Edward Chapa
Member
- Jun 30, 2012
- 72
- 12
Jamani mimi ni mteja wa StarTimes ambaye nimejiunga na kifurushi cha UHURU ambacho tunaambiwa kuwa kinaonesha jumla ya vipindi (Chanels) 47, lakini ukifiatilia ni kama chanel 42 tu zinazoonekana! Kwanini chanel kama KBC, UBC na nyinginezo zilizooneshwa katika kipeperushi hazionekani?
Nawasilisha kwa wahusika tu.
mimi nilikinunua kipindi cha kombe la dunia, baada ya hapo nikakifungia sandukuni. now nakula kitu cha Easy TV: ITV, Channel 10, Star TV, UBC, Citizen, TBCCM zote ndani.
DStv...so much more..
mimi nilikinunua kipindi cha kombe la dunia, baada ya hapo nikakifungia sandukuni. now nakula kitu cha Easy TV: ITV, Channel 10, Star TV, UBC, Citizen, TBCCM zote ndani.
Kama TBC wamo ndani, basi.Chezeiya mchina wewe washawaweka tbc mfukoni hata mfanye nini tcra wamelala......
mimi nilikinunua
kipindi cha kombe la dunia, baada ya hapo nikakifungia sandukuni. now
nakula kitu cha Easy TV: ITV, Channel 10, Star TV, UBC, Citizen, TBCCM
zote ndani.
WanaJF mambo vp?
Nina maswali machache kidogo yananitatiza kutokana na hii teknolojia ya hivi vingamuzi.
Hivi Dstv wao wanatumia teknolojia gani ya digtali au analogia? Kama wanatumia digitali kwa nini hawa startimes na ting na wao wasitumie njia hiyo ili mtu yeyote aliye ndani ya nchi hii apokee mifumo yao kwa njia ya satellite, badala ya mifumo yao hiyo ya kutumia transmita na ndio maana mtakubaliana nami kuna baadhi ya maeneo ya hapa dar picha zao zinakatikakatika. Kwani hizo transimita zao zinarusha mawimbi kwa umbali gani?
Tuingie kwenye teknolojia fulani inayoendana na jiografia ya nchi yetu. Nionavyo mimi wangejipanga wawe wanarusha matangazo yao kupitia kwenye satellite kwa mfano nyuzi 68 mashariki ambapo kama utakuwa unataka MY TV, au STARTIMES au TING utumie dish hilo moja kwa kuchagua mojawapo kati ya hizi sio kuleta teknolojia inayosambaa kwa kufuata miji mikubwa kwani waishio kwenye wilaya wao hawastahili?
Jamani hivyo ndivyo nionavyo mimi wewe unasemaje?