Hio Kampuni ya Media ambayo iko integrated kwa mambo ya tourism, ilibidi niiisimamishe kwa muda kwa sababu vijana waliokuwepo walikuwa waswahili, wavivu, na wasiojituma. Ili kuirudisha tena, nahitaji Vijana Wachapa Kazi sana. Kila mfanyakazi ni lazima ajue English vizuri kwa kunyooka sababu itahusika na International media productions.
Qualities za prospective team member jumla ni 5, namely,
(1)High level of English proficiency.
(2)Ability to commit kwa kazi na safari muda wowote.
(3)Uaminifu sana kwa kazi, rasilimali, na fedha.
(4)Akili ya kujifunza haraka,
(5)Mchapa kazi sana asiyeweka hela mbele.
Tanzania nifanyeje ili kupata vijana kama hao? Naombeni ushauri wana JF.
Studio kali. Majengo. Equipment za kisasa, na Magari (Land cruisers) vipo. Kweli kinachokosekana ni Team Kali. Na pasipo team kali, MAFANIKIO HAKUNA. Wajasiriamali wenzangu mnaelewa hilo. I.e. Your team will make you or break you. In other words, the quality of human resources determines whether the business succeeds or fails.
PS: Ofisi na makao makuu yako Arusha. Ila team itasafiri sehemu mbalimbali Tanzania.
PS: Tangazo official bado. Nimepost ili kupata ideas (brainstorming) za namna ya ku-recruit team members successfully. Kuna aliyeuliza contacts. Muda muafaka ukifika, zitawekwa.
Thanks for sharing with us,
"FAIL BIG, But always make sure that ,You FAIL Forward."Denzel Washington
Kwanza kabisa,Change your mindset,Kwa maana hesabu kuanguka mara ya kwanza ni sehemu ya kujifunza,Na bado kuna chance ya kuendelea kufanikiwa licha ya vikwazo na magumu uliyoyapata.
Kwenye media industry,Vifaa sio kitu,Kama hujajua what NICHE are you In.
Ni vema kuwa na clear VISION ambayo itatoa focus nzuri kupitia mission ulizonazo.Kwa maana lazima uwe tayari kushare na team unayotaka target na core aims ya/za kuanzisha media production yako.
Amini vijana wazuri wapo ,Na wewe unaweza kuwa sehemu ya kuwatengeneza.
Research kama hivi ulivoandika hapa JF ni sehemu ya kuwaandaa vijana hao.
Ajiri mtu au watu wenye uzoefu wa kutosha ambao watakuwa na team chini yao,Itakayowasaidia kuandaa vipindi kwa kadiri ya VISION yenu.
Kunahitajika orientation kwa team utakayokuwa nayo ,ili kujua nini mnapaswa kukifanya,misingi ya kampuni na hata utendaji kazi kwa ujumla.
Usiwe na too much expectation ,Instead give them permission to grow.
Training za mara kwa mara ,Zina nafasi kubwa ya kuinoa na kuiimarisha team unayoitaka.
Pia unaweza kuanza na wachache kama pilot project,Kuona utayari wao kabla ya kuanza kwa kasi kubwa bila kuona efficiency ya team.
Kwa uzoefu zaidi kuhusu masuala ya video and audio production karibu sana PM tujadiliane mkuu.