"Sasa hivi wanafunzi lazima waombe wenyewe kwenye vyuo husika kwa gharama zao, hivyo mwanafuzi atalazimika kuomba vyuo zaidi ya kimoja kwa gharama za uombaji za kila chuo na chuo ndicho kinanachochagua wanafunzi wa kusoma kwenye chuo chao na kutuma majina TCU kwa uhakiki."
Tusidanganyane, mwanafunzi aombe chuo anachotaka na akasome huko huko.
Suala la kusema eti elimu za vyuo vikuu vinafanana huo ni uongo mkubwa! Elimu zinatofautiana kabisaa.
Je, kuna mzazi yoyote aliyelalamikia gharama kubwa za kuomba vyuo vingi?
Kila mhitimu ana vigezo vyake vya kuomba chuo, mwingine anataka aishi mkoa fulani kutokana na sababu zake, sasa akipangiwa mkoa mwingine na CAS si ni shida!
Ipo wazi, baada ya kufuta mfumo wa CAS, vyuo fulani vya ujanja ujanja vilianza kukosa wanafunzi, kw sababu wanafunzi walikuwa hawavitaki.
Baadhi ya vyuo vilitumia hila kupata idadi kubwa ya wanafunzi, na kuzima ndoto za wahitimu. CAS inampeleka kwenye kozi na chuo ambavyo hana interest nazo!
Toa elimu bora, matangazo kwa sana, utapata tu wanafunzi, usitegemee CAS ikubebe baada ya kuhonga TCU!