Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nikikumbuka simu fake hawa jamaa siwaamini kabsaHawa jamaa wanapuyanga sana, kwahiyo wanataka watupangishe tena foleni?
Duh..nilikuwa sijui, na kampuni za simu zilikuwa nikiruhusu vipi usajili wa aina hiyo wakati wakijua wazi kwamba sheria ilishatungwa na hairuhusu muda wake ukifika? tatizo ni kubwa sana, mitaani mawakala wanasajili mamia ya lines kwa namba zao za nida nadhani hao ndo wanaolengwa.Ndio.
unategemea nn kutoka bunge dhaifu...full of vilazaz!.Wapuuzi sana sasa mbona kwenye sheria yenyewe hawajasema kama unatakiwa laini nyingine utolee ufafanuzi wa matumizi? Wakitaka kutunga visheria vyao vya hovyo wangekusanya maoni kutoka kada mbali mbali sio wanakurupuka kama "TAJIRI WA KIGOMA BROTHER K".
Hivi kabla ya kuandaa hivi vitu kwanini huwa hawashirikishi wananchi kwanza.Nawapongeza TCRA kwa kufata sheria ila nawalaumu sana wasomi wetu wenye PhD bungeni kwa kupitisha hichi kitanzi kwa wananchi.
Nahisi wali download file Google's bila kuedit likawa sheria
... yaani kila mwaka haya majamaa lazima yapigishe watanzania foleni hadi inakera! Ndani ya miaka hii mitano hatujawahi kupumua mifoleni yahusianayo na simu/SIM card!Kwa upande wangu leo ndo nimeona taarifa kwamba Kuna sheria ilitungwa na kupitishwa na Bunge kuwa kuanzia leo haruhusiwi mtu kumiliki laini zaidi ya moja za mtandao mmoja mfano Vodacom.
Taarifa hiyo inaongeza kuwa kama ukitaka kuwa na laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja utapaswa kuitolea maelezo laini ya ziada.
Tunaitaka Serikali itoe maelekezo kwamba ni wapi mtu akitaka kutolea maelezo laini ya ziada atapaswa kwenda ofisi zipi.
Maelekezo haya yanapaswa kulenga Tanzania kwa ujumla na siyo Dar es Salaam pekee.
... pia hayo ndio matokeo ya Bunge la gizani! Wananchi wangeshakuwa aware muda mrefu sana tangu mijadala ikiendelea Bungeni bahati mbaya ndio hivyo tena mambo gizani sijui kwa faida ya nani.Hivi kabla ya kuandaa hivi vitu kwanini huwa hawashirikishi wananchi kwanza.
... kama maelezo yenyewe ni ya kijinga hivyo ya nini kusumbua wananchi? Kuna ambaye atamiliki zaidi ya laini moja bila kuwa na sababu? Wanadhani mwenye kumiliki zaidi ya laini moja kwa nia ovu atatoa maelezo yanayoonesha nia yake ovu? Always, atatoa maelezo mazuri tu....
Mimi nilikua na laini ya Airtel kabla sijaajiriwa Coca-Cola. Au nahitaji laini ya Airtel kwa matumizi yangu binafsi sio ya kampuni.
Kwahiyo watu wote wakapange foleni tcra tena kujaza fomu ?Umeshaambiwa tcra,,,uzuri siku hizi wana matawi kila kona ya nchi
... kwanini hao TCRA waruhusu namba zisizosajiliwa kutumika? Kama zimesajiliwa, kwanini wahusika wanaotuma hizo sms wasikamatwe?Sheria saafi sana, ninafikiri ILE ELA TUMA KWENYE NAMBA HII itaelekea kupungua au kufa kabisa
Dah tunarudi kulekule tulikotoka NIDA watawala wa nchi hii ni watu waajabu sana, na usishangae ukajaza fomu majibu yakarudi 2022 kwamba ombi lako limekubaliwaKwahiyo watu wote wakapange foleni tcra tena kujaza fomu ?
Serikali nzuri inayoshirikisha wananchi kila hatua sio Bora liende... pia hayo ndio matokeo ya Bunge la gizani! Wananchi wangeshakuwa aware muda mrefu sana tangu mijadala ikiendelea Bungeni bahati mbaya ndio hivyo tena mambo gizani sijui kwa faida ya nani.
"Hata hivyo, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kuwa sheria hiyo haimzuii mtu kumiliki laini zaidi ya moja kwa mtandao mmoja, isipokuwa atalazimika kutolea ufafanuzi laini ya ziada".
Hayo maelezo unaenda kuyatolea wapi?Tcra/police/kwny Co. Ya simu husika au?