba yao maalumu (15040) unatumiwa tena ujumbe wa kitapeli kupitia hiyo hiyo namba uliyoiripoti baada ya muda kama wiki mbili hivi.

Kwa nini liwashinde hili? Au wana watu wao wanaofanya huo utapeli?
Itakuwa ni watu wao
 
TCRA ni takataka hakuna kazi wanafanya nilishareport kwao namba zaidi ya tatu,eti wakanishauri mimi ndio niende polisi.Sasa walikuwa wanaweka namba za kuwareport hao matapeli za nini?!.Yamenenepeana tu maofisini kama panya wa stoo.
 
TCRA matapeli wa tuma kwa namba hii dawa yao ni moja Ban NIDA iliyosajili hizo namba, pamoja na ku Ban namba zote zilizosajiliwa na hiyo NIDA

TCRA chukueni ushauri wangu mtateketeza matapeli wote ndani ya miezi mitatu

Swala la utapeli wa meseji za tuma kwenye namba hii ni kama limewazidi akili mpaka sasa hamjafanikiwa kuteketeza hawa wahalifu

Turejelee kuwa namba za hawa matapeli zinakuwa zimesajiliwa na Kitambulisho cha Taifa NIDA kwahiyo mhalifu anaweza kusajili zaidi ya namba moja kwa kutumia hicho kitambulisho jambo ambalo mki Ban namba moja anaweza kuendelea na nyingine zilizobakia

Dawa ya kuteketeza uhalifu huu ni kuwa baada ya kuthibitisha namba hiyo imetuma meseji za kihalifu kwanza kabisa Ban NIDA iliyosajili hiyo namba isiweze kusajili namba nyingine na baada ya hapo Ban namba zote zilizosajiliwa na hiyo NIDA kwasababu mmiliki wa hizo namba nyingine ni huyohuyo mhalifu mwenye hiyo NIDA

Ikiwa kuna mtu atakayeonewa akidai kwamba NIDA yake imesajili namba pasipo yeye kujua afike ofisi zenu kuthibitisha lakini hiyo ni baada ya NIDA pamoja namba zake zote kuwa Blacklisted
Nimeipenda hii
 
Mawakala wa kusajiri line wanachukua vitambulisho vya wateja wao na kusajiri laini zaid ya 4 zen moja wanampa mteja izo zingne 3 wanaenda kuziuza kwa matapeli
Sasa unaposema wafungie Nida wakat huyo mwenye nida ajui km nida yake imetumika kusajiri laini zaid ya 1

Suala ni TCRA pamoja na polisi watengeneze mfumo wa kufatilia namba inayo fanya utapeli endapo namba imefanya utapeli bas unaweza ifuatilia na kujua imetoka eneo gan na ata akizima simu bado iweze ku track
 
Mimi nahofia wengi wasio hatia watateseka kwa uhuni wa wengine.Nadhani labda namna nzuri ingekuwa tcra watengeneze utaratibu ambao utawavutia wanaopata hilo tatizo kutoa ushirikiano,ili wakipata jina na namba ya Mtumaji tcra wafuatilie hilo jina kujua ni nani na limesajili namba ngapi na Wakala aliyesajili,mimi nahisi huenda wanatumia hata namba za marehemu hivyo hata wakizifunga zinapatikana nyingine na Muhusika haathiriki kwa lolote,dawa ni kuwadhibiti Mawakala wa usajili na uwezekano huo upo.
 
TCRA matapeli wa tuma kwa namba hii dawa yao ni moja Ban NIDA iliyosajili hizo namba, pamoja na ku Ban namba zote zilizosajiliwa na hiyo NIDA

TCRA chukueni ushauri wangu mtateketeza matapeli wote ndani ya miezi mitatu

Swala la utapeli wa meseji za tuma kwenye namba hii ni kama limewazidi akili mpaka sasa hamjafanikiwa kuteketeza hawa wahalifu

Turejelee kuwa namba za hawa matapeli zinakuwa zimesajiliwa na Kitambulisho cha Taifa NIDA kwahiyo mhalifu anaweza kusajili zaidi ya namba moja kwa kutumia hicho kitambulisho jambo ambalo mki Ban namba moja anaweza kuendelea na nyingine zilizobakia

Dawa ya kuteketeza uhalifu huu ni kuwa baada ya kuthibitisha namba hiyo imetuma meseji za kihalifu kwanza kabisa Ban NIDA iliyosajili hiyo namba isiweze kusajili namba nyingine na baada ya hapo Ban namba zote zilizosajiliwa na hiyo NIDA kwasababu mmiliki wa hizo namba nyingine ni huyohuyo mhalifu mwenye hiyo NIDA

Ikiwa kuna mtu atakayeonewa akidai kwamba NIDA yake imesajili namba pasipo yeye kujua afike ofisi zenu kuthibitisha lakini hiyo ni baada ya NIDA pamoja namba zake zote kuwa Blacklisted

1. Hili sio suluhisho kwa sababu matapeli wengi hawatumii vitambulisho vyao vya NIDA; Wakipata copy ya mtu ya nida ndio wanaitumia kwa namba zao za kitapeli... Kwa hiyo kufungia hivyo, kuna adhiri na wasio husika

2. Nchi hii ina baadhi ya watu wajinga sana; wanatumia hiyo loop hole kureport namba za watu wasio husika na ndio sababu TCRA wanakuwa waangalifu kabla ya kufunga kila wanacho ambiwa....
 
Mimi nahofia wengi wasio hatua watateseka kea uhuni wa wengine.Nadhani labda namna nzuri ingekuwa tcra watengeneze utaratibu wa ambayo utawavutia wanaopata hili tatizo kutoka ushirikiano,ili wakipata jina na namba la Mtumaji tcra wafuatilie hilo jina kujua limesajili namba ngapi na Wakala aliyesajili,mimi nahisi huenda wanatumia hata namba za marehemu,dawa ni kuwadhibiti Mawakala na uwezekano huo upo.
 
Halafu 0738 huu mtandao una namba nyingi mnoooo za hawa matapel hii ni kumaanisha huu mtandao una mawakala wengi sana wasio waaminifu
 
Wakianza kufungia waongeze na mabenchi tutakuwa wengi sana namba ya nida inatumiwa vbaya na mawakala wao
 
Hili swala ili liishe polic, mitando ya cm na tcra wakae moja, tofauti na hapo selikali inaona ikiwabana watu wa mitandoa itpata hasara
 
Na wahusika wenye hizo NIDA wafunguliwe mashitaka ya matumizi mabaya ya kitambulisho cha NIDA kwa ajili ya kufanya utapeli.

Kama Serikali iliyopo madarakani ya CCM watashindwa kufanya hayo basi tutawaomba WAPINZANI ikitokea wakochukua nchi October 2025 watekeleze mawazo yetu.

GOD BLESS TANGANYIKA
 
Kuna mtindo huwa wanatumia ku reserve fingerprint yako. Unaweka kidole mara ya kwanza wanakuambia haijakubali, watakuambia uweke mara ya pili hata mpaka mara tatu. Ukiona hivyo ujuwe kuna uwezekano taarifa zako akaja kuuziwa mtu mwingine asiyekuwa na NIDA ili asajili laini kwa jina lako.
Hiki ndicho nnachokijua ila sio hicho alichoongea huyo ngumbaru hapo juu
 
Wale jamaa hawana akari,shingo zao zinaumia bure.
 
Mimi na hisi wanatumia Nida za marehemu........., why not fears ??
 
Back
Top Bottom