TEC ningekubaliana nao kama wangefanya hivi kipindi cha mauaji ya Magomeni mwembechai au mauaji ya Zanzibar,

Mauaji ya October 29 ni ya kinyama, tuache siasa na ujinga. Na ipo siku Samiah yatamrudia.
 
100%
(UNAFIKI WA WAZI WAZI)
Wa mwembe chai siyo watu wala wa zanzibar hawakuwa watu.

Wakati ule, kule Zanzibar kuna waliendekeza ufugaji wa magaidi, hadi walimwua padre wa Kanisa Katoliki. Walimwua padre, halafu ulitaka padre gani aendeshe misa wakati walimwua?
 
Kila Uhai wa Mwanadamu Una thamani, na kila familia iliyo poteza mpendwa inastahili huruma na heshima Matukio ya mwaka 1998 Na 2000 Yakumbukwe pia:

Fuatana Nami Mchambuzi wako Profesa Chotara Mweusi Sultan Bingwa wa Uchambuzi kutoka Viunga vya Sharif Shamba Ilala Dar Es Salam.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limewataka maaskofu, mapadri na waamini wa Kanisa Katoliki nchini kuadhimisha Misa Takatifu maalumu tarehe 29 Oktoba 2026, kwa ajili ya kuwaombea waliokufa, waliojeruhiwa na walioathirika katika matukio yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Huu ni uamuzi unaostahili kutafakariwa kwa upana, si kwa jazba, chuki wala ushabiki wa kisiasa, bali kwa kuzingatia haki, utu wa binadamu na umuhimu wa taifa kuwa na kumbukumbu inayo wajumuisha wote.

Kinacho nifanya nitafakari zaidi ni historia ya matukio mengine ya umwagaji damu yaliyowahi kutokea hapa nchini Tanzania.

👉Mwaka 1998, kulitokea Vifo Mwembe chai, Magomeni, Dar es Salaam.

👉Vilevile, Zanzibar ilipitia matukio ya umwagaji damu yaliyo husishwa na mvutano wa kisiasa na uchaguzi katika kipindi cha mwaka 2000, 2001.

Katika matukio hayo ya zamani, swali linalohitaji kujibiwa ni hili: Je, TEC iliwahi kuandaa misa maalumu ya kitaifa yenye nia inayofanana na hii kwa ajili ya kuwaombea waathirika wa matukio hayo?

Nataja jambo hili kama swali la kihistoria linalohitaji uthibitisho, si kama hitimisho kwamba TEC haikuwahi kufanya maombi yoyote kwa waathirika hao.

Lakini ikiwa kuna tofauti katika namna matukio haya yanavyo kumbukwa na taasisi za kidini, basi ni muhimu kuelewa sababu zake.

Je, tofauti hiyo inatokana na mazingira ya kila tukio, uamuzi wa kichungaji, au kuna mambo mengine yanayo paswa kuelezwa kwa umma?

Kwa sababu, pale taasisi yenye heshima kubwa katika jamii inapochukua hatua ya aina hii kwa tukio fulani, lakini wananchi wanakumbuka matukio mengine yenye maumivu makubwa ambayo hawajayaona yakipewa uzito unao fanana, ni lazima maswali yatazuka.

Na maswali hayo yasichukuliwe moja kwa moja kuwa ni chuki dhidi ya Kanisa Katoliki. Wakati mwingine, ni maswali yanayo tokana na kiu ya kuona haki, usawa na utu vikipewa nafasi bila upendeleo.

Hapa ndipo nina poona tafakuri pana zaidi kuhusu wanaoielekezea TEC vidole kutokana na hatua yake ya kuandaa misa maalumu kwa waathirika wa Oktoba 29, 2025.

Taasisi za dini zina nafasi kubwa katika kujenga maadili, kuponya majeraha ya jamii, kusimamia amani na kusaidia wananchi kuishi kwa kuheshimiana.

Lakini nafasi hiyo huambatana pia na matarajio makubwa ya wana nchi kuhusu usawa, kutobagua waathirika na kutokufanya maumivu ya kundi moja yaonekane kuwa muhimu kuliko ya kundi jingine.

Hata hivyo, ni muhimu kutofautisha mambo mawili👉 kuombea marehemu na kujeruhiwa kwa watu, kwa upande mmoja, na kutafuta ukweli, haki na uwajibikaji kuhusu mazingira yaliyo sababisha vifo na majeraha hayo, kwa upande mwingine.

Misa inaweza kuwa sehemu ya faraja ya kiroho, lakini haiwezi kuchukua nafasi ya uchunguzi wa haki, ukweli kuhusu yaliyo tokea, uwajibikaji wa wahusika na hatua za kuzuia kurudiwa kwa matukio kama hayo.

