Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

Hata sioni tatizo hapo wanataka muache kupoteza gharama kwenye mambo yanayoweza kufanywa simple na wanaopoteza muda na kufanya mambo makubwa walipe Kodi Ili watengenezewe miundo mbinu na huduma za jamii. Mpaka mbadilike mjue kuishi Kama ulaya mambo ya kupoteza muda Kama mnayo mlipie Kodi.
 
You knew Sengerema was going to set the precedent.

Sometimes wacha yawakute tu aiwezekani watu wajiamulie mambo na sheria ipo; halafu wahusika kwao iwe hewala tu.

Kesho watasema mechi za ndondo cup kuchezwa lazima walipie tozo ya laki moja ili kuwe na kiingilio.

Kikubwa kwao chochote kinachompa mtanzania starehe nchi ambayo wananchi wake wanatakiwa wawe na manung’uniko according global happiness index lazima kiangaliwe upya na kuitoa hiyo furaha maana ilo jambo ni anasa.

Haya ndio madhara ya kuwa na waziri wa fedha asie mwanasiasa na kura za ushindi aziitaji ushawishi; vinginevyo waziri mwingine yeyote asingekubali huu upuuzi.

Mwisho wa siku anaelipa ni wenye sherehe sio mpishi, MC, mwenye ukumbi wala photographer; just pathetic watu wakikubali huu upuuzi.

Mtu mwanawe kafaulu shule, mzazi amefurahi anataka kumfanyia ka part inabidi aachane na hilo Waco maana kuna tozo za halmashauri zinamsubiri; aisee na wananchi wanadhani this is OK ili swala likipita bila makash kash sasa ndio ntaamini watanzania ni kama kondoo.
Usisahau ile mbinu ya awamu hii 'Tengeneza tatizo,kisha litatue".Usishangae Mkulu akatengua siku mbili na kama mazuzu tukashangilia tena kwa nguvu!
 
Duh! Wananchi tuliambiwa tutambue haki yetu na nguvu tuliyonayo katika kuiwajibisha serikali lakini wapi, tumejawa na uoga, unafiki na kutengenezeana majungu katika mambo yasiyokuwa na msingi.
Mitano teeeena au nasema uongo jamani?
 
Kwa hiyo nikiwa na sabuhufa yangu nikawa napiga nyimbo za taaratibu huku nikifurahi na familia yangu na ndugu walionitembelea kunipongeza kwa kufanikisha jambo muhimu wakati huo huo tunakamatia ubwechwe, na mnuso wa nguvu! Kuna uwezekano Askari wa akiba wakatushika 'tanganyika jeki'😳😳😳😳
Na viboko kwanza wamesahau kuongeza apo kodi ya uchafuzi wa sauti kila mtu afunguwe redio sauti ambayo jirani hawezi sikia kabisa wala mtu aliyepo nje kwako liwe kosa la jinai
 
This is hogwash to say the least......

Kwahio kama DJ/MC kapata shughuli ya kulipwa elfu 25 au 10 kwa siku, itabidi atoe kwenye mfuko wake kulipa hio difference..., Au wanataka kusema profit kwa kila kazi kwa hawa watu zinazidi hizo kodi, in short kwa shughuli yoyote mtu inabidi aweke kando 180,000/ kwa ajili ya kodi no matter kama ametumia cost ya laki mbili au bilioni mbili ?
Techinically kuna impact mbili hapo,
1) Kuna ma mc wadogo wataacha hiyo kazi maana costs zitakuwa kubwa kwao kumudu ukizingatia ujira wao.

2) Wale wakubwa watapeleka bei kwa mlaji ambayo kwa kiasi itaongeza gharama za u MC.

Kwa ufupi hii policy ita discourage zaidi, wenye vile visherehe vidogodogo
 
This is hogwash to say the least......

