Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

Temeke, Dar: Ili upige muziki kwenye sherehe/shughuli utapaswa kulipia elfu 50 ya kibali

ccm nambari one na MAZWAZWA yatakenua na kuimba kwa furaha. Chanzo cha haya yote ni huyo dikteta baada ya kuamua kupora vyanzo vyote vya mapato ya halmashauri za Wilaya nchini.
Bahati nzuri sana hiyo namba tunaisoma nao. Japo wenzetu ni wanafiki mpaka basi, kwa hili wanaweza kumpongeza na akilikemea wakampongeza tena!
 
Hii nchi tunakoelekea sijui aiseeee mi birthday yangu nyumbani kodi ya nini kwani birthday ni biashara

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hili tango pori, barua yenyewe inajieleza. Hakuna upuuzi kama huu hata kuandamana tutaandamana tu hamna namna. North Sudan na ubabe wote wa Bashir wanaandamana kwa sababu ya mkate kupanda bei. Too much drama done with this regime mkuu!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hawa wakurugenzi wangaliwe vizuri akili zao hivi kweli mmeshindwa kuwezesha watu wafanye kazi mkusanye kodi? Kipaimara kinachofanyika nyumbani kwangu mm nilipe kodi? Huko kwenye kumbi za maharusi sawa daini maana kumbi zinakodishwa.
Tatizo la serikali ya kimagumashi hilo mwendawazimu
 
IMG-20190125-WA0089.jpg

Kiwango hicho cha tozo kitaanza kutozwa tarehe 01 Februari, 2019. Kibali hiki ni kwa watakaotaka kupiga muziki kwenye Bar, Pub, au ukumbi wa starehe

Lakini pia kitawahusu wanaotarajia kupiga muziki kwenye send-off, harusi/ndoa, jando na unyago na birthday

Aidha, kibali hiki kitapaswa kukatwa kwa watu wote watakahitaji kupiga muziki kwenye shughuli nyingine zote zinazofabana na zilizotajwa
 
Aisee

Kila goti litaguswa

Hiyo ipo kwenye kipengele gani cha matakwa nchini?
Ilipitishwa na akina nani? Maana mwandikaji hajaandika hata kipengele cha kuonyesha ni sheria sijui nini.
Pesa hizo zinatozwa kufanyia nini?
Na kwanini wanatoza wananchi.. mtu akikaa kwake kutaka kufurahia na ndugu na jamaa kuondoa mastresi ndio aanze kupiga picha kuchajiwa na serikali kwanza?

Kuna mengi kwenye wilaya zz nchinu bado ni majanga.. uchafu, kuelimisha wananchi mengi n.k.

Hivi wale akina Mama wanaofagia barabara kila siku kweli hakuna kazi zingine za kuwapatia na kuachia vigari vya kusafisha nakuvuta michanga ikafanya hayo.. pesa za kununua hakuna kweli!! au ndio kulipa wamama pesa ndogo kuwatesa tu kwenye jua.
 
Back
Top Bottom