Vivyo hivyo, kuhoji uamuzi wa TEC hakupaswi kutafsiriwa kama kupinga maombi kwa marehemu.

Mtu anaweza kuheshimu imani ya wengine na wakati huohuo akauliza maswali magumu kuhusu usawa na namna historia ya taifa inavyokumbukwa.

NASAHA ZANGU KWA TEC, VIONGOZI WA DINI, VIONGOZI WA SERIKALI NA WANANCHI.

👉 Kwanza, TEC iendelee kuwa sauti ya maridhiano, haki na utu wa binadamu. Ikiwa kuna maswali kuhusu tofauti ya namna matukio ya kihistoria yanavyo kumbukwa, ni vizuri kuyajibu kwa uwazi na kwa kutegemea kumbukumbu sahihi.

👉 Pili, tusijenge utamaduni wa kuomboleza waathirika kwa misingi ya upande wao wa kisiasa, dini yao, eneo walikotoka au mazingira yaliyosababisha vifo vyao. Kila Uhai wa binadamu Una thamani, na kila familia iliyopoteza mpendwa inastahili huruma na heshima.

👉 Tatu, serikali na taasisi zote zinazohusika zihakikishe Taifa haligaiwiki kwa maslahi ya watu binafsi.

👉 Nne, wananchi tuepuke kutumia misiba kama silaha ya kuchochea chuki za kidini au uhasama wa kisiasa. Kukosoa taasisi ni jambo linalowezekana katika jamii huru, lakini ukosoaji huo unapaswa kujengwa juu ya ushahidi, si uvumi wala tuhuma zisizo thibitishwa.

👉 Tano, taifa letu linahitaji kumbukumbu jumuishi. Tunapaswa kuwa na utaratibu wa kuheshimu waathirika wa matukio makubwa ya kitaifa bila kuchagua ni nani anayestahili kuombolezwa na nani asiyestahili.

TANZANIA INAHITAJI AMANI, LAKINI AMANI INAYOENDELEA PAMOJA NA HAKI, UKWELI NA HESHIMA KWA KILA UHAI WA BINADAMU.

N.b
Moderator acheni
Waliofanya mauaji ya Mwembechai 1988 na yale ya Zanzibar ni kina nani? Wataje ijulikane kama ni kundi tofauti na la wale waliofanya ya Oktoba 2025.

Waliofanya mauaji ya October 2025 wanafahamika na kundi lao linafahamika. Wataendelea kuzungumziwa hadi uwajibikaji ufanyike.

Hizi juhudi za kufanya haya mauaji kama ni mapambano kati ya Zanzibar na Tanganyika na pia kati ya Waislamu na Wakristo ni ujinga na upumbavu wa hali ya juu. Walioamua kuchukulia hivyo bila shaka wana nasaba na wauaji wa pande zote hizo.
 
Kila Uhai wa Mwanadamu Una thamani, na kila familia iliyo poteza mpendwa inastahili huruma na heshima Matukio ya mwaka 1998 Na 2000 Yakumbukwe pia:

Fuatana Nami Mchambuzi wako Profesa Chotara Mweusi Sultan Bingwa wa Uchambuzi kutoka Viunga vya Sharif Shamba Ilala Dar Es Salam.

Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) limewataka maaskofu, mapadri na waamini wa Kanisa Katoliki nchini kuadhimisha Misa Takatifu maalumu tarehe 29 Oktoba 2026, kwa ajili ya kuwaombea waliokufa, waliojeruhiwa na walioathirika katika matukio yaliyotokea wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025.

Huu ni uamuzi unaostahili kutafakariwa kwa upana, si kwa jazba, chuki wala ushabiki wa kisiasa, bali kwa kuzingatia haki, utu wa binadamu na umuhimu wa taifa kuwa na kumbukumbu inayo wajumuisha wote.

Kinacho nifanya nitafakari zaidi ni historia ya matukio mengine ya umwagaji damu yaliyowahi kutokea hapa nchini Tanzania.

👉Mwaka 1998, kulitokea Vifo Mwembe chai, Magomeni, Dar es Salaam.

👉Vilevile, Zanzibar ilipitia matukio ya umwagaji damu yaliyo husishwa na mvutano wa kisiasa na uchaguzi katika kipindi cha mwaka 2000, 2001.

Katika matukio hayo ya zamani, swali linalohitaji kujibiwa ni hili: Je, TEC iliwahi kuandaa misa maalumu ya kitaifa yenye nia inayofanana na hii kwa ajili ya kuwaombea waathirika wa matukio hayo?

