#COVID19 Teknolojia ya 5G na Chanzo cha Covid-19: Nadharia Njama (Conspiracy Theory) yenye maswali mengi

#COVID19 Teknolojia ya 5G na Chanzo cha Covid-19: Nadharia Njama (Conspiracy Theory) yenye maswali mengi

Wana subsidy lazima waongoze kwa sababu wanauza bei Chee mbona mnakua wagumu kuelewa

Kwa ubora hawawafikii Nokia au samsung na angalia Nokia na Samsung kwenye granted wamemzid Huawei
Weka Ericsson hapo muondoe Samsung.
 
UOMGO mtupu
kwanza hiyo siyo maana ya 5 Generation kila mtu anaingiza kivyake
5G - Wikipedia
halafu kuingiza Dini ndipo ulipoharibu kabisa
jinsi Generation inavyoendelea ndio tunagundua mengi na magonjwa yaliyopo yataonekana sasa
mwishowe mtatuambia 6G ndio mwisho wa Dunia

Ukwaju hebu fafanua zaidi. Uongo ni upi na ukweli ni upi. Utakua umetusaidia sana wasomaji wako.
 
Sio kweli Huawei ndo anaongoza kwenye 5G huu ni upotoshaji mwingine, Huawei amepewa subsidy na Chinese government matokeo yake anauza vifaa (hardware) za 5 G kwa bei nafuu a.k.a bei ya kutupa

Kinara wa 5G ni Samsung, na Nokia Ila wao gharama zao za hardware ziko juu, ndo maana nchi nyingi Zina prefer Huawei kwa sababu ya unafuu

dennis_robert namba nisaidie kunionesha ni mstari upi uliosoma kwenye maandishi yangu unaosema Huawei wanaongoza kwenye 5G. Nimeutafuta sijauona
 
Sawa, lakini mkuu, hata hii minara ya simu inamadhara makubwa ikiwa unakaa karibu nayo. Sembuse hayo ma 5G?

Lazima yatakuwa na madhara makubwa hata kama madhara hayo hayapelekei mtu kupata Corona.

Sent using Jamii Forums mobile app

mtingi1 uko sahihi. Kwenye uchambuzi wangu nimeeleza hilo kwa uwazi kabisa kwamba kuna uwezekano 5G ikawa na madhara kama teknolojia zilizomtangulia. Ila tunachokosa ni ushahidi wa aina gani ya madhara. Hiyo kusema lazima ina madhara zaidi ya zilizotangulia ndipo tatizo linapoanzia maana hatujui ni kigezo gani kinatumika kupata huo ulazima. Kuna uwezakano mkubwa kabisa teknolojia mpya ikawa salama kuliko iliyotangulia na hili liko kwenye gunduzi nyingi sio za mawasiliano pekee.
 
Ndugu yangu, si weusi tu, wengi wa hawa 5G Conspiracy Theorists ni weupe...

5G Conspiracy Theorists Are Using Fears About The Coronavirus To Make Money

For $350, they’ll sell you a USB stick they claim protects you from harmful 5G radiation and prevents infection from the coronavirus. (It doesn't.)
Uko sahihi. Na walioianzisha hizi nadharia njama sio weusi bali ni weupe. Ila shida kubwa sisi ndio huwa wahanga wa kila kitu maana tunameza na kuminishwa kirahisi sana. Mmoja wa wahubiri wa kingereza aliyeenza hili jambo, yeye alikua anasisitiza kabisa ana interest na Africa maana nadhani ndio ameona anaamika kirahisi
 
Huyo profesa ni clueless kuhusu madhara ya 5G...jiulize kwanini wanaojenga hiyo minara wanavaa HAZMART SUITS...Sars ilitokea baada ya 3G...Homa ya nguruwe H1N1 ikatokea baada ya 4G kuzinduliwa..saiz tuna corona baada ya kuzinduliwa 5G huko wuhan China mwishoni wa mwaka 2019...Spanish flu ilikuja 1918 baada ya madishi makubwa ya radio frequencies yalipozinduliwa duniani kote..toka nakua mpaka Leo nimeishi na imani kuwa minara ya simu ni hatari..inasababisha cancer ..tulifundishwa kukaa mbali na ile minara ili kuepuka mionzi...hii 5G inataka minara mingi.karibu kila baada ya nyumba kumi utakuta mnara wa 5G...Soo nchi ambazo walikua washaanzisha matumizi ya 5G kama China,Italy,Spain ,Iran nk ndio wanaoongoza kwa corona.jiulize kwanini Africa ambapo hatuna 5G Mbona corona haisambai sana...5G ni Kama silaha ya kijeshi....go do your research mkuu..usitegemee serikali zikuambie ukweli wakati wao wanapush kufanya dunia kuwa kama kijiji kwa gharama ya maisha ya watu
 
dennis_robert namba nisaidie kunionesha ni mstari upi uliosoma kwenye maandishi yangu unaosema Huawei wanaongoza kwenye 5G. Nimeutafuta sijauona
Teknolojia ya 5G inahitaji uwekezaji mkubwa wa miundombinu mipya ya mawasiliano kwa sababu inalazimisha kubadilisha ile iliyoko kwa sehemu kubwa. Hadi sasa kuna takribani nchi 35 (nyingi zikiwa tajiri) ambazo tayari zina miundombinu ya 5G na bado inajengwa. Ufungaji wa miundombinu hii kwa nchi nyingi umeanza mwaka 2019.

