Teknolojia ya habari, mawasiliano na mitandao ya kijamii ilivyo fanikisha maandamano na mageuzi katika mapendekezo ya kodi, tozo na ushuru Kenya

Teknolojia ya habari, mawasiliano na mitandao ya kijamii ilivyo fanikisha maandamano na mageuzi katika mapendekezo ya kodi, tozo na ushuru Kenya

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Hayakuandaliwa chini ya mwamvuli wa upinzani kama ilivyozoeleka. Hayana kinara wala kiongozi moja muwajibikaji...

Organization na mobilization ya vijana waandamanaji imefanyika na kuchochewa kupitia mitandao ya kijamii tu..

Imepelekea ugumu kwa polisi kubabaika, kwasababu haikuwa rahisi kubaini kinara wa maandamano ili kudeal nae, na pengine kumkamata na kumtia nguvuni...

Madhumuni ya maandamano hayo, ni kupinga musuada wa Sheria ya fedha kwa mwaka 2024/2025, uliowasilishwa bungeni na waziri wa fedha kwa majadiliano na hatimae kupitishwa kua sheria nchini humo..

Maandamano hayo yaliyopewa jina la "Kuchukua Bunge" yameratibiwa na kuhamasihwa kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo TikTok, X, Facebook, IG, Whatsapp n.k, na vijana wa kizazi kipya, waliojibatiza jina la Gen Zs, huku walengwa zaidi ni vijanaa wale waliozaliwa mwishoni mwa miaka ya 1990, na mwanzoni mwa miaka ya 2000, ambao wengi wao wako mtaani wakisota na athari za ukosefu wa ajira, na ugumu wa maisha baada ya kuhitimu masomo, huku wakibangaiza chochote kitu kwa hastle ngumu za hapa na pale ili mradi mkono uende kinywani...

Hekaheka za maandamano hayo yaliyosambaa kwa kasi sana mabarabarani, maeneo mbalimbali nchini Kenya, yanalenga kuilazimisha na kuishinikiza serikali ya William Samoe Arap Kipchichiri Ruto, kupitia bunge la Kenya, kubadili mara moja baadhi vifungu na mapendekezo ya kodi, tozo na ushuru, ambayo vijana wengi wanahisi yatasababisha maumivu na ugumu wa maisha yao zaidi, badala ya kuleta ahueni na nafuu ya maisha...

Ni maandamano ya aina yake kutokea nchini kenya. unaweza kusema ni ya kisasa na ya kisayansi sana katika siasa za vyama vingi...

Ni ya kipekee na kitofauti sana, ukilinganisha na yale yaliyokua yakiandaliwa, kuratibiwa, kufadhiliwa na kuchochewa na upinzani Kenya, ambayo kwa kiasi kikubwa yalikua na sura ya kikabila, ukilinganisha na haya yanayoendelea hivi sasa...

Mpaka sasa miongoni mwa mafanikio ya maandamano hayo ambayo upinzani nchini Kenya ulijitenga nayo, ni pamoja na kuondolewa kwa ushuru wa mafuta ya kupikia, huduma za pesa kwa simu, magari n.k

Vijana hususan Kenya, wamebaini kwamba upinzani, hashtags mitandaoni, mihemko, ghadhabu na kutukana viongozi waandamizi Serikali hapawasaidii chochote bali panawachelewesha, na zaid sana panazidisha ugumu wa maisha, na pengine kuwadidimiza nia na ndoto zao za maisha...

Hata hivyo upinzani nchini Kenya kumesalia kimya, na kusisitiza msimamo wao wa awali kwamba, musuada huo wote ni adhabu kwa mkenya na unapaswa kutupiliwa mbali wote kama ulivyo na sio kurekebisha basdhi ya vifungu...

Je kwa hali hii,
Vijana wamepoteza imani na upinzani kama jukwaa na mtetezi wa shida, unyonge na changamoto zao, na sasa wameamua kujiorganise na kujimobilise wenyewe kupitia teknologia ya mawasiliano na mitandao ya kijamii na kujitetea wenyewe dhidi ya uchokozi, udhalimu au uonevu wa mamlaka katika nchi zao kuanzia Kenya?

