TCRA waja na kibano kinginge: Wanaorusha matangazo mubashara ya matukio kuomba kibali kwanza kabla ya kwenda hewani

TCRA waja na kibano kinginge: Wanaorusha matangazo mubashara ya matukio kuomba kibali kwanza kabla ya kwenda hewani

Vijana wazee wazazi wa Tanzania mpo wapi.
Hamjionei Huruma wala hamuonei huruma watoto wenu maisha yao ya baadaye.

Litoeni hili Dubwana madarakani.
 
Aibu Yetu, Aibu Yao
Aibu Yao Wenyewe TCRA 😏😶🤨😑😗
 
Mbona sioni, ill-motive kwenye barua/tangazo hili?

Umechagua kutoiona kwa kuangalia pembeni tu, lakini iko mbele yako. Hutaweza kuona matukio kama wananchi wakipiga kura au wakihojiwa na kuelezea jambo WAKATI huo likitokea. Hutaona polisi walipiga watu live.

Kwa kifupi matukio mengi yatakuwa yamepitwa na wakati wake!!! Hata hatua utakazochukua nazo zitakuwa zimepitwa na wakati.

WAKATI!!!
 
Rubbish, acha kutisha watu. CCM ni chama kinachojitambua mno. Hata baada ya miaka 10,still kutakuwa na vyuma vingine vikali kuliko JPM. Watanzania hawawezi wapa saccos uongozi wa nchi hii, take it or leave it.
Sawa. Utaikumbuka hii
 
Sidhani kama watu wameshabashiri nini kitafuata baada ya huu uchaguzi.
 
Sijaona wanaposema kuomba kibali kwanza bali kuifahamisha tume.

Hiyo kuifahamisha TCRA automatically ni kutaka kuweka vitisho. Kuna maagizo ambayo unaona dhahiri yana nia ovu.
 
Sidhani kama watu wameshabashiri nini kitafuata baada ya huu uchaguzi.

Iwapo wapinzani watasimama kidete mgombea halali kutangazwa, mauaji ni lazima. Muda ni mwalimu mzuri.
 
Mkiishafahamishwa ili iweje?
Mbona ukiritimba mwingi namna hii, yaani badala ya kupunguza urasimu sisi tunaongeza ili tu mvitoze faini!!!
 
Haya mambo ndiyo yalivyoanza hata kwa jeshi la polisi hadi ikafika mahala jeshi hilo likajipa mamlaka ya kutoa kibali cha kuruhusu au kutoruhusu mikutano ya vyama vya siasa a.k.a mikusanyiko ya vibali! suala halikuwa vyama halikuwa vyama vya siasa kuomba au kupewa vibali bali ilikuwa ni kutoa taarifa ya mkutano ili polisi wakatoe ulinzi wa mkutano husika, sasa hapohapo ndio upenyo ambao jeshi likajipenyeza na kua mtoa vibali vya mikusanyiko badala ya mlinda mikusanyiko, Kwa hali hii na mwenendo huu wa TCRA naona tuendako kuna giza sababu mambo yote wanayoyazungumzia kwenye hivyo vibali yamo kwenye masharti ya leseni za vyombo hivyo na vina vibali vya jumla vilivyojumisha masharti yoote, kwanini leo wakati wa kampeni za vyama ndipo tuanze kutoa masharti nusunusu??? Au kutaka kuthibiti kile kipindi cha ITV cha DAKIKA 45 ??? Tuelezwe tu ukweli nyuma ya hili lazma kuna ajenda ya mjadala! Wataka wapewe taarifa ya tukio ili wajuwe kama ni Lissu wazuie au ni vipi??
 
Kwaiyo buku tano zile za youtube wameona haziwatoshi?
 
Mimi CCM lakini nakuhakikishia siku za chama tawala madarakani zinahesabika. Trust me hakina zaidi ya miaka 10 unless something dramatic happens.
Mimi nilikuwa ccm damu lakini nikang'amua wanaipeleka Nchi kubaya
Muda wao umekwisha sasa wanalazimisha
 
TCCMRA ni jumuiya yetu ya chama.Inazuia mabeberu wasije kuleta machafuko.
 
Sheria Hiyo haijatungwa Leo ni ya siku nyingi media wanaijua.TCRA wanakumbushia tu.Huo ni wajibu wa media wenyewe sio vyama ya siasa

Media zinazojielewa walishaomba hivyo vibali siku nyingi baada ya kupewa ratiba na wahusika wataka live
Iweke hapa tuione, tafadhali kama ipo ivo unavyosema
 
Back
Top Bottom