Teknolojia ya Digitali ya Startimes na Ting: Kero za watumiaji

Hawa jamaa ni wahuni sana. Hata mimi wamenikera sana kwa kweli sijui niwafanyeje? Hata hivyo nauza kidecorder chao bei 2,000/= ( elfu mbili maongezi yapo) ila cable siuzi.

Mwenye uzoefu na EASY TV anijuze, je naweza tumia decorder ile ile?

Ama kama mtu anajua jinsi ya kuchakachua yaani nitumie bila kulipa kulipia maumivu waliyokwishanipa anijuze
 
TCRA wako bike kulipana mahela ya mgao unadhani yanawaingia sna hayo? Ulisikia ripoti ya kamati ya bunge? Kaitafute
 

DSTV Mwisho wa yote
 
Hapo ndio wana ku allert ujiunge na DSTV mpango mzimaaaaaaa!!!!
 
Sikumbuki hii ni thread ya ngapi ikielezea uhuni wa star times. kinachoshangaza ni kwa nini watu wanaendelea kununua ving'amuzi vyao licha ya haya yote? Tumerogwa?
 

Sababu yao kubwa ilikuwa ni ipi hasa kibiashara? Hwakupenda wateja wao wafurahie AFCON?
 

Wadau,

Nimesikitishwa sana na Startimes kwa nini walikata channel ya KBC wakati wa fainali ya Kombe la Mataifa huru ya Africa, eti kwa kisingizio kuwa hawana kibali, je ilikuwaje wakaonyesha mechi za mwanzo isipokuwa nusu fainali ???, Je sisi kama wateja wa Startimes haki yetu iko wapi? Je hamuoni huu ni wizi? Nawasilisha:spy:
 
Hii kampuni imeanza wizi mapema sana.....chanel nying sana hazionekani moja kwa moja(temporally),kama vile bado wanafanya testing.

TCRA inabidi mfanye close monitoring.
 
TCRA+TBC+STARTIMES Unapata wizi mtupu. KBC UBC wameonyesha. Why not TBC?
 
mmh

sioni mantiki ya kulalamika hapa, coz huu ni wakati wa utandawazi na watu wapo kwasababu ya biashara tuu, ni kweli kwa maelezo tuliyopata startimes ni kuwa hawana kibali cha kuonyesha AFRICON kupitia KBC, but ni UBC tu so walifanya, hivyo kimakasa na kwamaelezo yao walipata barua ya malalamiko toka KBC wakati wa robo fainali

lakini kwa upande mwingine nadhani ni swala la marketing tu/biashara kwani nadhani walitaka wengi walipie kifurushi cha sh 18000 badala ya sh 9000.

lakini unaweza pia kuangalia DSTV nao walitufanyia mchezo huo huo kwani wao waliikata kabisa KBC na wakaacha chanel iliyokuwa katika kifurushi cha gharama za juu.

teh teh pole sana mnapenda za dezo
 
Nyie ng'ang'anieni tu hapo star time mpaka mkohoe damu! Hawana ishu! Ma channel mengi ni ya bure ktk dish la kawaida tu! Wao wanalipisha, movie ndo hakuna kitu, poleni.
 
Dawa pekee ni kutupa hivyo ving'amuzi vyao wakose wateja then warudi kwao China. Kwanini uendelee kuteseka kwa hela yako bwana? Kuna EASY TV, ZUKU na DsTV.
 
Huyu aliyeleta hii maada ana nia ya kuwatia hila tu Star Times, wote tumeona mpira kupitia Star Times kuanzia mechi ya kwanza hadi fainali. Sasa ni Star Times gani anayoisema?, kuhusu KBC wametoa tangazo karibu siku nzima kusema kuwa kutokana na haki ya kurusha matangazo KBC inabidi ifungwe wakati wa mechi na kuwashauri watazamaji wao waangalie kupitia UBC ambapo sote ndio tumeangalia hizi mechi.
Jamani mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni, au labda kuna ajenda ya zaidi maana haiwezi kupita wiki kabla haya jamaa hawatuhumiwa bora kuhamia kwingine pale unapoona huridhishwi kuliko malalamiko yasikwisha. Waacheni nao wapumue jamani!!!!!!!.
 
yaani sisemi kitu naweza bomoa hii pc ya offisi mchaga akaniwea ndani bure
 
Mie najuta ni kwann nilingia mkenge kununua hiki kidubwana!wizi mtupu jana wamenitia hasara ya kulipia elfu 18 ili tu nione fainal jaman inaniuma mpaka mda huu!
 
Acheni kulalama na kulalamika hivi bado mnahangaika na hao star times cjui dstv mara zuku huku easy tv??

Hapa JF kila kitu kinapatikana sie wengine ni watu wa kutest tu kwenye jukwaa la tech kuna kila njia ya kuchakachua na kujipatia channel zionyeshwazo na dstv bureee kabisaa.
Mii wengi nawa shangaa sana njia mbadala huwekwa humu humu badala ya kuzijalibu watu wanazibeza.

KAMA UNAONA UNAIBIWA NA WEWE IBA ILI MUWE NGOMA DROO.
mim toka mwaka 2010 nakula ubua tu nafaidi machanel kibao free.
Upande wa umeme ndiyo usiseme dawa ya jeuri kusudi.

Mwenzio akikomba mboga usilalamike wewe komba zaidi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…