Na nini hatma ya upinzani sasa kisiasa, Africa Mashariki, maana vijana wamechukua mkondo wao kupambania mahitaji yao wenyewe kisasa 🐒
 
Odinga kapoa, anaangazia AU apate shavu kule, vinginevyo angeyateka maandamano hayo kisiasa na yeye kuwa ndiye kinara wake. Hapa tz vijana wengi wameamua kuwa machawa hawana muda wa kuandamana kupinga miswada na tozo umiza. Ikitokea tz vijana wasio na ajira yaani ma hustlers wakaandamana wapinzani watayateka ili kujipatia sifa waungwe mkono kwenye siasa zao dhidi ya chama tawala na serikali yake
 
Mkuu vuta subira mambo mazuri hayataki haraka, na kila jambo na wakati wake

ipo siku bwege atajitambua na kuwa mjanja
mpaka waje wagundue kwamba mihemko, ghadhabu na matusi kwa viongozi hayasaidii, muda utakua umeenda sana 🐒
 
Odinga kapoa, anaangazia AU apate shavu kule, vinginevyo angeyateka maandamano hayo kisiasa na yeye kuwa ndiye kinara wake. Hapa tz vijana wengi wameamua kuwa machawa hawana muda wa kuandamana kupinga miswada na tozo umiza. Ikitokea tz vijana wasio na ajira yaani ma hustlers wakaandamana wapinzani watayateka ili kujipatia sifa waungwe mkono kwenye siasa zao dhidi ya chama tawala na serikali yake
sina hakika angeanzia wap,

kwa sababu tayari wabunge wa upande wake na msimamo wa chama chake cha AZIMIO LA UMOJA-ONE KENYA COALITION PARTY kilishachukua mrengo wa kupinga msuada wote wa fedha 2024/2025 kwa kuuita ni "adhabu" kwa mkenya, unadhani vijana hawakuliona hilo?

lakini pia,
maandamano yanayoratibiwa na kuandaliwa na upinzani ikiwa Raila ndie kinara hufanyika katika misingi ya kikabila na katika maeneo mengine hawashiriki kabisa wakiskia kinara wa maandamano ni Raila, wanamchukia sana 🐒

na kwa maoni yangu,
ikiwa Raila angejitokeza kama kinara wa maandamano yale, basi hamasa ingepungua na hayangekua na nguvu kama yalivyo ratibiwa na vijana ambao hawakuzingatia mirengo ya kisiasa 🐒
 
Sawa. Inaonekana haya maandamano hayana kinara wake wa kutoa back up, yakifanikiwa nani atakuwa msemaji wao? Na yakizidi kupata nguvu hayatageuka kuwa ni taasisi fulani iliyo na organisation system?
 
Sawa. Inaonekana haya maandamano hayana kinara wake wa kutoa back up, yakifanikiwa nani atakuwa msemaji wao? Na yakizidi kupata nguvu hayatageuka kuwa ni taasisi fulani iliyo na organisation system?
tunafuatilia kwa ukaribu mno jambo hili, ambalo kwa kiasi kikubwa sana tunaweza sema limefanikiwa, kwamba nani ataliendeleza kutoka hapa lilipoishia na kuelekea uelekeo gan....

mwana blogger David Ndii alitahadharisha mapema sana Serikali ya Kenya juu ya Jambo hili kutokea, lakini pia Jaji Mkuu mstaafu wa Kenya Willy Mutunga yupo mstari wa mbele sana kushauri uelekeo wa vijana...

ni mapema mno kusema nani anaweza kuchukua nafasi ya kua kinara wa kuwaunganisha vijana kwa sasa kwa hatua nyingine zaidi huko mbeleni...

wapo vijana wengi sana wa kuongoza wenzao...

na kwa ushauri wa hao wazee wachache niliowataja, miongoni mwa wazee wengi sana Kenya, vijana wanaeweza kushauriwa kuunganika kwa namna fulani na kuamua mustakabali wao, ama kwa kuchaguana wenyewe huko huko mitandaoni na kupata viongozi wa kubeba sauti na uelekeo wao wa siku zijazo 🐒

let's wait and see,
kama ni kweli vijana wameamua kuupa kisogo na mkono wa kwaheri upinzani ama laa 🐒
 
Huko tanzania kumeanzishwa TK ambayo ina elementi za CCM ingawa inajinasibu si kundi la ccm bali ni la vijana wote. Sasa CHADEMA au CCM wajue kuwa wao hawana tena uwezo wa kubeba maono ya vijana. Vijana hawategemei tena vyama vya siasa kuwapambania, wanajitosa wenyewe from no where kutetea maslahi ya nchi
 
huenda huo ni mwanzo,
but, kujiridhisha na kuthibitisha hilo,

let's wait and see, kama huo muunganiko utahimili influence ya vyama vya kisiasa, serikali, wanaharakati au wadau wa demokrasia 🐒

Otherwise linaweza kusambaratika na kujichuja na kubaki cream ya chama au Taasisi fulani moja, pasipo kua na misingi madhubuti ya kuanzishwa kwake, nia, dhamira na malengo mamoja ya kuwaunganisha vijana wote 🐒
 
Hawa vijana wa UVCCM, BAVICHA, NGOME ACT, CUF VIJANA ni walamba asali wa vyama vyao hawawezi kuchukua hatua bila misukumo ya vyama vyao. Vijana ma hustlers/walalahoi wanaojitambua kama hawa vijana wa kenya
 
Back
Top Bottom