TEC: Mipasuko kwenye jamii Husababishwa na Watu fulani kujiona bora zaidi na wako juu ya Katiba na sheria

Pale shetani anapoelekeza watu Mungu cha kufanya! Shen.zi sana
 
Hakuna nabii alienda kumkosoa mfalme kipindi cha mfungo .Kipindi cha mfungo walikitumia kwa kuwa mbele za MUngu tu Kuomba yao na kuombea taifa hawakwenda kukosoa.Huo mfungo batili baraza lifute huo waraka umekaa kifarisayo sio wa mfungo wa Kikristo!!
Ishu ya "kipindi cha mfungo" ni yako wewe just to suit your evil interests...

UKWELI na HAKI hauna msimu wa mfungo au wa kulakula chakula...

Unamfahamu Mfalme Sauli? Unamfahamu Nabii Samweli? Unafahamu Sauli kama mtawala alifanya nini na nini kilitokea baada ya hapo?

Alijaribu kufanya kama Magufuli kupitia kwa kamanda wake wa polisi Mambosasa dhidi ya Askofu Emmaus Mwamakula wa kanisa la Moravian...

Sauli alivuka mipaka kiasi cha kuanza kuingilia mambo ya Kiroho ambayo yeye hana mamlaka nayo kuyatenda dhidi ya watu wa Mungu aliokabidhiwa awatawale na kuwaongoza...

Kilichotokea ni kauli moja tu yenye sentensi zisizozidi tatu, ilimmaliza Mfalme na utawala wake ukafikia ukomo...

Tenda haki kwa watu unaowaongoza, nenda zako. Acha kuwakejeli watumishi wa Mungu. Hata kama wanakosea, sio jukumu lako kuwawajibisha. Ni jukumu la aliowaita na kuwapa kazi ya unabii, utume, uchungaji, uunjilisti ama ualimu wa Neno la Mungu...
 
Vyombo vyetu vya habari haviwezi kureport hii
 
Sasa wewe mademu wakristo ndo umewahi funga nini sahivi uko kujisifu uasherati hhhh

Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app
 
Namtafuta anayefunga hata mmoja mwaka huu, mana sija bahatika kumuona, unaweza kunitajia Hoteli na Bar hata tatu zinazofungwa kipindi hiki?

Hao "waliofunga unaowatafuta" una orodha yao na kwa hiyo unawataka wawe wana ripoti kwako uwapime mkojo?

Acha hizo bwana. Wewe mtu unajiandikia mambo kwa jumla jumla wakati uko hapo Yombo Vituka - Temeke ukiwa hujui hata nini kinaendelea ktk kona zingine za dunia na hususani Tanzania...!

Acha hizo we we. Acha kujipalia mkaa kwa kuhukumu watu na wewe ukijihesabia haki. Ni mbaya. Siyo sawa hiyo. Nimekuonya...
 
Wanasiasa ni waumini. Yesu alitumia muda mwingi kufikisha ujumbe wake kwa kuweka wazi uovu wa mafarisayo. Hawa mafarisayo ndio walikuwa wakuu wa utawala wa ndani wa Israel. Tena yeye hakuzunguka zunguka bali aliwasema wazi.

TEC walistahili kumweleza Magufuli kwa uwazi kuwa utawala wake ni wa kibaguzi wa sababu yeye na kikundi chake cha CCM wamejitwalia haki ya kuwa watanzania zaidi kuliko wengine. Lakini ujumbe umefika.
 
Niwatakie kwaresima njema nyinyi nyote
 
Unamsema Nkurunziza yupi yule marehemu au kuna mwingine?.
 
Beating around the bush
 
Tec wameanza kujitambua , kuwakemea Hawa wahuni waliopora uchaguzi kinahitani ujasiri
 
Hakuna nabii alienda kumkosoa mfalme kipindi cha mfungo .Kipindi cha mfungo walikitumia kwa kuwa mbele za MUngu tu Kuomba yao na kuombea taifa hawakwenda kukosoa.Huo mfungo batili baraza lifute huo waraka umekaa kifarisayo sio wa mfungo wa Kikristo!!
Hawa wahuni wakikosolowe unaumia kwa Nini?
 
Acha porojo na mkwara mbuzi, you know and I know hakuna anayefunga
 
Hiv kwa mfano nikibadilisha muda wa kula, yaan badala ya kula mchana nafunga halafu nakula usiku mzima si nakuwa nimefungaeee?!!!!

Na vyakula vinapanda bei na kuadimika masokoni sababu watu wanafukia sana
Sijui mungu wako alivyokuelekeza ufunge, and hoja ni kuwa mna mbwembwe nyingi siku ya kutangaza kwaresma but Sijawah kuona anayefunga chochote kile.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…