TCRA yatolea ufafanuzi sheria ya umiliki wa laini moja iliyoanza kutumika leo

Hizi sheria huwa zinatungwa kwa kuwalenga zinawalenga watu maalumu ndiyo maana huko mitandaoni kuna watu wanaweka picha za utupu na wanajulikana ila hawakamatwi pamoja na zile sheria zao,wale wezi kwenye mitandao ya simu bado wanaendelea.
 
Kweli akina Sanchi wanapeta tu kule insta
 
Dah tuendelee kusikia yatakayojir kwa watu wa upande wa kushoto
 
Mimi nauliza tu je nani anapoteza kwenye hili, naona kama serikali inapoteza mapato ambayo yalikua yanachangiwa sana na hizo line wanazosema hazina ulazima

Sent using Jamii Forums mobile app
 
piga "Call Centre" number ya mtandao husika watakupa mwongozo.
mimi nilifanya hivo juzi.
 
Nadhani kwa mwenyekiti wa mtaa wako unapoishi
 
Kweli akina Sanchi wanapeta tu kule insta
... Sanchi Instagram tena? Si juzi kati alisilimu huyu na kuachana mambo ya ku-post mipicha kwenye mitandao? Umekosea Mkuu.
 
... Sanchi Instagram tena? Si juzi kati alisilimu huyu na kuachana mambo ya ku-post mipicha kwenye mitandao? Umekosea Mkuu.
Sijamfatilia hivi karibuni.. Kama kaacha basi ni kheri!!
 
Hii sheria siwangeitoa mapema kabla ya usajiri? Au wazime tu, maana kuna line zinadaiwa mikopo baraa🤣🤣🤣🤣
 
piga "Call Centre" number ya mtandao husika watakupa mwongozo.
mimi nilifanya hivo juzi.

Mimi juzi nimekwenda ofisi za Tigo Kibaha, kujaza hiyo fomu. Kwanza hawaijui, na baada ya wenyewe kuulizia makao makuu wakachukua namba yangu ili baadae wanijulishe nini cha kufanya na hadi sasa nasubiri simu yao!!! ;-)
Wanadai wao wana template kwenye system kwa ajili ya mtu anayehitaji kuchukua line ya ziada ila kwa ambao tayari wana lines za ziada hawajui nini cha kufanya!!
 
Kama nimesajili kwa alama za vidole na kwa kitambulisho cha nida shida iko wapi?

Kwani hata kama ninazo tano ili mradi ninazitumia Mimi shida iko wapi?

Kama point ni kuzuia uhalifu si tayari wanajua ni laini yangu hvyo watanitafuta mm niliyesajili.

Tusipangiane matumizi kiasi hichi.
.eti nitolee ufafanuzi wa matumizi.

Haya line Moja ni ya ofisi na line ya pili ni ya familia na jamaa wa karibu, line ya tatu ni kwa ajili ya marafiki na madem zangu mbali mbali line ya NNE ni kwa ajili ya matumizi ya bando tu.
 
Unaweza sajili laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja kwa alama za vidole?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…