Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

Wakuu mimi sijaelewa, hiyo kodi ni Wapinzani tu au hadi sisi tuliomtukana Lissu kipindi cha kampeni?!
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] mitano tena , na bado , mchakato Wa katiba kubadilishwa ili aongezewe muda , lažima namba isomeke vizuri
 
Sherehe nyumbani na jitu wapi na wapi
Wataanza hadi unyago na ngoma za mashetani
Kwa hiyo nyumbani chakula umejinunulia mwenyewe sokoni

Kuku umewatoa banda kwako la kuku ufanye kasherehe ka mtoto kutoka jando

MC mjomba wa mtoto unaenda dai kodi?

Huo ni uhuni kwa sherehe za krimasi na iddi zinszofanyika majumbani watu wanawake hadi mahema mtafuata kodi?

Watu wakiwa wana sherehe ya kupokea mahari au barua ya uchumba mtaenda? Huo ni udhañimu
Ni jukumu la kila mtanzania kuchangia maendeleo ya nchi yetu tuweke kipaumbele kwenye kulipa kodi kwa kila mzalendo nchi inaendelea kwa kodi na sio vinginevyo lipo kodi kwani mjomba hatakiwi kulipa kodi
 
Na viboko kwanza wamesahau kuongeza apo kodi ya uchafuzi wa sauti kila mtu afunguwe redio sauti ambayo jirani hawezi sikia kabisa wala mtu aliyepo nje kwako liwe kosa la jinai
Mkuu, kuna majirani ni shida....Yaani, anafungulia "Hamsemi yakaisha" kwa sauti ya juu na ni 18/7 maana nikitoka ni huo asubuhi nikirudi ni huo huo jioni. Naunga mkono hoja yako, Mkuu.
 
Yaani hata sisi wa huku "mbavu za Mbwa" tunaoishi chumba kimoja tumeamua kubariki ndoa....tukachangisha kupata ndoo mbili za mbege na kreti mbili za soda na banana kadhaa...Mwenye yumba kajitolea "venue" uwani kwake..Mc ni Mtoto wa Mjomba, Spika na kinasa sauti tumeazimwa na Mchungaji mwenye banda lake hapo jirani analoliita "Kanisa la vuguvugu".

Na sisi tunahusika na hizo kodi ama?
Ndomanake
Lazima ulipe kodi
[emoji23][emoji23]

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Mkuu, kuna majirani ni shida....Yaani, anafungulia "Hamsemi yakaisha" kwa sauti ya juu na ni 18/7 maana nikitoka ni huo asubuhi nikirudi ni huo huo jioni. Naunga mkono hoja yako, Mkuu.
Tufike mahali tuishi kwa taratibu na sio mazoea nina shukuru Mungu ndiko tunaelekea ziwekwe sheria kila mahali ili kila mtu ajuwe haki yake
 
You knew Sengerema was going to set the precedent.

Sometimes wacha yawakute tu aiwezekani watu wajiamulie mambo na sheria ipo; halafu wahusika kwao iwe hewala tu.

Kesho watasema mechi za ndondo cup kuchezwa lazima walipie tozo ya laki moja ili kuwe na kiingilio.

Kikubwa kwao chochote kinachompa mtanzania starehe nchi ambayo wananchi wake wanatakiwa wawe na manung’uniko according global happiness index lazima kiangaliwe upya na kuitoa hiyo furaha maana ilo jambo ni anasa.

Haya ndio madhara ya kuwa na waziri wa fedha asie mwanasiasa na kura za ushindi aziitaji ushawishi; vinginevyo waziri mwingine yeyote asingekubali huu upuuzi.

Mwisho wa siku anaelipa ni wenye sherehe sio mpishi, MC, mwenye ukumbi wala photographer; just pathetic watu wakikubali huu upuuzi.