Kwahio kama DJ/MC kapata shughuli ya kulipwa elfu 25 au 10 kwa siku, itabidi atoe kwenye mfuko wake kulipa hio difference..., Au wanataka kusema profit kwa kila kazi kwa hawa watu zinazidi hizo kodi, in short kwa shughuli yoyote mtu inabidi aweke kando 180,000/ kwa ajili ya kodi no matter kama ametumia cost ya laki mbili au bilioni mbili ?
Mimi nafurahia sana haya mambo Sababu watz wengi bado hawajajitambua

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Huo ujinga ni Dar tu au na mikoani pia?
IMG_8413.JPG
 
Ni sawa kabisa! Unakuta sherehe kwa mfano ya harusi au sendoff watu mnachangishwa kila kichwa elfu hamsini mpaka laki moja,!

Unakuta sherehe moja tu ina gharimu mpaka milioni 10.

Unakuta kwenye bajeti ya sherehe eti
Mapambo milion 1.5
Ukumbi milion 1.2
Mc na music milioni 1.8
Picha na video milioni 1.6
Vinywaji milioni 1.7
Chakuala milion 4

Na hizi ni sherehe tu za uswahilini bado za ushuani ndio balaa

Unakuta mtu ana maisha magumu lakini akipewa kadi ya mchango anajipinda mpaka ipatikane, tena wanakuwekea masharti kabisa single 80,000 double 150,000.


Tena hili suala lilialamikiwa sana humu kwama ifike hatua hawa watu walipe kodi.

Walipe tu kodi aisee.

Hivi we unajua kwamba kumbi za sherehe zinalipa kodi. Hao ma MC wote unaowaona wamesajiliwa na wanalipa kodi.
 
Sherehe nyumbani na jitu wapi na wapi
Wataanza hadi unyago na ngoma za mashetani
Kwa hiyo nyumbani chakula umejinunulia mwenyewe sokoni

Kuku umewatoa banda kwako la kuku ufanye kasherehe ka mtoto kutoka jando

MC mjomba wa mtoto unaenda dai kodi?

Huo ni uhuni kwa sherehe za krimasi na iddi zinszofanyika majumbani watu wanawake hadi mahema mtafuata kodi?

Watu wakiwa wana sherehe ya kupokea mahari au barua ya uchumba mtaenda? Huo ni udhañimu
Lipa kodi mzee
Serikali iko sawa kabisa kudai kodi hapo
Tena itakuwa vizuri walete kabisa kodi ya kichwa

Ova

Sent from my SM-N920T using JamiiForums mobile app
 
Tunakoelekea hadi watembea kwa miguu watalipia kodi.Fursa hiyo kwa TANIRODI.
Dereva naomba niteremke nishafika kituo changu tafadhali.
 
Ni sawa kabisa! Unakuta sherehe kwa mfano ya harusi au sendoff watu mnachangishwa kila kichwa elfu hamsini mpaka laki moja,!

Unakuta sherehe moja tu ina gharimu mpaka milioni 10.

Unakuta kwenye bajeti ya sherehe eti
Mapambo milion 1.5
Ukumbi milion 1.2
Mc na music milioni 1.8
Picha na video milioni 1.6
Vinywaji milioni 1.7
Chakuala milion 4

Na hizi ni sherehe tu za uswahilini bado za ushuani ndio balaa

Unakuta mtu ana maisha magumu lakini akipewa kadi ya mchango anajipinda mpaka ipatikane, tena wanakuwekea masharti kabisa single 80,000 double 150,000.


Tena hili suala lilialamikiwa sana humu kwama ifike hatua hawa watu walipe kodi.

Walipe tu kodi aisee.
Basi wazilenge hizo za mamilioni.
 
Harusi yangu itafanyika kwenye ukumbi uliopo Kambi ya Twalipo Mtoni Sabasaba. Hao mgambo waje "kunusa" hapo!
 
Yaani hata sisi wa huku "mbavu za Mbwa" tunaoishi chumba kimoja tumeamua kubariki ndoa....tukachangisha kupata ndoo mbili za mbege na kreti mbili za soda na banana kadhaa...Mwenye yumba kajitolea "venue" uwani kwake..Mc ni Mtoto wa Mjomba, Spika na kinasa sauti tumeazimwa na Mchungaji mwenye banda lake hapo jirani analoliita "Kanisa la vuguvugu".

Na sisi tunahusika na hizo kodi ama?
 
Back
Top Bottom