#COVID19 Teknolojia ya 5G na Chanzo cha Covid-19: Nadharia Njama (Conspiracy Theory) yenye maswali mengi

Mathew Togolani Mndeme ninayemfahamu, yeye mwenyewe na dini ni pipa na mfuniko, muda wowote anakuchapa injili. Hapa kaandika akiwa anaijua dini vilivyo. Niishie tu kwa kusema, Ahsante kwa kutoa elimu hii.
 
Sasa mkuu unapinga bila kuthibitisha bila shaka uongo wa YASEMWAYO utafiti wowote unaanzia kwenye doubts hapa ndiyo tunaanza ku-develop hypothesis, kwasasa wacha tuendelee kufuatilia hizi tuhuma na tuzichukulie kama ukweli otherwise watoa huduma/wavumbuzi wafafanue kinyume chake. Cha ajabu wao wavumbuzi wako kimya why wasijitokeze kufafanua ukweli hasa ni upi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Ndugu bigmind,

Kitu ambacho huenda wewe na wengine wengi walioaminishwa nadharia njama ya 5G na Covid-19 hamukijui, ni ukweli kwamba mjadala wa madhara ya 5G haujaanza leo wala jana. Imekua ikijaribiwa kwa miaka kadhaa sasa na ndio mana nchi ziliozoanza kuweka miundombinu zimeanza mwaka jana . Kama zilivyo teknolojia mpya au gunduzi zozote zile, zinakabiliana na scrutiny kali ya watafiti/wanasayansi kabla au hata baada ya kuanza kutumika. Watafiti wameshaonesha hofu zao siku nyingi kuhusu 5G na wametoa plausible arguments za kwa nini wanadhani kuna 5G inatakiwa kuchukuliwa kwa tahadhari. Watafiti wengi wameshauri serikali zao zisikimbilie kukumbatia teknolojia hii hadi itakapothibitishwa ni salama kwa matumizi. Hawa wamefanya hivyo kwa tafiti za kisayansi na wanaonesha ushahidi wa preliminary results huku wakipendekeza tafiti zaidi kufanyika. Pia hoja zao zimejibiwa na hao unaosema wako kimya. Hizi hizi tahadhari za kizushi kwamba miili inatengeneza virusi.

Sasa hii ni tofauti sana na wanachokifanya waliokuja na nadharia njama ya 5G. Nadharia hii imeanzishwa na daktari mmoja wa Ubelgiji January mwaka huu. Aliandika makala kwenye gazeti bila ushahidi wowote akisema anahisi huenda Covid-19 ina inasababishwa na 5G network (wakati huo mlipuko ulikua bado uko China tu). Makala hiyo ilifutwa na gazeti hilo masaa machache baada ya kuoenaka ni baseless. Ila tayari ilikua imeshasomwa na watu kadhaa na ndipo uvumi ukaanza kusambaa kama moto wa mabua na kudakwa na opportunists wa nadharia njama. Kinachosikitisha, ni watumishi kulishwa tango pori na kulimeza kama lilivyo bila kulichunguza.

Itakua ni ajabu sana iwapo mtu atadai hiki kinachoongelewa na wahubiri wa 5G ni plausible hypothesis inayohitaji attention maana mengi wanayoongea wala sio scientific arguments. Ni uongo wa kutunga na hadithi za kuungaunga. Hii sio approach tunayoitumia ku-develop hypothesis. Ni sawa na mtu aibuke leo aanze kusema joto la dunia limeongezeka kwa sababu tumeweka international space station inazunguka dunia huku akiwa hana hoja yoyote inayosaidia claim yake. Kama kila uongo ukichukuliwa kuwa ni hypothesis basi kazi ya sayansi itakua ngumu sana na ya kujichosha. Hivi kweli wewe unahitaji ushahidi au akili gani kujua kwamba DR Congo hawajaanza kuwapa watu vaccine? Kw ahiyo uongo kama huu tuuite ni hypothesis? Unahitaji akili gani kuona uongo unaodai kwamba watu wanaingiziwa chip ya radio frequency kwa kupitia chanjo ya kinga?

Nimesema kwenye uchambuzi wangu kwamba ni sahihi kuhoji, kuweka mashaka, kuuliza maswali na kubisha au kupinga lakini fanya hivyo kwa evidence na kutumia taarifa sahihi sio za uongo na za kujengea watu hofu. Mimi kama mkristo, nninona aibu kubwa sana kuona watumishi wanasimama madhahubi wanatumia muda mwingi kuongelea 5G kwa hoja za kizushi, uongo na zisizo na scintific evidence yoyote. Ni kazi ya wanaovumisha kuhusu 5G watuambie hiyo sayansi ya mwili kuzalisha virusi wanaoambukizwa imefanyika wapi na lini.

