Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
Teknolojia itumikayo katika usafiri wa anga, imenakili pakubwa kutoka katika viumbe vya asili.
Ndegehai ni moja ya sababu kubwa ya ndege kupaa leo.
Ukiacha mbinu za kimuundo na upaaji, sehemu ya tafiti za viumbehai zinaonesha jinsi baadhi ya ndegehai kama Bukini mara kadhaa hugeuza kiwiliwili chake juu chini akiwa angani ili kupunguza kasi na mwinuko kwa haraka (rapid lose of speed and Altitude) kabla ya kutua, au kuepuka ndege wengine wanaowawinda.
Kitendo hicho kinaitwa "Whiffling" ni ujanja unaohusisha kuviringisha juu chini kiwiliwili na mabawa kwa haraka wakati kichwa kikiwa kimenyooka na kutengeneza mburuto (Drag) na kufanya breki kali ya angani (Air Brake).
Ujanja huu kwa mtindo tofauti, pia hutumika kwa ndege isiyo na injini maarufu 'Glider' ambapo rubani huweza kupaa kwa ubavu wa ndege "side slip maneuver" kupunguza mwendo na mwinuko kwa haraka.
Kwa upande wa ndege nyingi za kawaida (hasa kubwa) hutumia ujanja tofauti wa vifaa vya kuua mwendokasi na mnyanyuko maarufu "Speed brake au spoilers" zilizo katika sehemu tofauti kutegemea na aina ya ndege.
"Alpha Mike Tango"