Nataja jambo hili kama swali la kihistoria linalohitaji uthibitisho, si kama hitimisho kwamba TEC haikuwahi kufanya maombi yoyote kwa waathirika hao.

Lakini ikiwa kuna tofauti katika namna matukio haya yanavyo kumbukwa na taasisi za kidini, basi ni muhimu kuelewa sababu zake.

Je, tofauti hiyo inatokana na mazingira ya kila tukio, uamuzi wa kichungaji, au kuna mambo mengine yanayo paswa kuelezwa kwa umma?

Kwa sababu, pale taasisi yenye heshima kubwa katika jamii inapochukua hatua ya aina hii kwa tukio fulani, lakini wananchi wanakumbuka matukio mengine yenye maumivu makubwa ambayo hawajayaona yakipewa uzito unao fanana, ni lazima maswali yatazuka.

Na maswali hayo yasichukuliwe moja kwa moja kuwa ni chuki dhidi ya Kanisa Katoliki. Wakati mwingine, ni maswali yanayo tokana na kiu ya kuona haki, usawa na utu vikipewa nafasi bila upendeleo.

Hapa ndipo nina poona tafakuri pana zaidi kuhusu wanaoielekezea TEC vidole kutokana na hatua yake ya kuandaa misa maalumu kwa waathirika wa Oktoba 29, 2025.

Taasisi za dini zina nafasi kubwa katika kujenga maadili, kuponya majeraha ya jamii, kusimamia amani na kusaidia wananchi kuishi kwa kuheshimiana.

Lakini nafasi hiyo huambatana pia na matarajio makubwa ya wana nchi kuhusu usawa, kutobagua waathirika na kutokufanya maumivu ya kundi moja yaonekane kuwa muhimu kuliko ya kundi jingine.

Hata hivyo, ni muhimu kutofautisha mambo mawili👉 kuombea marehemu na kujeruhiwa kwa watu, kwa upande mmoja, na kutafuta ukweli, haki na uwajibikaji kuhusu mazingira yaliyo sababisha vifo na majeraha hayo, kwa upande mwingine.

Misa inaweza kuwa sehemu ya faraja ya kiroho, lakini haiwezi kuchukua nafasi ya uchunguzi wa haki, ukweli kuhusu yaliyo tokea, uwajibikaji wa wahusika na hatua za kuzuia kurudiwa kwa matukio kama hayo.

Vivyo hivyo, kuhoji uamuzi wa TEC hakupaswi kutafsiriwa kama kupinga maombi kwa marehemu.

Mtu anaweza kuheshimu imani ya wengine na wakati huohuo akauliza maswali magumu kuhusu usawa na namna historia ya taifa inavyokumbukwa.

NASAHA ZANGU KWA TEC, VIONGOZI WA DINI, VIONGOZI WA SERIKALI NA WANANCHI.

👉 Kwanza, TEC iendelee kuwa sauti ya maridhiano, haki na utu wa binadamu. Ikiwa kuna maswali kuhusu tofauti ya namna matukio ya kihistoria yanavyo kumbukwa, ni vizuri kuyajibu kwa uwazi na kwa kutegemea kumbukumbu sahihi.

👉 Pili, tusijenge utamaduni wa kuomboleza waathirika kwa misingi ya upande wao wa kisiasa, dini yao, eneo walikotoka au mazingira yaliyosababisha vifo vyao. Kila Uhai wa binadamu Una thamani, na kila familia iliyopoteza mpendwa inastahili huruma na heshima.

👉 Tatu, serikali na taasisi zote zinazohusika zihakikishe Taifa haligaiwiki kwa maslahi ya watu binafsi.

👉 Nne, wananchi tuepuke kutumia misiba kama silaha ya kuchochea chuki za kidini au uhasama wa kisiasa. Kukosoa taasisi ni jambo linalowezekana katika jamii huru, lakini ukosoaji huo unapaswa kujengwa juu ya ushahidi, si uvumi wala tuhuma zisizo thibitishwa.

👉 Tano, taifa letu linahitaji kumbukumbu jumuishi. Tunapaswa kuwa na utaratibu wa kuheshimu waathirika wa matukio makubwa ya kitaifa bila kuchagua ni nani anayestahili kuombolezwa na nani asiyestahili.

TANZANIA INAHITAJI AMANI, LAKINI AMANI INAYOENDELEA PAMOJA NA HAKI, UKWELI NA HESHIMA KWA KILA UHAI WA BINADAMU.

N.b
Moderator acheni
TEC wamekuwa kama Gen Z, wanaenda na upepo wa mambo ulivyo.
 
Sawa usikubaliane nao, sisi wengi tunakubaliana nao.
 
Back
Top Bottom