Tlaatlaah
JF-Expert Member
- May 18, 2023
- 24,665
- 25,388
Hayakuandaliwa chini ya mwamvuli wa upinzani kama ilivyozoeleka. Hayana kinara wala kiongozi moja muwajibikaji...
Organization na mobilization ya vijana waandamanaji imefanyika na kuchochewa kupitia mitandao ya kijamii tu..
Imepelekea ugumu kwa polisi kubabaika, kwasababu haikuwa rahisi kubaini kinara wa maandamano ili kudeal nae, na pengine kumkamata na kumtia nguvuni...
Madhumuni ya maandamano hayo, ni kupinga musuada wa Sheria ya fedha kwa mwaka 2024/2025, uliowasilishwa bungeni na waziri wa fedha kwa majadiliano na hatimae kupitishwa kua sheria nchini humo..
Maandamano hayo yaliyopewa jina la "Kuchukua Bunge" yameratibiwa na kuhamasihwa kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo TikTok, X, Facebook, IG, Whatsapp n.k, na vijana wa kizazi kipya, waliojibatiza jina la Gen Zs, huku walengwa zaidi ni vijanaa wale waliozaliwa mwishoni mwa miaka ya 1990, na mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambao wengi wao wako mtaani wakisota na athari za ukosefu wa ajira, na ugumu wa maisha baada ya kuhitimu masomo, huku wakibangaiza chochote kitu kwa hastle ngumu za hapa na pale ili mradi mkono uende kinywani...
Hekaheka za maandamano hayo yaliyosambaa kwa kasi sana mabarabarani, maeneo mbalimbali nchini Kenya, yanalenga kuilazimisha na kuishinikiza serikali ya William Samoe Arap Kipchichiri Ruto, kupitia bunge la Kenya, kubadili mara moja baadhi vifungu na mapendekezo ya kodi, tozo na ushuru, ambayo vijana wengi wanahisi yatasababisha maumivu na ugumu wa maisha yao zaidi, badala ya kuleta ahueni na nafuu ya maisha...
Ni maandamano ya aina yake kutokea nchini kenya. unaweza kusema ni ya kisasa na ya kisayansi sana katika siasa za vyama vingi...
Ni ya kipekee na kitofauti sana, ukilinganisha na yale yaliyokua yakiandaliwa, kuratibiwa, kufadhiliwa na kuchochewa na upinzani Kenya, ambayo kwa kiasi kikubwa yalikua na sura ya kikabila, ukilinganisha na haya yanayoendelea hivi sasa...
Mpaka sasa miongoni mwa mafanikio ya maandamano hayo ambayo upinzani nchini Kenya ulijitenga nayo, ni pamoja na kuondolewa kwa ushuru wa mafuta ya kupikia, huduma za pesa kwa simu, magari n.k
Vijana hususan Kenya, wamebaini kwamba upinzani, hashtags mitandaoni, mihemko, ghadhabu na kutukana viongozi waandamizi Serikali hapawasaidii chochote bali panawachelewesha, na zaid sana panazidisha ugumu wa maisha, na pengine kuwadidimiza nia na ndoto zao za maisha...
Hata hivyo upinzani nchini Kenya kumesalia kimya, na kusisitiza msimamo wao wa awali kwamba, musuada huo wote ni adhabu kwa mkenya na unapaswa kutupiliwa mbali wote kama ulivyo na sio kurekebisha basdhi ya vifungu...
Je kwa hali hii,
Vijana wamepoteza imani na upinzani kama jukwaa na mtetezi wa shida, unyonge na changamoto zao, na sasa wameamua kujiorganise na kujimobilise wenyewe kupitia teknologia ya mawasiliano na mitandao ya kijamii na kujitetea wenyewe dhidi ya uchokozi, udhalimu au uonevu wa mamlaka katika nchi zao kuanzia Kenya?
Na nini hatma ya upinzani sasa kisiasa, Africa Mashariki, maana vijana wamechukua mkondo wao kupambania mahitaji yao wenyewe kisasa 🐒