Mtu mwanawe kafaulu shule, mzazi amefurahi anataka kumfanyia ka part inabidi aachane na hilo wazo maana kuna tozo za halmashauri zinamsubiri; aisee na wananchi wanadhani this is OK ili swala likipita bila makash kash sasa ndio ntaamini watanzania ni kama kondoo.
Nchi hii hawataki watu wawe na furaha, duuuu
 
NI MWENDO WA KUNUNA TU, furaha wanatakiwa wawe nayo viongozi tu, wananchi wote ni majonzi tu, migambo watapiga doria kila kaya wakiongozwa na pua zao zinazonusa harufu nzuri ya pilau,nyama choma nk, masikio yanayosikiliza shangwe na muziki
"au nasema uongo ndugu zangu?"
 
Mbona hili lilisha elezwa na TRA tangu mwaka 2016!

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imesema inafanya utaratibu wa kuhakikisha inawatoza kodi wamiliki wa kumbi za harusi, wapishi na washereheshaji wa sherehe (MC).

Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi wa TRA, Richard Kayombo, alisema wanatarajia kutoza kodi katika sekta hiyo ili kuhakikisha wanaongeza mapato ambayo yatasaidia nchi kupata maendeleo na kuachana na utegemezi kwa wahisani.

Alisema mtu yeyote mwenye vigezo vya kulipa kodi, anatakiwa kujisajili ikiwa ni pamoja na kuchukua namba ya utambulisho (TIN) ambayo itamwezesha kutambulika kirahisi kwenye mfumo wa mamlaka hiyo.

“Kisheria kila mtu au mfanyabiashara anatakiwa kuwa na TIN ambayo itamwezesha kutambulika kirahisi na pia itawasaidia maofisa wetu kuwatambua mahali walipo walipakodi wetu,” alisema Kayombo.

Alisema hivi sasa wapo washereheshaji wanapata kazi na kulipwa kiwango kikubwa cha fedha, lakini hawalipi kodi sambamba na ukodishaji wa kumbi za sherehe.

“Tunajua wapo ma-mc, wapishi wakubwa na hata watu wanakodisha kumbi wanaingiza kiwango kikubwa cha fedha, lakini hawalipi kodi, ni wakati mwafaka nao kuanza kulipa kodi.

“Tunawaomba watupe ushirikiano, hivi sasa unaandaliwa utaratibu mzuri wa kukutana nao kupitia chama chao ili kuwaeleza utaratibu huu mpya ambao utasaidia kujenga nchi yetu na kuwa na maendeleo zaidi,” alisema.

Katika hatua nyingine, mwishoni mwa wiki iliyopita, TRA ilikutana na wamiliki wa maduka ya kubadilishia fedha katika semina ya siku moja iliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwafundisha sheria mpya ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)
 
You knew Sengerema was going to set the precedent.

Sometimes wacha yawakute tu aiwezekani watu wajiamulie mambo na sheria ipo; halafu wahusika kwao iwe hewala tu.

Kesho watasema mechi za ndondo cup kuchezwa lazima walipie tozo ya laki moja ili kuwe na kiingilio.

Kikubwa kwao chochote kinachompa mtanzania starehe nchi ambayo wananchi wake wanatakiwa wawe na manung’uniko according global happiness index lazima kiangaliwe upya na kuitoa hiyo furaha maana ilo jambo ni anasa.

Haya ndio madhara ya kuwa na waziri wa fedha asie mwanasiasa na kura za ushindi aziitaji ushawishi; vinginevyo waziri mwingine yeyote asingekubali huu upuuzi.

Mwisho wa siku anaelipa ni wenye sherehe sio mpishi, MC, mwenye ukumbi wala photographer; just pathetic watu wakikubali huu upuuzi.

Mtu mwanawe kafaulu shule, mzazi amefurahi anataka kumfanyia ka part inabidi aachane na hilo wazo maana kuna tozo za halmashauri zinamsubiri; aisee na wananchi wanadhani this is OK ili swala likipita bila makash kash sasa ndio ntaamini watanzania ni kama kondoo.
Sasa kuna kipi mtafanya😂??? Kama kwenye kura tu mmechezewa sana
na hamjafanya kitu kwa hili kuna kipi mtafanya?
 
Back
Top Bottom