MM Togolani
 
TCRA ni taka taka.

Wako wapi wanamuachia Gwajima anapotosha umma.
Hadi youtube wanafuta mavideo
Clip ya wazushi
 
Hawa wanaojiita manabii sishangai kutumia njia hii kupiga hela za watu, wao ni scammers kama scammer wengine, cha kusikitisha ni kuona watu wazima wengine na elimu zao wamesoma hadi PhD alafu wanaamini upuuzi kama huu unakuta wanapiga magoti kabisa wanalia wanasali mungu asilete 5G. Nyooooko. PhD tupa kule stupid
 
Jiulize kwa nini.
Wakati wa uzinduzi wa 3G kulitokea tetemeko kubwa lililoua watu 20,000.
Michael Jackson alifariki na Satellites za Marekani na Urusi ziligongana pia wakati 4G inazinduliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na wewe ni mwongo hujui kinacho endelea
 
Mimi sio muumini wa hii conspiracy theory, na ninaichukia sana. Lakini, hoja ulizojenga ku-refute madai yao nyingi (kama sio zote) hazina mashiko.
 
Funny thing is half of these tinfoil hat wearing idiots have a microwave oven at home and don't mind exposing their food to large amounts of radiation from a microwave oven which let's out more radiation than 5G tech
 
Umechambua na kutoa elimu vizuri kasoro ulipodanganya neno Nadharia njama umelitohoa mwenyewe wakati lipo muda mrefu tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndugu Yoda, unadhani nidanganye ili iweje kwa mfano? Nifaidikaje?

Kwenye ujumbe wangu nimekiri sijawahi kujua wala kusikia maana ya conspiracy theory kwa kiswahili.

Nadhani badala ya kusema nimedanganya, ungenijulisha tu kwamba hilo neno lipo hivyo nimebahatisha na kupatia.

MM Togolani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jiulize kwa nini.
Wakati wa uzinduzi wa 3G kulitokea tetemeko kubwa lililoua watu 20,000.
Michael Jackson alifariki na Satellites za Marekani na Urusi ziligongana pia wakati 4G inazinduliwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
@Yoda, hizi ndio nadharia njama zenyewe. Zinatafuta kila namna ya kujenga hoja za ajabu kwa lengo la luwaletea watu hofu. Nikuukize maswali.

Moja,nini kinatofuaitisha siky 3G (kama kweli ilikuwepo) ilippzinduliwa na siku zingine za mwaka?

Mbili, kwani kabla ya siku ya kuzindua 3G hakukuwahi kuwa na matetemeko na watu wakafa?

Tatu, hawakuwahi kufa watu maarufu kama Mike Jackson kabla ya hiyo siku?

Nne, Satelite kugongana (kama ni kweli) kunamaanisha nini kwenye nadhania yako?

MM Togilani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Very clever...

Publicity stunt and argument diversion... Yes, Electromagnetic waves cannot 'create' semi-live streams ie viruses... But the critical argument is -- is 5G thoroughly safe? IT IS NOT... And 'Corvid19' the moniker for common virus 'Corona'... What about the 'rapid tests' across the world do they 'detect' the virus or symptoms of the cumulus of possible viral infections of which common flu could be one of them?

There are many red flags in the purported 'pandemic'? And why does it instigate the rally for the global possible mandatory vaccine? Anyone who thinks governments and Mainstream media are to be trusted at this juncture is compromised when it comes to common sense... The global population is surely being played out...

There is a time, what goes around and comes around outta the conspiracy theories community could hold grains of truth far better than typical social complacency and believing men of 'position of power' and 'experts' who are doing nothing but exerting status quo -- most of them playing the game of 'monkey see monkey do' -- of careful manipulation of events and narration of the story. And these days, it is well known -- how does it follow when you say to public 'research has found...', 'scientists say...', 'Prof Who of Ivy School says...', 'The Government Official has said...' Well, Governments can be manipulated by the corporate world... People are likely to believe whatever is presented in such fashion.

Why should You or I believe blindly just because the government says or BBC or CNN? We have got to be a progressively discerning society... Our Global Leadership is compromised in many accounts... And this is never--- the first time...

Re:


Now, listen to the true 'experts'... Scientist, Innovator and Inventor of email:


Man from the Industry...


Public hearing in the city of Sacramento, CA.


Senate hearing...


Okay, let it sink in.

About the 'virus' issue -- What do prominent and independent scientists (virologists) have to say?


Now, how many here think or have a feeling that there could be 'deep state' affairs mingling with global economies?

Somebody in this thread has hinted it right -- there are so many things going on below the surface of what we are made to hear, see and have to talk about...

People, enlighten yourselves!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…