Fredo Fred,
TA aliyesoma miaka mitatu na mitano si huwa wana scale tofauti ?
Vyuo vya umma (Tanzania) kama chuo kikuu cha Dar es Salaam unalipwa kuanzia viwango vifuatavyo kabla ya makato;
Tutorial Assistant (Mkufunzi Msaidizi)
Shahada ya miaka mitatu - Tshs. 1.6 M
Shahada ya miaka minne - Tshs. 1.7 M
Shahada ya miaka mitano - Tshs. 1.8 M
Assistant Lecturer (Mhadhiri Msaidizi)
Elimu ya umahiri/uzamili (Masters degree) - Tshs. 2.5 M ~ 2.7 M
Lecturer (Mhadhiri)
Elimu ya uzamivu (Doctor of Philosophy, Ph.D) - Tshs. 3.2 M ~ 3.5 M
Senior Lecturer (Mhadhiri Mwandamizi)
Elimu (Ph.D) plus teaching, publications & consultations above 5.0 points academic rating - Tshs. 3.6 M ~ 3.8 M
Associate Professor (Profesa Mshiriki)
Above 7.5 points - Tshs. 4.0 M ~ 4.5 M
Full Professor (Profesa Kamili)
Above 8.5 points - Tshs. 4.5 M ~ 5.0 M
Teaching kila mtu hupewa 2.0 points, Utofauti huja ktk publications na ndipo pana points nyingi sana. Ukiwa na kichwa kizuri kama una-publish ktk international journals unapanda faster. Unaweza kuwa profesa kamili na miaka 31 tu ukiwa mjanja.
Watu pekee wanaolipwa zaidi ya Tshs. 6 M ni Administrative post kama makamu mkuu wa chuo na wale manaibu wake (taaluma, utafiti na utawala) na mwanasheria mkuu wa chuo.
Wengine kama wakuu wa idara na principals/deans huwa inaongezeka kuanzia Tshs. 400,000 ~ 1 M kulingana ngazi uliyokuwepo mpaka ulipopanda. Cheo cha chini ni ukuu wa idara cha juu ni principal/dean.
Mishahara ya chuo kikuu cha Dar es Salaam inafanana sana na ya benki kuu (BoT). From Junior level to principal officer level mpaka managers & directors except for executives (gavana na manaibu wake).