Teknolojia itumikayo katika usafiri wa anga, imenakili pakubwa kutoka katika viumbe vya asili. Ndegehai ni moja ya sababu kubwa ya ndege kupaa leo.

Teknolojia itumikayo katika usafiri wa anga, imenakili pakubwa kutoka katika viumbe vya asili. Ndegehai ni moja ya sababu kubwa ya ndege kupaa leo.

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Teknolojia itumikayo katika usafiri wa anga, imenakili pakubwa kutoka katika viumbe vya asili.
Ndegehai ni moja ya sababu kubwa ya ndege kupaa leo.
1733721994865.jpg

Ukiacha mbinu za kimuundo na upaaji, sehemu ya tafiti za viumbehai zinaonesha jinsi baadhi ya ndegehai kama Bukini mara kadhaa hugeuza kiwiliwili chake juu chini akiwa angani ili kupunguza kasi na mwinuko kwa haraka (rapid lose of speed and Altitude) kabla ya kutua, au kuepuka ndege wengine wanaowawinda.

Kitendo hicho kinaitwa "Whiffling" ni ujanja unaohusisha kuviringisha juu chini kiwiliwili na mabawa kwa haraka wakati kichwa kikiwa kimenyooka na kutengeneza mburuto (Drag) na kufanya breki kali ya angani (Air Brake).

Ujanja huu kwa mtindo tofauti, pia hutumika kwa ndege isiyo na injini maarufu 'Glider' ambapo rubani huweza kupaa kwa ubavu wa ndege "side slip maneuver" kupunguza mwendo na mwinuko kwa haraka.

Kwa upande wa ndege nyingi za kawaida (hasa kubwa) hutumia ujanja tofauti wa vifaa vya kuua mwendokasi na mnyanyuko maarufu "Speed brake au spoilers" zilizo katika sehemu tofauti kutegemea na aina ya ndege.

"Alpha Mike Tango"
 
Ni kweli kabisa, na siyo kwenye ndege tu bali hata uundwaji wa vyombo vingine ulitokana na kukopi baadhi ya mifumo ya viumbe hai. Kwenye gari kuna mifumo mingi inayoshabihana naya kibinadamu kama respiration na digestion. Gari inatumia fuel, hewa safi na kutoa hewa chafu ili kufanya locomotion kama binadamu. Hata aliyegundua treni huwa nahisi alikopi kutoka kwa jongoo.
 
Vipi kuhusu mtu kupaa angani, hawajagundua namna ya kutengeneza mabawa kwa binadamu kupaa angani kama ndegehai? Mabawa ya kuvaa kama maboya ya kuelea majini
 
Jongoo na tandu
Ni kweli kabisa, na siyo kwenye ndege tu bali hata uundwaji wa vyombo vingine ulitokana na kukopi baadhi ya mifumo ya viumbe hai. Kwenye gari kuna mifumo mingi inayoshabihana naya kibinadamu kama respiration na digestion. Gari inatumia fuel, hewa safi na kutoa hewa chafu ili kufanya locomotion kama binadamu. Hata aliyegundua treni huwa nahisi alikopi kutoka kwa jongoo.
ongoo
 
Back
Top Bottom