Englishlady
JF-Expert Member
- Apr 11, 2013
- 2,736
- 3,644
Asante kwa darasa, nimejifunza jambo. sikuwahi kujua kama WIFi ni shidaaa......nilikuwa naweka on tu duuuu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Binafsi sikubaliani na wewe kwa kiwango kikubwa juu ya argument yako hii...
Umeshindwa kuwataja hao unaowaita "manabii wa uongo" kwa majina. Lakini kwa hakika kabisa mmojawapo uliyemlenga ni Bishop Dr Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima...
Huyu ameshajitokeza hadharani na wa wazi na kumzungumzia mdudu - kirusi huyu aitwaye Korona kwa mantiki uliyoeleza hapa...
Katika maelezo ya Mch. Gwajima, sijaona mahali anapokataa kuwa janga la COVID-19 halipo....
Sijaona mahali ambapo Mch. Gwajima anawahimiza wafuasi wakristo wenzake wadharau na wasijikinge na virusi vya Corona....
Wala sijaona ktk maelezo yake yote iwapo Mch. Gwajima anapingana na maendeleo ya teknoljia ya mawasiliano ya 5G yenye nia njema kumwendeleza na kumsaidia binadamu katika utendaji wa shughuli zake za kila siku....
Maudhui ya maelezo ya Mch. Dr Gwajima yamejikita zaidi ktk kuwaelemisha wakristo juu ya ujanja wa binadamu wanaotumikia ulimwengu wa uovu kutumia mambo mazuri (mfano teknolojia ya mawasiliano ya 5G) tunayopewa na Mungu kwa ajili ya manufaa yetu ili kutekeleza ajenda zao ovu...za kuangamiza kizazi cha binadamu....
Lakini watu hawa waovu ambao tunaweza kuwaita mawakala wa shetani - baba wa uovu wanageuza kusudi jema la Mungu na kilipa sura ya ubaya ili tu wao waweze kutekeleza malengo na nia yao ovu dhidi ya uumbaji wa Mungu na kumwangamiza binadamu....
Hii mbinu ndugu zangu kwa sisi watu wa imani tunaelewa kuwa haijaanza ktk majira haya ya mlipuko wa COVID-19 tu.....
Imeanzia tangu enzi zile mara baada ya uumbaji wa Mungu kukamilika. Baada ya hapo Mungu akamuumba mtu (Adamu) ili atawale UUMBAJI huu. Kwa hiyo kusudi la Mungu kutuumba kwa "mfano wake" lilikuwa ni kumiliki na kutawala uumbaji wake kwa niaba yake.....
Wakati huohuo alikuwepo malaika aliyeasi enzi yake huko mbinguni na Mungu hakuwa na option nyingine isipokuwa kumwadhibu kwa kumtupa chini akiwa amenyang'anywa kila kitu kwa maana ya mamlaka ya umiliki na utawala wa uumbaji wa Mungu. Huyu ndiye shetani kwa tafsiri ya "mdanganyifu".....
Mamlaka ya umiliki na utawala ya uumbaji wa Mungu yakakabidhiwa kwetu binadamu....
Huyu muasi (Shetani) vita yake na Mungu inaendelea hadi leo na binadamu ndiye uwanja wa vita hii...
Ndiyo maana Mara baada ya Adamu na Hawa kukabidhiwa mamlaka ya utawala wa uumbaji wa Mungu pale Eden, shetani akiwa katika sura ya nyoka na kwa udanganyifu wa hali ya juu kwa kumtumia Hawa (Eva) mke wa Adam alifanikiwa kuupotosha UKWELI wa Mungu kuwa UONGO naye akauamini UONGO badala ya UKWELI .....
KWA mara ya kwanza binadamu akaasi maagizo ya muumba wake. Akawa chini ya utawala wa Shetani wa KIFO na MAUTI hadi miaka zaidi ya 2000 iliyopita alipokuja Yesu Kristo - Mungu mwenyewe ktk umbo la binadamu kuturejeshea tena mamlaka na utawala wetu binadamu dhidi ya uumbaji wa Mungu tulionyang'anywa na shetani pale Eden...
Hata hivyo vita hii si kwamba imeisha, bado inaendelea na walio upande wa Yesu Kristo wanaishinda kwa ukamilifu wake....
Hira na mbinu za shetani kuupumbaza ulimwengu (watu wa dunia) ni za hali ya juu sana kwa kutumia haya haya tunayoita maendeleo ya kisayansi na teknoljia....
Mungu wetu mwaminifu anatutia moyo kwa kutuambia
".....hamtakosa kuzitambua hila na fikra (mbinu na mikakati) zake (shetani)....."
Angalia historia ya matukio ya Kibiblia utagundua kuwa binadamu siku zote ni mgumu kuamini maelezo na maagizo rahisi kabisa ya wokovu wake toka kwa Mungu dhidi ya majanga mbalimbali yanayomnyemelea kumwangamiza ...
Mara zote binadamu huyu huyu hung'ang'ana na maarifa na akili zake kutaka kujiokoa na mwisho wake huangamia kabisa....
Hata nyakati za gharika, watumishi WA KWELI wa Mungu i.e Nuhu alipata changamoto hii hii alipokuwa anawaambia watu kujiandaa na wokovu kwa sababu dunia ilikuwa inakwenda kuangamizwa/kufutiliwa mbali kwa maji...