Nchi zinazoongoza kuwa na miundombinu ya 5G kwenye miji mingi ni South Korea, China, na Marekani. Kwa miaka kama 2 iliyopita, utakua umesikia siasa za 5G kati ya mataifa makubwa hasa Marekani, Uingereza na China. Hii imetokana na ukweli kwamba kampuni ya

Huawei ya China imekua mbele hatua kadhaa kitkiteknologia na kuzifanya nchi nyingi zikiwemo za Magharibi kutumia teknolojia zake

Soma hayo maandishi niliyooigia mstari ambayo wewe umeandika mbele maana yake anaongoza
 
Ndugu dennis_robert , wewe umetafsiri kitu ulivyotaka kisha utumie tafsiri yako kuniita mwongo. Sio sawa.

Sina hakika umetumia methodolojia gani kutafsiri ila kusema iko mbele kiteknolojia maana yake sio sawa na kusema "kuongoza kwenye 5G". Hakuna ubishi Huawei iko mbele kiteknoljia (sio kwa 5G pekee maana 5G ni teknolojia hivyo haimilikiwi na mtu au kampuni moja). Wana teknolojia nyingi zinazotumiwa na nchi nyingi duniani kuanzia kwenye simu hadi mufumo ya usalama wa nchi. Hivyo, kua mbele nilivyoitumia mimi ni tofauti na tafsiri yako.

Pili, nadhani mada kuu ya huu mjadala sio kufananisha nani anaongoza 5G na ndio mana hakuna mahali nimefananisha makampuni. Sababu ya kuitaja Huawei hapo ni kugusia tu mgogoro wa 5G baada ya Marekani kuona Huawei wanawazidi nguvu kwa mitambo yao. Wametumiwa na nchi nyingi za Ulaya kuwafungia teknolojia nyingi ikiwa ni pamoja 5G. Majuzi Uingereza wameipa kazi hiyohiyo pamoja na kupingwa na Marekani na hoja iliyotumika sio ughali wala urahisi wa huduma bali ni uwezo wao. Sasa nakuachia uhukumu mwenyewe iwapo inastahili kuambiwa iko mbele, nyuma au katikati.
 
Kwa nini nchi zenye 5G ndo waathirika wakubwa wa corona

Sent using Jamii Forums mobile app
Sina uhakika na data zako ila kama umetumia zinazotumiwa na wataalamu wa hadharia njama, watakua wamekuingiza chaka maana wanadai kwamba Italy ndio nchi inayoongoza kwa 5g netowork na ndio mana ina wagonjwa wengi.

Ili tuweze kujibu hili swali objectively na sio kinadharia njama, labda tungeweka hapa zata zinazoonesha coverages ya 5G kwa kila nchi na zinazoonesha maambukizi ya Covid-19 halafu tupime.Halafu tusiishie hapo bali tupige hatua mbele tutazame nchi ambazo hazina 5G tulinganishe na data zake za Covid-19 halafu tujiulize zinapataje maambukizi ya Covid-19 wakati hazina 5G networks.
 
Samahani kwa kutokuelewa, lakin waingereza na nchi nyingine wanataka kutumia Huawei kwa sababu iko cheap, na pia watatumia mitambo ya Huawei 5g sio kwenye core parts of their telecoms networks
 
Sina uhakika na data zako ila kama umetumia zinazotumiwa na wataalamu wa hadharia njama, watakua wamekuingiza chaka maana wanadai kwamba Italy ndio nchi inayoongoza kwa 5g netowork na ndio mana ina wagonjwa wengi.

Ili tuweze kujibu hili swali objectively na sio kinadharia njama, labda tungeweka hapa zata zinazoonesha coverages ya 5G kwa kila nchi na zinazoonesha maambukizi ya Covid-19 halafu tupime.Halafu tusiishie hapo bali tupige hatua mbele tutazame nchi ambazo hazina 5G tulinganishe na data zake za Covid-19 halafu tujiulize zinapataje maambukizi ya Covid-19 wakati hazina 5G networks.

Unamaanisha kwamba kama COVID-19 ni 5G related basi aeleze kama je, tukichukua watu 500 wenye ''Corona'' toka Marekani tukawaleta Tanzania (kusiko na 5G) wakasambaa mtaani basi ama watu hao wapone corona au wasiweze kumwambukiza hata mtu mmoja.

Kama akisema hivyo, hapo ndipo atatakiwa kueleza hawa 24 tulionao Tanzania, na wagonjwa wengine barani Afrika wametoka huo kwenye nchi zenye 5G...

Mkuu nakuaelewa sana
 
Manabii wa UONGO, yu mkini haya walio wateule wa Bwana watakengeuka.

Ukienda kanisani ukasikia au ukaona mtumishi anaanza mambo ya NIMEONESHWA, NIMEOTESHWA ogopa na hasa kama ni mambo ya kuogopesha maana hawa wanaooteshwa na kuoneshwa huonyeshwa mambo ya kuogopesha.

Wamelaaniwa maana Bible inasema ULAANIWE MGUU UPELEKAO HABARI MBAYA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom