DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
Hatua hiyo inafuatia ukaguzi na ufuatiliaji uliofanywa na TCRA, ambao umebaini changamoto mbalimbali ikiwemo uwekaji usio salama wa nyaya, nguzo zilizoinama, nyaya zinazoning’inia chini, pamoja na kutokuwepo kwa alama zinazotambulisha wamiliki wa miundombinu hiyo.
Aidha, baadhi ya watoa huduma wamekuwa wakichelewa kuwasilisha ramani kamili za kijiografia za miundombinu yao (GIS maps) na taarifa za hatua walizochukua kurekebisha kasoro zilizoainishwa wakati wa ukaguzi.
TCRA imeelekeza watoa huduma husika kurekebisha kasoro zilizobainika, kuwasilisha ushahidi wa marekebisho kwa njia ya picha na taarifa za utekelezaji, pamoja na kuhakikisha wanapata idhini ya Mamlaka kabla ya kuanza uwekaji mpya wa nyaya za fibre optic.
Vilevile, watoa huduma wametakiwa kuzingatia utaratibu wa kushirikiana katika matumizi ya miundombinu ya mawasiliano ili kupunguza msongamano wa nyaya kwenye nguzo, kuondoa urudufu wa miundombinu na kuongeza ufanisi wa matumizi ya rasilimali zilizopo.
TCRA imeendelea kusisitiza umuhimu wa watoa huduma kutekeleza maelekezo ya udhibiti kwa wakati, kujibu barua za maelekezo na kuwasilisha taarifa za kina kuhusu hatua za marekebisho. Kwa mujibu wa taarifa ya ufuatiliaji ya Agosti 2026, ni watoa huduma wanne tu kati ya tisa walioombwa kuwasilisha taarifa za kina za hatua za marekebisho waliokuwa wamejibu.
Hatua hizi zinalenga kuhakikisha uwekaji wa nyaya za fibre optic unazingatia viwango vya usalama, kulinda watu na mali, na kuboresha mpangilio wa miundombinu ya mawasiliano kwa manufaa ya wananchi na sekta nzima ya mawasiliano.
Pia soma:
~ DC Mpogolo: Nyaya za mawasiliano Kariakoo zimetanda kama buibui
~ Ufungaji holela wa nyaya za intaneti Kariakoo si rafiki kwa mandhari ya Jiji