TCRA waja na kibano kinginge: Wanaorusha matangazo mubashara ya matukio kuomba kibali kwanza kabla ya kwenda hewani

TCRA waja na kibano kinginge: Wanaorusha matangazo mubashara ya matukio kuomba kibali kwanza kabla ya kwenda hewani

Yawezekana nchi ya 'Malawi ya Kaskazini' kwa sasa ikawa inaongozwa na 'Kiongozi' aliyefuzu Kozi zote Kuu mbili duniani za Ukatili na Unafiki sana.
 
Kwahio mfano limetokea tukio ghafla..., jengo hapo town linawaka moto...., inabidi kwa haraka sana nitume barua pepe kwa TCRA halafu ningoje mrejesho kabla sijaingia mubashara kuwahabarisha watu...., ila kwa bahati mbaya moto ushazimika.....

Haya ni maigizo kama kampuni ina leseni na wataalamu wa tasnia husika, basi ni vema kwa hii Taasisi kuwaachia wenyewe hao wataalamu sababu wanajua nini cha kufanya kulingana na utaalamu wao....
Hapo wamechemka, yaani jengo linawaka Moto mnachukua makamera mnaenda kwenye computer mnaanza kutuma E-mail mnangoja majibu ndo mrushe matangazo!
TCRA muwe mnafikiria kwanza kabla ya kutenda msifikiri dharura wanapata wapinzani tuu hata Wana ccm mnatuudhi.
 
Umeambiwa matukio ya ki calendar sio impromptu!!

Kampeni za uchaguzi mfano ni matukio yenye calendar kabisa ndiyo yanaongelewa au scheduled interview
Wamesema matukio ya dharura unaandika email na wametoa hizo email, hujui kusoma vizuri?
 
Sheria ndivyo inavyotaka
Wanakumbushwa tu wasije jisahau wakafungiwa na kutozwa faini

Hiyo Sheria imetungwa na Watu kwa maslahi yao ,usihalalishe jambo linalo umiza wengine kisa lilitungwa na walio madarakani.
 
Mbona sioni, ill-motive kwenye barua/tangazo hili?

Hawatoruhusiwa kurusha maandamano, au mikutano fulani fulani Live maana ili warushe hiyo lazima wawe waliitaarifu TCRA siku 14 mapema, na hapo watanyimwa ruhusa!

Na obvious inalenga events za wapinzani!.

Next time jifunze kusoma between the lines vitu ambavyo on the surface vinaonekana ni innocent ila behind the scene ni evil
 
Ila watanzania bana

Hii thread imeangaliwa na watu zaidi ya 3.6k kama at least nusu ya hawa wangeamua kuingia mtaani kupinga huu ushenzi, serikali ingekazimika kurekebisha sheria hii, sasa tuko juu ya makochi tukiishia kusema hii Serikali imezidi, haifai, mwisho mwaka huu

ACTION SPEAK LOUDER THAN WORDS
 
Tusipepese ukweli ni kwamba baada ya kufungia vyombo vya habari baada ya kuonyesha habari za upinzani na vingine kufutwa kabisa wameogopa kuonuesha habari za Lissu.

Watu wa tehama wakajipanga kwenye live streaming za mitandao ya kijamii.

Wameona isiwe nongwa kwa sababu waliokuwa wanafatilia kupitia link ni wengi kuliko wanaomwangalia magufuli live kwenye tv kwa sababu Magufuli hana jipya na hana sera mbadala ni yale yale sasa kumdhibiti Lissu ni kuzifungia hata page za watu binafsi kurusha matangazo ya moja kwa moja na sio lengo lingine zaidi ya hilo
 
Aaaah baada ya muda mrefu sasa nishapata picha yote. Lengo kuu la hawa viumbe kumbe ni kuunyima kibali mdahalo wa.Wagombea wa Urais pamoja na mualiko wa Magu ITV iwe sababu ya Magu kutoshiriki mdahalo na mahojiano ya Live.
 
Sheria Hiyo haijatungwa Leo ni ya siku nyingi media wanaijua. TCRA wanakumbushia tu.Huo ni wajibu wa media wenyewe sio vyama ya siasa

Media zinazojielewa walishaomba hivyo vibali siku nyingi baada ya kupewa ratiba na wahusika wataka live
Majibu mengne dag😀😀
 
Lissu anawajambisha hawa wakoloni weusi bila huruma. Antipas pungunza kasi Aisee Hali ya hewa inachafuka kwa mwendo wa mbrrr mbrrr
 
Lissu hatakiwi kuangaliwa kokote kule.
 
Back
Top Bottom