Binafsi sikubaliani na wewe kwa kiwango kikubwa juu ya argument yako hii...
Umeshindwa kuwataja hao unaowaita "manabii wa uongo" kwa majina. Lakini kwa hakika kabisa mmojawapo uliyemlenga ni Bishop Dr Josephat Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima...
Huyu ameshajitokeza hadharani na wa wazi na kumzungumzia mdudu - kirusi huyu aitwaye Korona kwa mantiki uliyoeleza hapa...
Katika maelezo ya Mch. Gwajima, sijaona mahali anapokataa kuwa janga la COVID-19 halipo....
Sijaona mahali ambapo Mch. Gwajima anawahimiza wafuasi wakristo wenzake wadharau na wasijikinge na virusi vya Corona....
Wala sijaona ktk maelezo yake yote iwapo Mch. Gwajima anapingana na maendeleo ya teknoljia ya mawasiliano ya 5G yenye nia njema kumwendeleza na kumsaidia binadamu katika utendaji wa shughuli zake za kila siku....
Maudhui ya maelezo ya Mch. Dr Gwajima yamejikita zaidi ktk kuwaelemisha wakristo juu ya ujanja wa binadamu wanaotumikia ulimwengu wa uovu kutumia mambo mazuri (mfano teknolojia ya mawasiliano ya 5G) tunayopewa na Mungu kwa ajili ya manufaa yetu ili kutekeleza ajenda zao ovu...za kuangamiza kizazi cha binadamu....
Lakini watu hawa waovu ambao tunaweza kuwaita mawakala wa shetani - baba wa uovu wanageuza kusudi jema la Mungu na kilipa sura ya ubaya ili tu wao waweze kutekeleza malengo na nia yao ovu dhidi ya uumbaji wa Mungu na kumwangamiza binadamu....
Hii mbinu ndugu zangu kwa sisi watu wa imani tunaelewa kuwa haijaanza ktk majira haya ya mlipuko wa COVID-19 tu.....
Imeanzia tangu enzi zile mara baada ya uumbaji wa Mungu kukamilika. Baada ya hapo Mungu akamuumba mtu (Adamu) ili atawale UUMBAJI huu. Kwa hiyo kusudi la Mungu kutuumba kwa "mfano wake" lilikuwa ni kumiliki na kutawala uumbaji wake kwa niaba yake.....
Wakati huohuo alikuwepo malaika aliyeasi enzi yake huko mbinguni na Mungu hakuwa na option nyingine isipokuwa kumwadhibu kwa kumtupa chini akiwa amenyang'anywa kila kitu kwa maana ya mamlaka ya umiliki na utawala wa uumbaji wa Mungu. Huyu ndiye shetani kwa tafsiri ya "mdanganyifu".....
Mamlaka ya umiliki na utawala ya uumbaji wa Mungu yakakabidhiwa kwetu binadamu....
Huyu muasi (Shetani) vita yake na Mungu inaendelea hadi leo na binadamu ndiye uwanja wa vita hii...
Ndiyo maana Mara baada ya Adamu na Hawa kukabidhiwa mamlaka ya utawala wa uumbaji wa Mungu pale Eden, shetani akiwa katika sura ya nyoka na kwa udanganyifu wa hali ya juu kwa kumtumia Hawa (Eva) mke wa Adam alifanikiwa kuupotosha UKWELI wa Mungu kuwa UONGO naye akauamini UONGO badala ya UKWELI .....
KWA mara ya kwanza binadamu akaasi maagizo ya muumba wake. Akawa chini ya utawala wa Shetani wa KIFO na MAUTI hadi miaka zaidi ya 2000 iliyopita alipokuja Yesu Kristo - Mungu mwenyewe ktk umbo la binadamu kuturejeshea tena mamlaka na utawala wetu binadamu dhidi ya uumbaji wa Mungu tulionyang'anywa na shetani pale Eden...
Hata hivyo vita hii si kwamba imeisha, bado inaendelea na walio upande wa Yesu Kristo wanaishinda kwa ukamilifu wake....
Hira na mbinu za shetani kuupumbaza ulimwengu (watu wa dunia) ni za hali ya juu sana kwa kutumia haya haya tunayoita maendeleo ya kisayansi na teknoljia....
Mungu wetu mwaminifu anatutia moyo kwa kutuambia
".....hamtakosa kuzitambua hila na fikra (mbinu na mikakati) zake (shetani)....."
Angalia historia ya matukio ya Kibiblia utagundua kuwa binadamu siku zote ni mgumu kuamini maelezo na maagizo rahisi kabisa ya wokovu wake toka kwa Mungu dhidi ya majanga mbalimbali yanayomnyemelea kumwangamiza ...
Mara zote binadamu huyu huyu hung'ang'ana na maarifa na akili zake kutaka kujiokoa na mwisho wake huangamia kabisa....
Hata nyakati za gharika, watumishi WA KWELI wa Mungu i.e Nuhu alipata changamoto hii hii alipokuwa anawaambia watu kujiandaa na wokovu kwa sababu dunia ilikuwa inakwenda kuangamizwa/kufutiliwa mbali kwa maji...
