TCRA yatolea ufafanuzi sheria ya umiliki wa laini moja iliyoanza kutumika leo

Hatari sana na mwaka huu wa uchaguzi TCRA ndo wanaamka wakati bado wana usingizi
 

You know why? Bunge la gizani ndio matokeo yake haya
 

Naheshimu sana wasomi na wataalamu wetu lakini kuna baadhi ya maamuzi yananifanya nitilie mashaka weledi wao.

Kwanza, kuna sababu gani ya msingi mtu kuzuiwa kumiliki line zaidi ya moja iwe tu kwa mtandao mmoja? Kama suala ni kudhibiti watu kuwa na laini nyingi, kwa nini waruhusiwe kumiliki line nyingine za mitandao mingine?
Ikiwa mantiki ni kuwa na line moja kwa matumizi ya kupiga, message na data - basi hawakutakiwa kujali ni mtandao gani. Ama sivyo, basi kuna uwezekano mtu kusajili mtandao A kwa matumizi binafsi, na mtandao B na C kwa uhalifu.

Pamoja na hayo yote, suala la kuzuia uhalifu kwa kukataza watu kusajili line zaidi ya moja HALINA MANTIKI. Zoezi la kusajili, tena kwa kutumia kitambulisho cha taifa, linatosha kabisa kuwa na taarifa sahihi za mtu pasipo kujali amesajili line ngapi.

Kama kuna sheria kali ambayo TCRA walipaswa kuweka ni kukataza mtu kutumia kitambulisho chake kusajili line ambayo haitumii yeye. Hapo wangeweza kuweka namna ya watu kuona vitambulisho vyao vimesajili namba zipi na kuweka jukumu kwa raia kuhakikisha wanatoa ripoti pale wanapobaini kitambulisho chao kimetumika kusajili line zisizo zao.

Pili, idadi ya line 30 kwa kampuni imewekwa kwa kuzingatia nini? Kitu cha msingi sio namba ya line, ni utaratibu wa usajili. Kampuni zinatofautiana sana miundo yao na aina za biashara wanazofanya. Kwa mfano, siku hizi kuna mapinduzi makubwa kwenye sekta ya customer care. Kitengo tu cha customer care kinaweza kuwa na watu zaidi ya 30. Je, serikali inataka kuingingiza urasimu kwenye kusajili kila laini zitazoongezeka? Kwa nini kusiwe zisichukuliwe taarifa za kutosha wakati wa kusajili na suala la udhibiti wakaachiwa kampuni?
Kwa nini adhabu kali ya matumizi mabaya ya line isiwekwe juu ya kampuni iliyosajili ili kuhakikisha wanasimamia waajiriwa wao ipasavyo? Nani alikuja na hiyo 'magic number' 30?

Tatu, ikiwa TCRA wanataka nieleze matumizi yangu ya line - kwa nini wasiweke hilo swali wakati wa usajili? Mtu akiwa anasajili angeweza kuchagua baina ya 'mawasiliano binafsi', 'biashara', 'simu ya nyumbani', 'kifaa cha electroniki' na kadhalika. Kuna ulazima gani ya kuweka urasimu wa kujaza maelezo baadae ikiwa yangeweza kuchukuliwa wakati wa usajili? Je, TCRA wana watu wa kutosha kupitia maelezo yetu sote? - Kutakuwa na mabaraza ya kukubali ama kukataa maelezo?

Matumizi ya line za simu ni muingiliano wa mambo mengi ikiwemo uhuru wa watu kuwasiliana na kuchagua njia ya mawasiliano, biashara ya baina makampuni ya simu na kwa ujumla kutafuta namna ya kurahisisha maisha, biashara na maendeleo. Udhibiti ni jambo jema maana ni kweli kuna watu wanania ya kutumia mitandao vibaya. Lakini njia za udhibiti zisisababishe urasimu usio na sababu, zisilazimishe watu kutumia mitandao wasiochagua na wala zisionyeshe muelekeo wa kuingilia biashara huria za makampuni ya simu.
Kitambulisho cha NIDA ni njia sahihi ya kusajili line za simu. Tena kwa kutumia fingerprint, inakupa uhakika kuwa ni lazima mwenye kitambulisho mwenyewe alikuwepo siku ya usajili. Serikali iangalie mapungufu machache iyafanyie kazi - isianze kutapa tapa na utitiri wa sheria, matakwa na urasimu ikidhani kwamba ndio njia ya kuboresha kumbe inaharibu.
Tuendelee na NIDA inatosha sana, na sio kwenye simu tu na hata mahala pengine pote. Tukianza leo kutapa tapa kama taifa lisilo na mwelekeo, kesho tutaamuru kila mwanachi awe na akaunti moja benki.
 

Hivi kuna vifaa vingine vinavyotumia laini za simu (sim card) zaidi ya simu za mkononi?
Je ni vifaa gani hivyo?
 
Hivi kuna vifaa vingine vinavyotumia laini za simu (sim card) zaidi ya simu za mkononi?
Je ni vifaa gani hivyo?
mi nnazo mashine kibao zipo site, zinatumia sim card, kuwasha/kuzima vifaa kwa sms
not to mention mita smart za maji, zinatumia sim card for internet access
 

Ni makosa kwetu wananchi kutoshirikishwa kwenye utungaji sheria wao wakishakaa utunga Sheria na kutuletea,wasiwe na dhana moja tu ya uhalifu twajua wawasaka wakosoaji mhalifu mwenye nia ya uhalifu hazuiliki kwa kumiliki line moja pekee.
Waweke wazi hayo maelezo ya kutaka kumiliki zaidi ya line moja wanayatolea wapi TCRA,polisi, kampuni za simu
 
Laini zaidi ya moja inaweza kuwa fursa kwa serikali,watwambie tu tutakuwa tunalipia kiasi gani kila mwezi ili waongeze mapato ,Kama laini ziko 500,000 na wao wakaamua kuchukua 1,000@ kila mwezi tayari watakuwa wameteneza mpunga wa kutoka 500,000,000 (Milioni mia tano kila mwezi)
 
Mimi naona mauzauza tu, alama ya vidole imemaliza kilakitu hapo niliwaunga mkono lakini hii ya line 1 kiukweli wamekurupuka inabd wafkrie tena
 
Sasa kama mpeleka sheria ni yule mama Jenista Mhagama mnadhani kuna kitu hapo au utopolo tu? Hili limama litakufa mdomo wazi.
 
Mimi nina laini tatu za voda na zote zinatumika na hiyo milioni tano ya faini sina wakianza kukamata wambieni waanze na mimi maana hata mtaani huku maisha ni tait nikale vya bure
 
mi nnazo mashine kibao zipo site, zinatumia sim card, kuwasha/kuzima vifaa kwa sms
not to mention mita smart za maji, zinatumia sim card for internet access

Tuviorodheshe maana inaelekea wataalamu wa TCRA hawajui uwepo wa vifaa kama hivyo hata kushindwa kuwashauri wabunge wetu wakapitisha sheria hii ambayo inapitwa na wakati kabla haijaanza kutumika.
 
Tuviorodheshe maana inaelekea wataalamu wa TCRA hawajui uwepo wa vifaa kama hivyo hata kushindwa kuwashauri wabunge wetu wakapitisha sheria hii ambayo inapitwa na wakati kabla haijaanza kutumika.
wanajua fika, wametoa mwongozo hapo juu, kama unataka izo zengine ziwe online rasmi, ni kuwaandikia 'barua/ombi'
 
wanajua fika, wametoa mwongozo hapo juu, kama unataka izo zengine ziwe online rasmi, ni kuwaandikia 'barua/ombi'

Je kumiliki simu ya ziada kwa ajili kuwasiliana na nyumbani (makazi) kwangu nayo itahitaji barua/ombi ?
 
Wakati tunaanza usajili hawakututangazi hilo la kutoa ufafanuzi na kwanani, anyway sheria hii ilipitishwa na wabunge wa CCM bila kuhoji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…