Nuhu alidharauliwa, alioonekana kama nabii tapeli aliyewataka watu kuchangia sadaka za ujenzi wa Safina ili ajipatie fedha tu....
Alionekana ni mtu asiyeweza kuthibitisha unabii/maelezo yake aliyoyapokea toka kwa Mungu kwa misingi ya sayansi ama maarifa ya kibinadamu.....
NB: Hata hivyo nakubaliana na wewe kwa kitu kimoja kuwa, ni kweli kabisa wapo manabii wa uongo ambao hutumia fursa kama hizi kupotosha watu
Lakini Mungu yuko kazini, akiwatumia watu (watumishi) wake waaminifu kuokoa watu wake kutoka katika hila za uangamivu za shetani
Mimi naaamini. Kwa Mungu ni KUAMINI TU. Hatutumii maarifa na akili na ujuzi wetu binafsi kujiokoa isipokuwa kwa NEEMA YAKE KRISTO...!!
Tusiwajumuishe wote kwa namna hii. Tupambane na tatizo tu. Tatizo sio kuoneshwa au kuoteshwa (mambo haya yako kiimani), tatizo ni matumizi ya mabaya ya dhana ya kuoteshwa au kuoneshwa huko.Manabii wa UONGO, yu mkini haya walio wateule wa Bwana watakengeuka.
Ukienda kanisani ukasikia au ukaona mtumishi anaanza mambo ya NIMEONESHWA, NIMEOTESHWA ogopa na hasa kama ni mambo ya kuogopesha maana hawa wanaooteshwa na kuoneshwa huonyeshwa mambo ya kuogopesha.
Wamelaaniwa maana Bible inasema ULAANIWE MGUU UPELEKAO HABARI MBAYA.
Sent using Jamii Forums mobile app
Umewasha taa kila mtu anaweza kuona.Mlipuko wa Covid-19 unasambaa ukiambatana na taarifa nyingi zisizo sahihi au za kupotosha. Taarifa hizi zinatengenezwa, ama kwa watu kukosa uelewa sahihi wa jambo wanalolizungumzia au kwa makusudi, kama “Nadharia Njama” (
Ha ha ha haaaa well notedUmegusa maeneo mengi sana precisely. Kuna baadhi ya watumishi wa mungu ukiwasikiliza unajisikia aibu mwenyewe. Angalizo: sijakosea kuandika mungu badala ya Mungu.
Sent from my iPhone using JamiiForums
Ooopsss!!! Du !!! Sasa sijui tatizo ni Mimi ndio sjaelewa au?UOMGO mtupu
kwanza hiyo siyo maana ya 5 Generation kila mtu anaingiza kivyake
5G - Wikipedia
halafu kuingiza Dini ndipo ulipoharibu kabisa
jinsi Generation inavyoendelea ndio tunagundua mengi na magonjwa yaliyopo yataonekana sasa
mwishowe mtatuambia 6G ndio mwisho wa Dunia
Umeshindwa kuwataja hao unaowaita "manabii wa uongo" kwa majina. Lakini kwa hakika kabisa mmojawapo uliyemlenga ni Bishop Dr Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima...
Hivi mpaka sasa huyo shekhe hamjampeleka milembe mnasubiri nini?Ni kweli kabisa afrika tupo katika mkwamo mzito sana, tunaishi dunia ya copy and paste halafu wakati mwingine tunajifanya kujua kuliko wajuaji halisi.
Kuna Shekhe mmoja jirani yangu, yeye anasema COVID 19 ni matokeo ya dhambi za wakristo ndio kisa cha Italia na nchi za kikristo kuwa na vifo vingi, lakini akili ya kawaida tu ni kwamba MECCA mwaka huu hakuna waliokwenda kuhiji.
Israel imezifunga zile sehemu takatifu ambazo ni sehemu muhimu kwao katika kuingiza fedha za utalii, hili ni janga zito, halipaswi kuunganishwa na imani za kidini, kule Ujerumani wanakufa wapagani wengine tu.
Kuna nchi hazimwamini Mungu wa Biblia na Quran na hazina idadi kubwa ya wagonjwa wa Corona.
Ndugu John E. Luyangi, ninadhani ndugu Kitaturu ni member wa kwa Bishop (kutokana na maelezo yake). Kwa kuwa sikua nimesikiliza alichokirejea toka kwa Bishop, nimelazimika nitafute hiyo clip ili nielewe kwa nini Kitaturu alinivaa. Nimetamani ningekua nimemsikiliza kabla ya kuandika uchambuzi huu maana nadhani kuna points ningekua nimeziongeza au kuzipanua zaidi.Kitaturu
Umeiona clip ya pili ya Gwajima kuhusu Corona, Bill Gates na chanjo yenye chip? Mtizamo wako kwa muktadha wa hii mada ni upi?
Mathew Togolani Mndeme
Asante sana. kwa ruhusa yako, naomba nitumie bandiko mabandiko yako namba 1 na 57 kama rejea. Naamini kupitia kwa maandishi yako, kuna jamii itasaidika hata kwenye mapambano dhidi ya Corona.