Nuhu alidharauliwa, alioonekana kama nabii tapeli aliyewataka watu kuchangia sadaka za ujenzi wa Safina ili ajipatie fedha tu....
Alionekana ni mtu asiyeweza kuthibitisha unabii/maelezo yake aliyoyapokea toka kwa Mungu kwa misingi ya sayansi ama maarifa ya kibinadamu.....
NB: Hata hivyo nakubaliana na wewe kwa kitu kimoja kuwa, ni kweli kabisa wapo manabii wa uongo ambao hutumia fursa kama hizi kupotosha watu
Lakini Mungu yuko kazini, akiwatumia watu (watumishi) wake waaminifu kuokoa watu wake kutoka katika hila za uangamivu za shetani
Mimi naaamini. Kwa Mungu ni KUAMINI TU. Hatutumii maarifa na akili na ujuzi wetu binafsi kujiokoa isipokuwa kwa NEEMA YAKE KRISTO...!!
Mpendwa
Kitaturu, kwa kuwa umeongea kwa uzito sana na kumtaja mtu/mtumishi kwenye maelezo yako, naomba nikujibu ili kuweka rekodi sawa na tusipotoshe mada.
Moja, nashukuru sana kwa mawazo yako na kutupa summary ya kazi ya ukombozi. Kwa bahati nzuri kwangu, huwa najitahidi sana kutojadili watu kwenye umma (public) kama sio lazima kufanya hivyo. Naweza kujadili hoja zao bila hata kurejea majina yao lakini sio kuwajadili wao. Ndio mana unaona sijataja jina la mtu hata mmoja katika uchambuzi wangu.
Pili, ni bahati mbaya sana kwamba umesoma nilichoandika ukiwa na mtu wako kichwani na umetafsiri kila nilichoandika kwa kumlenga yeye. Kama unafuatilia yanayoendelea duniani, utafahamu kwamba nadharia njama ya 5G imeongelewa na watu wengi sana na miongoni mwao wako "watumishi wenye majina" kama nilivyosema. Hivyo, ninahofia sitajibu chochote kinachomlenga yeye moja kwa moja au mwingine kama wewe ulivyofanya. Ninamfahamu na ninamweshimu.
Tatu, sina hakika kama kuna mahali nimetumia neno "manabii wa uongo" katika uchambuzi wangu. Kama pako ni makosa. Ni bahati mbaya kwamba wewe umeyachukulia maneno kama manabii, wainjilisti na wahubiri katika muktadha wa kikristo pekee . Maneno haya yana maana pana. Mtu anaweza akawa mwinjilisti au muhubiri wa kilimo, wa viwanda, wa teknolojia, nk. Pia mtu yoyote anaweza kuwa nabii wa pombe, sigara, uongo, uovu, 5G, nk. Popote nilipotumia neno manabii au wahubiri katika uchambuzi wangu sijayatumia katika muktadha wa kikristo bali katika upana wake nikimaanisha
manabii/wahubiri/wainjilisti wa nadharia njama ya 5G. Nilipolenga imani nimetumia neno "watumishi".
Nne, uko sahihi sana kuhusu njama za wanadamu katika kuasi kusudi la Mungu. Ila sina hakika kama Mungu tunayemuamini, anahitaji sisi kutumia habari za kupikapika, kuungaunga au za uongo na za kutisha watu ili kuonesha kwamba kuna mbinu na njama ovu duniani. Yeye ni mkweli na anakaa katika kweli. Haitaji kusaidiwa na uongo au uzushi au mambo ya kubuni kutusaidia kuijua kweli yake.
Tano, nimesikitika sana kusoma hoja yako kwamba wanaomwamini Mungu hawahitaji kutumia akili, maarifa wala ujuzi binafsi bali wanatakiwa kuamini tu. Hii ni hatari kubwa sana na inaelezea kwa nini imani inatumika sana kupotosha watu. Ninatamani jukwaa hili lingekua la kiimani tujadili huu mtazamo kibiblia kwa reference (maana ndiyo uliyoirejea kwenye maelezo yako). Ninataka kukuhakikishia kwamba Biblia inapingana wewe sana kwenye fikra hizi. Kama hatuhitaji akili, maarifa, elimu, sayansi, na ujuzi biinafsi kama nyenzo za kutusaidia kumjua Mungu zaidi, sasa alitupa vya kazi gani na kutumia wapi? Kwa nini anataka tutafute elimu na maarifa?
Naomba nikomee hapa na nikuombe sana tujadili mada bila kujadili majina ya watu au watumishi kama mimi nilivyofanya. Kama kuna mtumishi ameongea kitu na kinaangukia kwenye mada niliyoandika, basi tujikite tu kwenye hiyo hoja bila kumtaja na kama kuna maswali yanayomhusu yatajijibu. Usichukue comments za watu wengine wanaotaja watu kuwa ndio mtizamo wangu.
MM Togolani