TCRA yawafungia Wasafi FM kwa kutumia lugha za matusi

TCRA YAKIFUNGIA KITUO CHA WASAFI FM KWA SIKU 7
-
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imekifungia kutoa huduma za utangazaji Kituo cha Redio cha Wasafi FM kwa muda wa siku saba kuanzia Septemba 12 hadi Septemba 18 mwaka huu
-
Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Mhandisi James Kilaba amesema uamuzi huo umechukuliwa kutokana na kituo hicho kukiuka kanuni namba 11 ya Kanuni za Mawasiliano ya kielektroniki na Posta ya mwaka 2018 katika vipindi vya The Switch na Mashamsham
-
Aidha, Mkurugenzi huyo ametoa rai kwa Vyombo vya Habari kuzingatia kanuni za utangazaji wa maudhui yenye lugha ya staha kwa Watanzania huku akiitaka Wasafi FM kuomba radhi kwa Umma
 
Kama ni hivyo tcra wapo sawa, tena hiyo adhabu ya wiki 1 ni ndogo sana, shwain zao.
 
Wanazuga tu ili ionekane kuna haki....laanaturahi
 
Mwendo wa kabali.
 
Kwa hili TCRA wanastahili pongezi,kumekuwa na lugha za kuudhi zisizo na staha ambazo zinatolewa baadhi ya watangazaji.Napendekeza adhabu iwe kubwa zaidi,swala la maadili lazima kuwa wakali zaidi.
 
IS JAMII FORUMS STILL WHERE WE DARE TO TALK OPENLY???
 
Ila kweli hapa wamezingua, Serious

WCB Mnaleta waongeaji ongeaji tu wasiofuata weledi wa kazi
Mnaambiwa muajiri watangazaji wasomi nyie mnasemaa oooh haina haja

Huyu baba levo kazingua big time, anafikiri studio hapo wanapiga soga kama za vijiweni...kuna maneno yanatakiwa yasiende On Air, wayaongee Off mic
Baba Levo nae anaropokaga ropokaga hovyo tu, siridhishwi na aina yake ya utangazaji hasa ya kuropoka bila kupangilia maneno

Katuponza sisi wasikilizaji wa vipindi vya michezo #SportsArena na #SportsCourt


[emoji35][emoji35][emoji35][emoji35]

Mondi na Dabiliyusibii wajitafakari hiii aina ya watangazaji wanaowaleta.. Sio kila mzungumzaji au anayeongea ongea tu na kwa kuwa ni maarufu basi ana kipaji cha kutangaza...Mambo ya kufosi vipaji tuyaacheni twendeni kwenye Weledi wa kazi...

Uandishi wa habari na utangazaji una ethics zake
 
Kwa hili TCRA wanastahili pongezi,kumekuwa na lugha za kuudhi zisizo na staha ambazo zinatolewa baadhi ya watangazaji.Napendekeza adhabu iwe kubwa zaidi,swala la maadili lazima kuwa wakali zaidi.
Kuna maneno fulanifulani ya Kisukuma ni matusi ya nguoni kwa lugha yetu kwa hiyo Rais wetu mpendwa anapohutubia kilugha tukiwepo au kwenye vyombo vya Habari tunadhalilika sana na kumwona hana maadili. TCRA waangalie hili.
 
Jose tafuta mabilioni na wewe ufungue chako!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…